Muendelezo Kuhusu CCTV

Muendelezo Kuhusu CCTV

Mnyongeni Mnyonge

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2015
Posts
628
Reaction score
731
Habari ndugu zangu wana JF baada ya kuwapatia salamu za heri kwenu naomba niendelee na kile nlichokianzisha elimu kuhusu CCTV.

Aidha kwenye topic iliyopita tuliweza kujifunza habari kidogo kuhusu CCTV aina muundo ufanyaji wa kazi ila kwa hapa ntakupa muendelezo mdogo ambao utakusaidi kung'amua umuhimu wa CCTV ukiweka sehemu yako ya biashara,nyumbani au ofisini.

Katika mada iliyopita tuliweza kuona aina mbili za CCTV ambazo tulisema zipo za IP Camera na Zipo Za HD/analogy camera kwa kutumia mifumo hii yote ya camera unaweza kufanya nyumba yako kuwa salama wakati wote,kusimamia monitoring biashara yako na hata kujua nn kinaendelea nyumbani kwako.

Swali je ni kweli muda wote unatakiwa uwe macho kuangalia nn kinafanyika kupitia mifumo yako ya CCTV unayokuwa umeiweka?? Jibu ni laa unaweza kufanya hivo kama utaajiri mtu maalumu ambaye yeye all the time anaangalia mfumo huo au unaweza kufanya mwenyewe kutumia mifumo ya internet kuweza kufanya hilo.

Teknolojia imetusaidia hilo kwa maana ya kuwa unaweza safiri nje ya nchi au mbali na eneo unalotaka kuliangalia hivo kwa kutumia mfumo wa network unaweza kuangalia cctv zako kupitia simu yako ya mkononi smartphone ili mradi sehemu uliyopo unapata mawasiliano ya internet na cctv yako ikiunganishwa kwa internet hilo ni suala jepesi tuu kwenye teknolojia hakishindikani kitu.

By the way watu watajiuliza je unatakiwa uwe unaangalia simu yako kila mara kujua kinachotendeka pale sehemu husika jibu ni jepesi kuna mfumo unaitwa GSM alarm System mfumo huu unaweza kukupa taarifa kwa kukupigia simu au kutuma meseji kukujulisha kuwa hapo kwenye ofisi au nyumba au sehemu ya biahsara kuna tukio linalotokea ambalo uangalizi wako ni muhimu na ww utaweza kuchukua hatua utazoona ni stahiki.

Hilo ni kwa ufupi somo kuhusu GSM alarm system litakujia soon hapa hapa kwa maelezo ya kina na yenye tija.

Ahsanteni
FB_IMG_1541679759458.jpg
IMG_20180408_234347_505.jpg
 
Teknolojia imetusaidia hilo kwa maana ya kuwa unaweza safiri nje ya nchi au mbali na eneo unalotaka kuliangalia hivo kwa kutumia mfumo wa network unaweza kuangalia cctv zako kupitia simu yako ya mkononi smartphone ili mradi sehemu uliyopo unapata mawasiliano ya internet na cctv yako ikiunganishwa kwa internet hilo ni suala jepesi tuu kwenye teknolojia hakishindikani kitu.

Hapo ...je kama upo mbali na office internet haisomi eneo la biashara bado nitaweza kuona matukio ?au ndio hadi internet ikae sawa?
 
Hadi internet iwepo ili uweze ku link na simu yako
 
Kiongozi vijana wa Saloon ya kunyoa wanatusumbua saana...naweza funga hizi Camera zikasaidia kuangalia idadi ya watu wanaoingia kupata huduma ....Gharama zake zikoje ?Tuanze na ya bei ya chini ya kabisa!
 
Mkuu hebu nitajie full package ya cctv installation vitu muhimmu vinavyohitajika, kwa mfano nikitaka kuanza na camera 4( 1mp)@1
Dvr yenye hard disk
Cable cat 6 au coaxial
Camera nne
Router kama unataka kufanya remote access
Power pin,bnc au video baluni,waterproof box,power supply au power adapter,trunkin au conduit pipe,data cabinet 4u
Hapa kazi yako itakuwa safiiiii
 
Hpo roughly budget inaweza fika ngapi kibongo bongo?
 
Back
Top Bottom