Mufti awataka waislamu kuacha MAJUNGU

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,080
103,312
Katavi. Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Katavi wametakiwa kuacha tabia ya kupigana majungu kuchafuana wao kwa wao badala yake washirikiane kwa pamoja kudumisha mshikamano, umoja na upendo.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 5 na Mufti Mkuu wa Tanzania, Shekhe Abubakar Bin Zuberi amebainisha hayo leo Jumatatu Oktoba 05, 2021 akiwa ziarani mkoani Katavi wakati akihutubia umati wa waislaamu kwenye Msikiti wa Ijumaa uliopo Manispaa ya Mpanda.

“Hatuwezi kupata maendeleo yeyote tusipokuwa na umoja pamoja na mshikamano. Uupweke ni adhabu ukiwa peke yako tu hushirikiani na wenzako, utakosa mambo mengi ambayo ungeyapata kwa wengine,” amesema Mufti.

“Kwahiyo tusijengeane chuki tuambiane kuna jambo halijakaa vizuri lieleze vizuri usikae kando kando kusema sema kwenye vijiwe. Musilaamu hazungumzi kandokando anazungumza waziwazi au moja kwa moja,” amesema Mufti.

Akiwa mkoani Katavi amezindua mradi wa ujenzi wa ofisi ya Bakwata, Mkoa uliogharimu zaidi ya Sh25 milioni zilizotokana na sadaka za waumini, michango ya wadau na serikali.

Pia ametembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya Bakwata Wilaya ya Mpanda, shule ya msingi iliyopo msikiti wa Kasimba pamoja na shamba la korosho lilipo Kakese.
 
Hayo ni kawaida kwa viongozi wa DINI kuwausia waumini wenzao.

Kwani DINI ni kukumbushana na kuusiana.

#SiempreJMT
#NchiKwanza
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Wewe Zuberi enzi za Magufuli ulikuwa mnafiki na majungu kibao.
Tena ulikuwa muongo unasema eti siku Magu anakata roho wewe na Pengo mlikuwepo?! Hamjui hata tarehe aliyokufa, ile maiti imefichwa wiki mbili nzima nyie mnasema mlikuwepo!
 
Ohoooo
 
76.gif
 
Kimeumana walikuwepo kumbe wanasema hahahaha bongo hatari Sana waziri mkuu yeye akatoa boko Zaid

SSH akasema vimafua tu msiwe na waswas

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Katavi. Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Katavi wametakiwa kuacha tabia ya kupigana majungu kuchafuana wao kwa wao badala yake washirikiane kwa pamoja kudumisha mshikamano, umoja na upendo.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 5 na Mufti Mkuu wa Tanzania, Shekhe Abubakar Bin Zuberi amebainisha hayo leo Jumatatu Oktoba 05, 2021 akiwa ziarani mkoani Katavi wakati akihutubia umati wa waislaamu kwenye Msikiti wa Ijumaa uliopo Manispaa ya Mpanda.

“Hatuwezi kupata maendeleo yeyote tusipokuwa na umoja pamoja na mshikamano. Uupweke ni adhabu ukiwa peke yako tu hushirikiani na wenzako, utakosa mambo mengi ambayo ungeyapata kwa wengine,” amesema Mufti.

“Kwahiyo tusijengeane chuki tuambiane kuna jambo halijakaa vizuri lieleze vizuri usikae kando kando kusema sema kwenye vijiwe. Musilaamu hazungumzi kandokando anazungumza waziwazi au moja kwa moja,” amesema Mufti.

Akiwa mkoani Katavi amezindua mradi wa ujenzi wa ofisi ya Bakwata, Mkoa uliogharimu zaidi ya Sh25 milioni zilizotokana na sadaka za waumini, michango ya wadau na serikali.

Pia ametembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya Bakwata Wilaya ya Mpanda, shule ya msingi iliyopo msikiti wa Kasimba pamoja na shamba la korosho lilipo Kakese.
Mufti anataka kutenganisha uislamu na majungu?!
 
Back
Top Bottom