SoC02 Muda umewadia wa kuanzisha Serikali za Majimbo

Stories of Change - 2022 Competition

IFAC

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
3,604
9,040
Tanganyika ilipata uhuru zaidi ya miaka sitini(60) iliyopita, ikirithi mfumo wa kiutawala wa Serikari toka kwa waingereza.

Tukarithi pia mfumo wa Kijeshi toka kwa wakoloni.

Mifumo yote miwili Haina tija Wala manufaa kwa jamii zilizopo nchini Tanzania.

Mfumo wa kiutawala wa Serikari tuliorithi una mapengo mengi lakini pia auhusishi jamii za maeneo husika moja kwa moja.

Ni mfumo unaoitenga jamii na serikari iliyopo madarakani, yaani jamii haishirikishwi moja kwa moja ila kunakuwa na dude liitwalo serikari ambalo jamii hujitenga nalo hivyo kuchelewesha maendeleo.

Maendeleo hupangwa na serikari bila kujali uhitaji wa jamii husika Wala vipaumbele vyao.

Mfumo wa sasa hauna tofauti yoyote na ule wa kikoloni, kwani viongozi kibao wanateuliwa bila matakwa ya Wananchi bali watawala wanavyojisikia.

Mfano: Mchakato mzima jinsi Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyopatikana, inajulikana wazi wafuasi wa chama kile watakavyo amua ndio huamua nani raisi wa nchi na sio wananchi watakavyo hitaji.

Uteuzi wa wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya, Makatibu tawala, Wakurugenzi wa Halmashauri hawa ni watendaji kwenye tawala za mikoa na serikari za mitaa ila hawatokani na matakwa ya Wananchi.
Hii Ina tofauti gani na enzi za mkoloni.

Wawakilishi wa Wananchi, kwenye wilaya kuna mbunge, madiwani, meya, mkurugenzi, mkuu wa wilaya, Katibu Tawala kiasi Cha hawa kuingiliana majukumu Yao na yupi ni mkubwa.

Mara nyingi ugonvi hutokea kati ya Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa wilaya juu ya nani ni mkubwa, kumbuka wote huteuliwa na mtu mmoja.

Kwa nini serikari ya majimbo Sasa?

Utagundua mfumo huu wa kiutawala tumekuwa nao toka mwaka 1960 ila haujamsaidia Mtanzania kuuondoa umasikini, kufanya serikari isiwajibike, Watawala kujiona miungu watu na kufanya maamuzi kwa manufaa yao badala ya watu walio tumwa kuwatumikia.

Hivyo uanzishwaji wa Serikari za majimbo itasukuma gurudumu la maendeleo kwa Kasi kubwa, itakuwa ni jukumu la watu wa eneo husika kujiletea maendeleo badala ya kusubiri serikari kuu.

Serikari kuu itabaki na vitu vichache, Tena muhimu vya kushughulikia, pamoja na kusawazisha Pato la Taifa.

Vitu kama Ulinzi, Usalama, Diplomasia, Mapato, Kodi, Nishati, Miundombinu ya Barabara, Huduma za afya kitaifa.

Ila sera zote zinazohusu Serikari za mitaa na tawala za mikoa zinarudishwa mikononi mwa majimbo.

Kumbuka mfumo wa sasa umedunisha miji na maeneo ambayo yana Mapato makubwa lakini pesa zake zimekwenda kufanyiwa mambo mengine nje ya jimbo husika.

Maeneo yenye Mapato makubwa Tanzania ni kama mji wa kahama, mji wa Geita, Jiji la Mbeya, Mkoa wa Tanga na maeneo mengineo.

Majimbo yataharakisha kuvitambua vipaumbele vyao vya maendeleo na kuvifamyia kazi kwa haraka badala ya kwenda kumuomba mtu mmoja yupo Magogoni ambaye ndiye atakaye amua.

Majimbo yataharakisha yanaendeleza watu wake kwenye nyanja zote.

Mfano wa Majimbo ni:

Jimbo la Mashariki lenye mikoa kama Morogoro, Pwanill, Dar es Salaam na Tanga.

Jimbo la kusini lenye mikoa kama Lindi, Mtwara, Ruvuma baadhi ya eneo la Mahenge mkoani Morogoro.

Jimbo la Kaskazini lenye mikoa kama Korogwe, Kilimanjaro, Arusha, Mara baadhi ya maeneo mkoa wa Manyara.

Jimbo la Kati lenye mikoa kama Dodoma, Singida, Baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tabora na Manyara.

Jimbo la Magharibi lenye mikoa kama Tabora, Kigoma na Katavi.

Jimbo la Nyanda za juu kusini lenye mikoa kama Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Sumbawanga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom