Ole
JF-Expert Member
- Dec 16, 2006
- 2,157
- 975
Anazitoa mfukoni mwake au ni kodi za watanzania na zinatolewa kwa mujibu wa sheria? kama anahuruma sana mbona TLP na UDP hawapi? sijui hizi tope mlizoweka vichwani wenzetu mlizitoa wapi?Hivi ni Mungu aliwaumba hivyo kweli?
Mkuu fahamu kitu kimoja kupata ruzuku chama chochote ni kwa mujibu wa sheria. Kama umefuatilia hiyo video utaona kabisa Chadema kama Chama cha upinzani kimeshindwa kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa kanuni na sheria tulizojiwekea. Mfano: Mweka fedha wa Chadema kapata hiyo position kwa sababu ya nepotism. Magari yote ya Chadema yanafanyiwa matengenezo kwenye kampuni ya Mwenyekiti, anayehoji matumizi ya hicho chama anang'olewa. Mifano ipo mingi na wale wote wanaotilia mashaka ya mwenyekiti wa miaka 20 iliyopita wakiuliza kuna mawili aidha wanahama chama au maisha yao yapo hatarini. Je, Msajili halioni hili kwamba hiki chama kina walakini? Wengine tayari tunaona hiki ni chama cha ukoo wa Mbowe. Je, wewe unakubali kweli kodi yako inatumika sahihi kumtajirisha Mbowe na familia yake?
Ruzuku wanayopata ingeweza kujenga ofisi yenye hadhi ya Chama cha upinzani sio kibanda hasara. Je, umeshaona Chadema wakifanya hata mkutano moja kwenye ofisi zao? Sifahamu hata kama kuna vyoo vya kutosha pale ufipa.
Jiulize ni kwa nini Dr. Slaa alikimbia chama hiki? Je, ni kwa nini Mropokaji mkuu na mpotoshaji alikimbia Chadema na kuanzisha chama cha mfukoni? Je, ni kwa nini wanachama wengi wanaondoka kutoka hiki chama? Ukichunguza utaona hakuna uwiano wa Demokrasia wanayoipigia kelele asubuhi, mchana jioni na usiku linapokuja swala la ruzuku ambayo inatumiwa kumtajirisha Mbowe na familia yake pekee. Bila kusahau jinsi waziri mkuu mstaafu alivyokimbizwa kama ukoma.