Mbona tunawaamini ccm haraka kiasi hiki? Haya magamba yametoka wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona tunawaamini ccm haraka kiasi hiki? Haya magamba yametoka wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Apr 20, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Naomba kusahihishwa kama nitakuwa nimepotoka, maana sielewi kitu kuhusiana na baadhi yetu kutaka CCM ipongezwe kwa kujivua magamba na wengine kudai sasa CDM inatumiwa na mafisadi dhidi ya CCM ya JK yenye gamba jipya eti kwa kuwa imetaja mafisadi wapya.

  Ninavyojua, hapa nchini ufisadi umekuwepo siku nyingi na umekuwa unaongezeka kila siku zinavyosonga. Baada ya CDM kuanza kupiga kelele kuhusiana na swala hili kwa kuwataja baadhi ya vigogo na namna wanavyohusika kulipora taifa takribani CCM nzima ilikanusha kwa nguvu zote (Hata Sitta anayeonekana mpiganaji leo alithubutu kumwita Dr.Slaa mzushi au jina kama hilo).

  CCM wengine walianza kupiga kelele walipogundua ushahidi ni mkubwa na mgao wao haukuendana na walichopora wanamtandao wenzao. Ki-msingi kelele za Sitta na wapiganaji wenzake wengi ndani ya CCM ni chuki dhidi ya kupunjwa na si kweli kwamba wanachukia ufisadi kiasi hicho. Labda swala zaidi ni tabia ya RA kupenda kuwatesa asiowapenda kwa kutumia fedha ambazo wanajua anakozipata hasa katika kugombea nafasi za uongozi.

  WanaJF kumbukeni kauli ya Lowasa wakati anaachia ngazi "... Tatizo ni U-waziri mkuu...." Kuna uvumi kwamba wakati wanapanga mikakati ya kuingia madarakani kuna watu waliahidiwa vyeo na baadaye wakapewa watu tofauti. Ndiyo maana hata baraza lilikuwa kubwa mno. Jamaa walitaka kugawana matunda ya kazi yao.
  Ukifuatilia kwa undani utagundua CCM wengi ni watafuta fedha tu wakigawana fedha za Dowans vizuri na kukubaliana namna ya kila mmoja kula hakuna atayepinga ufisadi wala kujinadi kama mpiganaji. Kwa bahati mbaya sana watanzania wengi tupo hivyo.

  Si nia yangu kukumbushia yanayoeleweka tayari hivyo, naomba nigusie hasa hili swala la juzi linalonadiwa na CCM kama kujivua gamba ili kurejesha hadhi yake miongoni mwa wananchi. Mabadiliko ambayo yapo wazi ni kwamba kwa sasa jamaa zetu wameteua Sekretarieti mpya na Kamati Kuu mpya ambayo haiwashirikishi Rostam, Chenge na Lowasa.

  Hawa "Mapacha Watatu" hawajafukuzwa NEC wala uanachama wa chama hicho na hakuna kiongozi aliyewataja hadharani wala katika taarifa rasmi kwamba hao jamaa wanaondolewa katika chama na kwa tuhuma zipi? Lakini cha ajabu watu kibao wanapiga kelele kweli kuhusu magamba utadhani kweli chama kimebadilika. Cha ajabu kabisa Zakhia Meghji aliyedai fedha zilizochotwa na KAGODA zilitumika kwenye maswala ya usalama wa taifa kateuliwa ndani ya nyumba. Je kuna tofauti na kumwacha Rostam mwenyewe? Wadanganyika wanachekesha!

  Tunaolalamikia Chama Cha Mapinduzi kugeuka Chama Cha Mafisadi tulilaumu pia rais JK kuonekana kuwakingia kifua waziwazi mafisadi wakubwa wasibanwe na sheria. Mnakumbuka ile ya EPA ya kurejesha fedha lakini kutoshtakiwa. Ndo kusema walilipwa kimakosa au waligushi ili walipwe? Katika makosa haya kama kuna gamba la kuvuliwa ni JK na wote katika Baraza lake la Mawaziri endapo walihusika kuamua kauli hiyo ya rais. Aliyedai hawajui DOWANS pamoja na kuwa na vyombo vyote vya kiuchunguzi ni nani kama si "Mzee Sijui" JK mwenyewe? Hata hapo bado mnaamini CCM wamejivua gamba?

  Mwenyekiti wa CCM rais JK amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza miradi ya RA na EL dhidi ya wabaya wao kama Sitta, Selelii na wengineo. Tuwe wakweli jamani! mradi wa kumwondoa Sitta katika kugombea uspika tena dakika za mwisho pasipo kumpa taarifa ulikuwa unamnufaisha nani kama si mafisadi? JK (wanadai) yeye ni msafi ila wasaidizi wake ndo si wasafi sasa kwa nini amwogope na kumwondoa Sitta kwenye uspika na kutusababishia vurugu za Bi. Kiroboto ambazo hata hatujui zitamalizika vipi? Guys, I tell you Ngojeni awamu ya nne imalize muda wake ndipo mtasikia mambo ya JK mpaka mchoke. Kwani nani alijua Mkapa angeanikwa kiasi hicho katika kupora nchi.

  Kwangu mimi yeyote katika CCM, anayewaita RA, EL na Chenge magamba yaliyovuliwa ningependa ataje wazi tuhuma zao ili tuone kama zinafanana na tunazozijua wananchi na kama kweli wamejivua na kashfa zote au la. Pia tupewe Road Map ya kuwafikisha mbele ya sheria. Kama kumwondoa Sitta ilikuwa mbinu ya mafisadi aka magamba basi, wajivue na hilo pia.

  Naomba kuwaasa watanzania wote wanaokusudia kuibadili nchi hii wakumbuke kwamba CCM kurejesha hadhi yake miongoni mwa wenye akili ni kazi kubwa ambayo mpaka sasa haijaanza. Tutumie kila kilicho ndani ya uwezo wetu kuhakikisha ama CCM inaondoka madarakani au uongozi mzima wa chama hicho cha kifisadi uachie ngazi pasipo kumsahau "Mzee Sijui" maana matatizo yote ni kukosa kwake sauti na msimamo wa kiongozi madhubuti. Utabembeleza watuhumiwa halafu utake watu wawalaumu wao wakati madaraka unayo wewe?

  Hata walioipa TICTS mkataba juu ya mkataba na kuifanya Bandari kudorora waliongozwa na Mwenyekiti wa CCM ndani ya Baraza la Mawaziri. Naomba wapenzi wa CCM mlioamua kujipofusha maksudi na kuziba masikio muwambie viongozi wenu mimi bado sijadanganyika na mchezo wao wa sasa (Mungu anijalie uwezo zaidi) nitatumia kila niwezalo kuhakikisha wote ninaoweza kuwafikia wanaelewa mzaha uliopo katika karata yenu hii ya gamba.

  Siwezi kuandika yote katika thread hii lakini angalieni hata kauli za viongozi wapya wa CCM kama Nape. Hawa jamaa badala ya kuwaza kukisafisha chama chao kikweli wao wanachofurahia ni kuona uongozi umeondolewa kwa watu ambao wao wanadhani waliwadhulumu madaraka na mali za uporaji wanazoamini ni haki yao wote kwa pamoja.

  Sijui hata ni kwa nini watu wanashawishika kuwaamini haraka kiasi hicho maana amini mtu yeyote lakini usiamini utakachaambiwa na CCM dhidi ya ufisadi maana kama si uongo basi ni usanii na kama si usanii basi ni utapeli wa waziwazi. Ushauri wangu ni kwamba angalieni kitakachofanyika baada ya miezi mitatu ndiyo muamini maneno yangu. Hawafukuzani wala nini maana wote ndiyo hao hao. Tofauti ya RA na JK ni kwamba mmoja alifanikisha wizi na kumfadhili mwenzie ili ashike dola kwa niaba yake. Tofauti ya EL na JK ni kwamba EL ni mkali wazi wazi wakati JK anafinya kimyakimya huku akitabasamu lakini mwisho wa siku utagundua wote magamba tupu!

  Narudia tena watanzania msidanganyike na watu hawa hadi mtakaposikia wamefukuzwa katika chama na kufikishwa mahakamani kwa uharamia wao dhidi ya mali zetu tena wote Chenge, Karamagi, Rostam, JK, EL na vikaragosi wao wengi tu pasipo kumwacha mtu.

  Kuwepo kwa Spika Kimeo ni magamba yao kwani walidhani mambo yatapoa akiondoka S.Sitta.
   
Loading...