Muda wa mapacha watatu umewadia...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Baada ya kurejeshwa kwa chenji ya Rada nchini ambayo imepangwa 'kununulia' madawati,muda umefika kwa mapacha watatu-EL,AC na RA kushughulikiwa.Taarifa zilizonifikia zinabainisha kuwa wakuu wa nchi walikuwa wakisubiri kurejeshwa kwa chenji ili kila pacha awe na jambo lake linaloonekana wazi mbele ya wananchi.

Wakati EL akihusishwa na Richmond-Dowans,RA hatoki kwenye Dowans na KAGODA;AC anakabwa koo na Rada.Kwa mpangilio huo,taarifa zinadai,hakuna atakayesalimika.Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi tayari alishakabidhiwa mafaili ya mapacha watatu.Ni muda wake muafaka sasa kuchukua hatua.Rais wetu Kikwete na asimwingilie.

Picha inaanza..
 
Sidhani kama kuna haja ya kuendelea na upelelezi wakati ushahidi wote upo..yaani ni fungua kesi, kamata, hukumu, weka lupungo..kazi kubwa iliyobaki sasa ni kufikiria ni miaka mingapi wakae lupango..i suggest 30yrs.
 
Kikwete si ameapa kuilinda katiba bila woga wala upendeleo? Rais hamwogopi mtu...
 
Day dreaming! Lowassa hahusiki na Richmond [ rejea kauli yake aliyoitoa kwa JK kwenye kikao cha NEC Dodoma, haijawahi kukanushwa].
 
Day dreaming! Lowassa hahusiki na Richmond [ rejea kauli yake aliyoitoa kwa JK kwenye kikao cha NEC Dodoma, haijawahi kukanushwa].
Mbona umemsemea Lowassa tu? Kwa taarifa yako,Lowassa ni fisadi aliyetukuka,msanii wa Shahada..
 
Mapacha wana mboga kikwete ana ugali ukimwagaa tu na mimi namwagaa... katika mchezoo hakuna sadakalawe.
 

Wewe ni msemaji wa Mahakama na unawezaje kufikiwa na taarifa hizo? kama nani yaani. Ni vyema na wewe ukachunguzwa kwa kuingilia vyombo ya dola.
 
Wewe una shahada ya madrassa! Hakuna wa kumzuia Lowassa kuingia ikulu 2015.

Mkuu hebu tuambie atatumia mbinu gani iliyokufanya uamini kuwa Lowassa kuingia ikulu 2015?
 


Kwa mfumo tulionao wa kutizama matumbo yetu hakuna hatua yoyote itakoyochukuliwa hapo
 
Aliapa na kuitetea katiba kwenye kitabu tu mkuu! Kikwete is not the man of action at all!
Mali bila daftari hupotea bila kujua. JK bab kubwa, wasiyomkubali ni majungu yao tu. Katika changamoto hizi za kidunia JK kajitahidi sana, na sioni mwingine wa kuweza kkabiliana na changamoto kama za mtiksiko wa uchumi duniani, mabadiliko ya kisiasa, majanga yasiyo ya kujitakia kama Mafuriko, ujambazi, uhuru wa vyombo vya habari uliopita kiasi na mengine mengi. Hebu tusubiri hiyo 2015 then atakayekuwa amechukua nchi tuone kama hataomba kuondoka pale magogoni.


KILA LA HERI JK kuelekea kutupatia Katiba Mpya.
 
Eliezer Feleshi? Hawezi kumshughulikia msukuma mwenzake AC atawaweza EL na RA? Na hawa huwezi kuwashughulikia labda uanze na JK!
 
Under the leadership of kikwete, forget about that point! Labda kikwete awe ametoweka dunian!
 
Wewe ni msemaji wa Mahakama na unawezaje kufikiwa na taarifa hizo? kama nani yaani. Ni vyema na wewe ukachunguzwa kwa kuingilia vyombo ya dola.
JF tupo wa kila aina humu.Take care!
 

Hizo ni ndoto za alinacha. Hilo la kuwashitaki hao mabwana halitakuja kutokea kamwe. Inaonekana wewe huujui huu mfumo vizuri, hakuna anayeweza kumshughulikia mwenzake hata siku moja. Ngoja mpaka 2015 nguvu ya umma itakapoingia madarakani.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…