mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,248
- 4,687
Mufti amesema hayo katika Sherehe za Maulid ya Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Kalangalala Mjini Geita ambapo maelfu ya Waisalmu wamehudhuria akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini.
Mufti amesema “Mtume alikuwa Mtu wa subra, alikuwa Mtu wa pole, alikuwa akifundisha amani, Mungu alimtayarisha akawa ni Mtu wa namna hiyo hakufanya mambo ya kipuuzi hata siku moja”
Soma Pia: BAKWATA yatoa tamko kuhusu joto la utekwaji na mauaji
“Na Mungu ametueleza katika Quran juu ya masuala ya amani ni ajabu Umma huu leo ikawa hawa ndio wanaovunja amani wao ndio wanaoharibu ulimwengu, msilete uharibifu, msieneze uharibifu katika Nchi, Mungu ametukataza na Muislamu hatakiwi kila jambo ambalo linafanywa na anafanya na yeye”
“Tusisumbuliwe na Watu, kikundi au fikra za baadhi ya Watu kwa makusudio yao au zile mambo wanayokuwa nayo, rudi katika uislamu, je, uislamu unaniamlisha Mtume kasema yafaa kufanya jambo hili ?, haiwezekani Muislamu unaambiwa jambo unakwenda unauharibu uislamu na unatoka katika mafunzo ya uislamu na uislamu hauko huko, Muislamu ndio Mtu wa kwanza kuchunga mazingira, usiwe kama Mtu ambaye ana tabu ya afya ya akili, sasa unaona Watu wanapita barabarani wewe unaingia ‘eeh hatukubali Bwana’ haukubali nini sasa!?”
“Tutumie akili zaidi, Muislamu haambiwi jambo halafu anakwenda, anaanza kufikiri, ukiambiwa jambo unalitia katika mizani kwanza kisha ndio unakwenda, sio unaambiwa jambo unakwenda tu ‘hatutaki hatutaki’ asili yake unaijua?, lazima tulinde amani Nchini hatuna Nchi nyingine Nchi yetu ndio hii, tusisumbuliwe na fikra za Watu au kikundi cha Watu, jiulize hakuna mambo mengine hapa?, lakini Muislamu unaambiwa jambo unakwenda unauharibu uislamu”