Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 39,564
- 91,860
MATUNDA YA DEGREE ZETU NI MUDA KUYAONYESHA.
Na, Robert Heriel
Nafikiri huu ndio wakati uliosubiriwa kwa kipindi kirefu, wakati wa kuliinua taifa hili katika nyanja zote za maisha, kiuchumi, kijamii, kisiasa, na kiutamaduni.
Kama taifa hatuwezi kufikiri jambo moja wakati wote, kufikiri jambo moja ni ishara mbaya katika kulijenga taifa hili. Taifa linapaswa lijengwe katika misingi ya kufikiri na kujikita katika mambo mbalimbali. Ikiwa taifa litajikita katika jambo moja litatengeneza vijana wanaofikiria jambo moja tuu pekee. Na hii ndio hatari zaidi kwa nchi kwani itasababisha nchi kuwa tegemezi na yenye utumwa mamboleo.
Tumesoma, tumeelimika, tuna mavyeti ya kila aina; Nikijitolea mfano, ninavyeti visivyopungua kumi vya kozi mbalimbali, hii ni kusema nina ujuzi na elimu wa aina mbalimbali, udereva mimi, basic computer mimi, monitoring, evaluation na management mimi, Ualimu mimi, Uandishi mimi, teolojia mimi, Marketing and selling mimi, Develepment Study mimi, Ufundishaji Kiswahili kwa wageni mimi, miongoni mwa mambo mengine.
Sio mimi tuu wapo vijana wenzangu wengi tuu wamesoma, wengine welding, wengine Tour Guide, Photographer, Muziki, uhasibu, injinia, uanasheria, Utabibu, Ulinzi, Usekretari miongoni mwa mambo mengine.
Kwa kiasi cha kati, watanzania wengi tunaelimu na ujuzi wa fani mbalimbali, ni lazima kwanza tujivunie na tujipongeze kwani hiyo tosha ni hatua kubwa kama taifa. Huu ni muda wa kuonyesha elimu zetu katika jamii zetu, ni wakati wa jamii zetu kula matunda ya elimu zetu.
Taifa hili linafursa nyingi mno, najua sio kila mtu anaweza kuziona, lakini lipo kundi la vijana wachache wanamacho ya kuchungulia fursa zilizopo ndani na nje ya nchi. Hatuwezi ku-limit akili zetu, kuzi-limit akili zetu ni kuathiri maendeleo yetu, kila kitu ni muhimu ndio maana kipo, kila kitu chafaa kwa matumizi kama sio kwetu basi kwa wengine kwa kuzingatia sheria za taifa letu, miiko ya tamaduni zetu na sheria za dini zetu.
Lazima tutumie kila kilichopo kujinufaisha sisi wenyewe kama nchi. Ubora wa taifa unajengwa katika kutumia rasilimali zilizopo kujenga maisha ya wananchi wa tabaka zote. Na zile Rasilimali tusizokuwa nazo basi tutazivuta kwa kutumia Rasilimali tulizonazo. Lakini lazima tuangalie ni Rasilimali ipi bora tuliyonayo itumike kuvuta Rasilimali tusizonazo.
Rasilimali ya kujivunia ndani ya taifa letu ni WATU, Rasilimali watu ndio msingi na nguzo kuu kwa taifa. Ili taifa lolote liinuke lazima liwekeze zaidi katika Rasilimai watu, liijenge nguzo hii kuliko nguzo yoyote ile.
NAMNA YA KUWEKEZA KATIKA RASILIMALI WATU NDANI YA TAIFA.
Nitatoa mbinu kadhaa za kuwekeza katika Rasilimali watu kwa manufaa ya taifa. Nafikiri hapa niweke Nadharia yangu niliyoipa Jina KIKIMI au kwa kingereza nimekipa jina HEpBOFE.
Katika nadharia hii kuna mbinu kuu tatu tuu kama nitakavyoeleza baadae.
KIKIMI ni nini?
KIKIMI ni nadharia ya Taikon(Yangu) niliyoibuni mwaka 2016 nilipokuwa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo nilieleza mbinu bora ya kutumia rasilimali watu kwa ngazi ya taifa ni kutumia ipasavyo kichwa, kiwiliwili na Miguu(KIKIMI) vya watu waliondani ya taifa.
Nilieleza kuwa, Taifa lazima liwekeze zaidi katika vichwa vya watu kabla ya kuwekeza katika jambo lolote lile. Kisha ndipo liwekeze kwenye Kiwili wili na miguu. Nilieleza kuwa, serikali kuwekeza katika vichwa vya watu itajipunguzia mzigo katika utekelezaji wa sera zake za uletaji wa maendeleo.
KIKIMI ni ufupisho wa maneno "KI" ikimaanisha KICHWA, "KI" ya pili ikimaanisha KIWILI WILI(Kimwili mwili. herufi 'm' ikiwa imedondoshwa), "MI" ikimaanisha MIGUU. Mambo hayo matatu ni muhimu katika kuwekeza na kutumia Rasilimali watu ndani ya taifa.
Kwa lugha ya kingereza, kama nilivyosema niliipa jina HEpBOFE.
"HE" represent HEAD
"pBO" represent Physical Body
" FEET" represent FEET
Nilieleza kuwa, kichwa ndicho kinabeba mwili licha ya kuwa kwa macho ya kawaida watu huona miguu ndio hubeba mwili. Kichwa kikiwa kizito kuliko mwili ni ngumu kwa mwili kusimama.
Turudi kwenye mada.
Mbinu kuu tatu za kuwekeza katika Rasilimali watu kwa kutumia Nadharia ya KIKIMI
1. LISHA KICHWA ELIMU SAHIHI (Give the Head the Right Education)
Hapa kuna elimu za aina tatu kuu
1..1 Elimu ya kiutambuzi binafsi (The inner knowledge)
1.2 Elimu ya Utambuzi wa mazingira yanayomzunguka mwanadamu (The Environmental Knowledge)
1.3 Elimu ya utambuzi wa mazingira yaliyonje ya mwanadamu (The Spiritual Knowledge)
Elimu hizi ni muhimu nazalazima kwa kila mmoja wetu ndani ya taifa hili. Kujitambua ni kutambua wengine, kutotambua wengine ni kutokujitambua.
Elimu lazima ijikite katika kumfanya mtu ajitambue zaidi kuliko kutambua wengine, hii itamfanya awatambue wengine. Elimu inapaswa ijikite katika kumfanya mtu ajiheshimu, ajipende yeye binafsi kwani kufanya hivyo kutafanya awapende wengine na kuwaheshimu.
Elimu ikijikita katika kuwaheshimu wengine zaidi itatengeneza jamii ya watu wabinafsi kwani kila mmoja atataka kuheshimiwa, na wale wenye kuheshimiwa kama jamii ilivyo watataka wazidi kuheshimiwa zaidi na zaidi.
Kutaka kuheshimiwa ni dalili ya kutokujiheshimu, kutaka kupendwa zaidi ni ishara ya kutojipenda; kutaka kutambuliwa ni dalili ya kutojitambua. Jamii inapaswa kujengewa elimu sahihi ili kuleta manufaa miongoni mwa watu.
Serikali sharti iliwape watu wake elimu sahihi kabisa, na sio elimu potofu kama ya sasa ambapo kila mmoja husoma na kutafuta elimu ili kutaka kuheshimika na watu wengine, watu huhangaika kutafuta mali ili waheshimike badala ya kujiheshimu katika kutafuta mali na ndipo hapo dhulumma, ufisadi, wizi, na dharau hujitokeza.
Si ajabu msomi wa shahada akamdharau mshona nguo ambazo yeye mwenyewe kazivaa, au siajabu kuona watu wenye vyeo wakidharau na kutishia watu wa chini kwa kuwaambia; unajua mimi ni nani? Jambo ambalo linadhihirisha kutokujitambua na elimu potofu aliyonayo mtu huyo.
Elimu sahihi ni ile inayohangainga kutafuta suluhu ya matatizo yaliyopo ndani ya jamii kwa kutatatua. Na sio mwenye elimu kuwa sehemu ya matatizo yanayosubiriwa kutatuliwa. Mathalani, msomi mwenye elimu aliyepo kwenye jamii yenye changamoto ya ukosefu wa ajira; hapaswi kuongeza tatizo la ukosefu wa ajira kwa kusubiri kuajiriwa badala yake anapaswa atumie elimu yake kuajiri wengine na hivyo kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la ajira ndani ya jamii yake.
Mtu akishapewa elimu ya utambuzi wake binafsi, kisha apewe elimu ya mazingira na mwisho kabisa apewe elimu ya nje ya mazingira yake yaani elimu ya kidini lazima mtu huyo atakuwa mtu bora kabisa.
Hii ni kusema, mtiririko wa elimu unapaswa uwe hivi;
Binafsi >> Mazingira>>> Kiroho(mazingira ya nje.
Kuvunja mtiririko huo ni kutafuta matatizo ndani ya jamii. Mfundishe mtoto yeye ni nani, wanaomzunguka, mazingira yake, kisha ndio umfundishe asiyoyaona.
Kumfundisha mtoto kwanza mambo asiyoyaona(kiroho) ni kumjengea maisha ya kudhania dhania tuu, kila kitu atakichukulia kama dhahania dhahania. Utamjengea mtoto tabia ya kuogopa vitu asivyoviona, utazima uthubutu wake, ubunifu wake, hivyo akikua atakuwa mtu wa kutojaribu mambo.
Huwezi mfundisha kwanza mtoto mambo asiyoyaona wakati anayoyaona na yaliyopo katika mazingira yake hujamfundisha huku ni kumharibu mtoto.
Mtoto ahusike kwenye mafunzo kwa asilimia 80%, kwani yeye ndiye mhusika mkuu.
Serikali, iwekeze katika ubongo wa watu wake, kuibua vipaji, kuviinua na kuviendeleza.
Serikali iwape watu elimu ya kujithamini wao wenyewe kabla hawajathamini watu wengine, kwani kwa kufanya hivyo watu watathamini nchi yao, rasilimali zao na kujipenda wao wenyewe.
Serikali ifundishe watu wake kujipendelea, kubagua wageni, kwani huo ndio uzalendo kwa taifa.
Taifa lolote lisilofundisha watu wake wajipendelee na kuwafundisha wapendelee wageni kuliko wenyeji lazima liwe masikini, taifa lolote ili liendelee lazima llijifunze kubagua wengine (Isolation Policy).
Kwenye kichwa kuna macho, pua, mdomo, masikio, ulimi, meno miongoni mwa mengine.
Serikali lazima ihakikishe kuwa watu wake wanamacho ya kuona miaka mia ijayo, macho yakuona fursa, masikio ya kusikiana kusikiliza mambo yenye manufaa ndani ya nchi, pua yenye kunusa harufu nzuri na kuzifuata na zile harufu mbaya kuziacha. Ulimi wenye kujaribu ladha mbalimbali lakini serikali iwafundishe kuonja ladha tamu, na kuongea lugha njema.
Kupitia kuwekeza kwenye kichwa, taifa litajikita katika mambo haya;
1. Tafakuri, falsafa, Nadharia, Chambuzi, Idia, na mambo yote Yahusuyo Ubungo
2. Muono, matarajio, mipango, na malengo kwa kupitia macho.
3. Lugha nzuri, kwa kupitia kiungo Ulimi. Kumbuka Lugha ni chombo cha mawasiliano.
4. Sauti kutoka nje, Kupitia masikio
5. Kunusa, ubashiri, utabiri kwa kupitia pua.
Serikali itazingatia kichwa hakiathiriwa hivyo itawekeza kwenye mambo haya;
1. Taasisi za elimu
2. Vyombo vya habari
3. Taasisi za kidini
Kwamba yanayoonekana, yanayosikika, yanayosemwa katika vyombo vya habari, taasisi za elimu, na za kidini yanaendana na elimu sahihi kulingana na mipango ya taifa kwa wakati uliopo na unaokuja.
Sio mipango ya nchi ni maendeleo na ufanyaji kazi, lakini vyombo vya habari vinaonyesha filamu za kivivu na maisha ya bahati nasibu, huo ni upumbavu.
2. KIWILI WILI KIFANYE KAZI.
Kiwili wili kuna Mikono, tumbo, mgongo, na ndani kuna moyo, figo, mapafu n..k.
Lakini ili kiwili wili kifanye kazi lazima kiunganike na kichwa kwa kupitia shingo. Hivyo lazima kuwe na mahusiano ya karibu baina ya kichwa na kiwili wili kwa shingo.
Mtu akishapewa elimu kinachofuata ni utekelezaji, tunafahamu kuwa kichwa ni muhimu sana lakini hakiwezi kujitegemea peke yake pasipokuwa na kiwili wili.
Elimu kijana akishapewa lazima iweze kutekelezwa na mikono yake. Lazima kuwe na ukaribu baina ya kile mtu alichofundishwa na kazi za mikono yake.
Mtu asifundishwe nadharia pekee yake bali afundishwe na vitendo. Na hapa kiwili wili ndio kinaingia pamoja na Miguu.
Serikali iwekeze katika kazi za mikono ya watu wake na kuiamini.
3. Kutumia Miguu.
Miguu kazi yake ni kujongea, kutembea au kukimbia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Serikali inayowajibu wa kuwaunda vijana wenye uwezo wa kujongea kutoka hatua moja kwenda nyingine, wasiwe kama mti ambao kujongea kwake ni pale pale lakini mizizi ndio inajongea
Elimu lazima iitoe jamii kutoka hatua moja na kuipeleka katikka hatua nzuri zaidi. Elimu isiyo na miguu hiyo sio elimu, ni elimu hatari kabisa katika jamii.
Sasa Tumesoma, hatuna haja ya kuchukiana, ni wakati sasa wa kutatua changamoto ndani ya jamii zetu. Ukweli ni kuwa umuhimu wa elimu upo katika utatuaji wa changmoto za jamii. Bila changamoto za maisha ndani ya jamii basi hakuna umuhimu wa elimu.
Kwa vile nchi yetu bado jamii zetu zinakabiliwa na changamoto nyingi hii inatoa fursa kwa sisi vijana kutumia elimu zetu kukabiliana na changamoto hizo. Na sio sisi tuongeze changamoto ndani ya jamii ambazo kimsingi hakuna awezaye kuzitatua.
Kwa mfano zipo changamoto nyingi katika Kilimo, ni wajibu wetu sisi wasomi kuzitatua changamoto hizo kwa kuhakikisha kilimo chetu kinakua. Mazao yanapatikana vya kutosha kazi hii itafanywa na maafisa Kilimo na wataalamu wa kilimo, utafutaji wa masoko hii ifannywe na waliosomea masuala ya masoko, miundombinu kama barabara ifanywe na serikali yenyewe.
Serikali inachopaswa kuwasaidia vijana ni katika kuwasapoti katika harakati zao za kutatua changamoto, kama serikali haina pesa za mikopo ya kuweza kuwakopesha vijana basi yaweza toa muda kwa vijana kuanzisha miradi pasipo kulipa kodi hata kwa miaka mitatu au mitano. Serikali itoe vibali na hati za kusafiria kwa bei nafuu na masharti nafuu, vijana wahangaike huku na huko duniani kote.
Serikali iangalie baadhi ya biashara zilizoharamu wazifanyie maboresho ili kila kitu kitumike pasipo kuathiri jamii. Mathalani, biashara ya Bangi, gongo, na Mirungi ziruhusiwe kwa matumizi yasiyo anasa kama vile kunywa au kuvuta.
Kingine, kama sisi kama taifa hatutumii hii haimaanishi sehemu zingine duniani hawaruhusu.
Mathalani, Biashara ya Mirungi, ni moja ya biashara ambayo hapa nchini ni haramu lakini baadhi ya nchi sio haramu, kama vile somalia, Kenya, na Congo. Hii ingekuwa fursa kwa serikali kuruhusu watu walime Mirungi kwa kibali maalumu, serikali ingepata pesa na watu wangepata ajira, kisha hiyo Mirungi ikauzwe katika nchi zinazotumia.
Kule Makanya kwetu, wilaya ya same, nilipozaliwa watu wamenufaika na Mirungi, wamejenga, wamesomesha watoto kwa hiyo hiyo mirungi licha ya sheria kuwabana. Nafahamu serikali ililenga kulinga maadili na afya ya watu ambalo ni jambo zuri lakini naishauri iunnde utaratibu wa kutoa vibali maalumu kwa watu walime kisha wakauze katika nchi zinazohitaji. Ila sheria za kula mirungi iwe vile vile.
Kuna fursa nyingi sana, kwa mfano kuna kile kikundi sijui cha panya Road gani huko, ile ilikuwa fursa nzuri mno kwa nchi, kuwa na vikundi ndani ya nchi vya namna ile ni moja ya hatua za maendeleo. Wale vijana walipaswa wachukuliwe wakapewe mafunzo ya kijeshi wapelekwe kwenye nchi zenye mali kama madini n.k. Kila kitu kitumiwe kwa manufaa ya taifa, watu wa nchi yako wakililia wembe unawapa, ila wakajikatie nchi zingine.
Ndivyo mataifa makubwa yafanyavyo, kwa sasa tunazidi kuwa wengi, hatuwezi zuia baadhi ya tabia zitazozuka na wingi wetu kama taifa, njia bora ni kufungua madirisha na kuvamia nchi zingine.
Tusipowatumia vijana wetu wenye kupenda vurugu kuwapeleka nchi za wenzetu, basi nchi za wenzetu watatuletea vijana wao nna kuwatumia vijana wetu kutuvuruga.
Hatuwezi kufikiri tena kama taifa changa lenye watu milioni kumi, kwa sasa sisi ni taifa kubwa lenye watu takribani milioni sitini ambapo tunashika nafasi ya tano Barani Afrika na nafasi ya ishirini na nne duniani.
Idadi kubwa ya watu ni fursa kwetu au kwa mataifa ya wenzetu. Tusipoitumia sisi wataitumia wao. Tusipojitumia kuvuruga wengine, watatutumia kujivuruga.
Nitoe mifano michache,
Mataifa yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kama vile, Nigeria, Ethiopia, Misri, na Congo ambayo yanatuzidi yote yamevurugwa kwa vile yameshindwa kuvuruga wengine.
Nigeria wapo Boko Haramu
Ethiopia tunajua kinachoendelea jimbo la Tigray
Misri tunajua kulikuwa na civil war miaka iliyopita
Congo wanahangaika na waasi.
Sasa lazima tuwe wajanja kama taifa. Idadi kubwa ya watu nayo ni rasilimali kubwa na muhimu kama zilivyo rasilimali za madini na Gasi.
Hamuwezi mkawa wengi alafu mataifa makubwa yakawaangalieni tuu kama midoli, watu ni rasilimali lazima itumiwe kujinufaisha aidha sisi au wao, kuwavuruga au kuvurugwa.
Ni wakati muhimu sana kwa wasomi katika nchi yetu kutumia nafasi zilizopo.
Muhimu serikali lazima iongozwe na watu wajanja wanaojua kutumia kila kitu bila kuathiri taifa letu. Taifa lisiwe na mipaka katika matumizi ya rasilimali ikiwa tuu haina madhara kwa nchi yetu.
Mataifa makubwa kama Marekani, Uchina, Ujerumani, Urusi n,k. Huwa hayanaga mipaka katika matumizi ya rasilimali zao au za wenzao ilimradi zinufaishe mataifa yao.
Huoni Marekani haitaki nchi zingine zizalishe Nyuklia wakati wao wanazalisha.
Huoni wazungu wanakuambieni muwe na uzazi wa mpango wakati wao wapo wengi kama sisimizi.
Yaani Marekani akuambie usizae sana wakati nchi yako inaeneo kubwa na hata hamjafika milioni mia mbili nawe unakubali. Wakati wenzako wapo zaidi ya milioni mia tatu huoni janja yao.
Taifa lisiwe na mipaka katika matumizi ya rasilimali, killa fursa itumiwe kwa uangalifu.
Leo niishie hapa nimeshachoka kuandika, nawe najua utakuwa hoi. Nikupongeze tuu kama umesoma mpaka hapa.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam
Pichani Ni Taikon wa Fasihi akiwa na wahitimu wenzake mnamo 2017 kwenye mahafali yaliyofanyika chuo kikuu cha Dar es salaam