Muda ni mwalimu na mwamuzi mzuri

Muda ni mwalimu na mwamuzi mzuri

Superhuman 1995

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2020
Posts
1,513
Reaction score
2,470
Muda uliamua historia kubwa na nzito duniani, muda uliamua kukatisha maisha ya majenelari walioogopwa katika historia ya dunia,muda uliwakatisha uhai wakaishia ahera,muda huinua dhaifu na kuwa mwenye nguvu,muda huamua na kubadilisha historia ya dunia kwa sekunde,muda ni mwalimu mzuri kwa sisi tulio hai,unatufanya tujifunze kwa walio pita,kung'amua mazuri na mabaya,mabaya tuyaache maana yatatuadhibu kwa ghadhabu kubwa hata kizazi na kizazi

Muda ukifika haijalishi ulifanya uchawa kiasi gani utatwaliwa na futi sita utafukiwa lakini ghadhabu haitakuacha salama karma iko pale pale historia mbaya na ya kutisha itaandikwa katika kizazi chako,samaki mmoja akioza wote wanaoza.

kitatafunwa kwa kosa lako wewe,ndipo msemo mmoja huja ukiua kwa upanga na wewe utauawa kwa upanga,historia toka dunia iumbwe ,haijawahi kwenda kinyume,matukio yatapita lakini historia na nature itabaki kwenda na kanuni ya kiasili,maiti haiwezi kumzika maiti mwenzake,bali aliye hai umzika aliyekufa,Tutende mema ,tufanye haki,uadilifu ndio msingi mkubwa wa kutengeneza taswira yetu ya haki milele,na kuwa mwanamapinduzi wa haki kizazi hadi kizazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom