Kumekuwa na matukio ya ajali kila uchao pasipokuwa na dalili zozote za lini hizi zaweza au angalau kupungua. Palikuwa na haja ya kujitathmini vilivyo kwani yawezekana sababu halisi za haya twajaribu kuzikwepa na pengine mbaya zaidi ni kwa maslahi binafsi.
Angalia hawa hapa:
Wanahabari wapata ajali msafara wa JPM
Haiwezekani kuwa tunagharimiwa na haya yafuatayo (however unpalatable they may be)?:
1. Impunity: - yaani sheria za barabarani ni kwetu sisi kina yakhe si kwa hawa wa misafara ya vigogo na wakubwa (aka wazito) kama wale tuliowashudia siku za karibuni ajalini?
2. Vipi kuhusu stress (aka misongo ya mawazo) kutokana na adha za hawa waliojiwekea malengo ya kukusanya mapato tokea katika makosa bambikizi ya kutafuta yasiyokuwa hata na athari yoyote kwa jamii. Makosa ambayo aghalabu huyatafuta hata ya mithili ya kumulika kwa tochi ili mradi tu zile bilioni za malengo yao zitimie?
3. Vipi miundo mbinu ya barabara ambaye mwajibikaji ndiyo kajikita kwenye makusanyo kama ilivyo hapo #2?
4. Vipi kujitenga kutoka kwa wadau wanaohusika barabarani kwa mamlaka na kujikita katika matamko yasiyo na mashiko? Mara madereva waende shule - - kwenye hili shule wao hawajaenda wala curriculum za huko shule hawazijui achilia mbali tija ya shule zenyewe kuzifahamu.
Eeh mola wetu hebu na utunusuru sisi waja wako na hawa mamba watu waliao machozi eti ya kutuhurumia siye hali kiuhalisia hawana chembe yoyote ya nia ya kumaliza tatizo hili.
Iko kama vile wakuu hawa wamekula yamini ya kujikusanyia mapato at the expense of our blood.
Pathetic.
Eeh mola wetu pokea dua zetu sisi tulio marehenu watarajiwa tuliowekwa rehani kwa sababu ya njaa zao.