Muda mwingine naona aibu kumsema vibaya Kikwete!

shalet

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,430
3,531
wasalaam,
Jamani pamoja ba mapungufu ya Kikwete kama binadamu kuna mambo mazuri mengi kayafanya kwanini hatuyaongelei hayo tunataka awe alikamilisha kila kama vile sisi miaka 10 iliyopita tumefanya mazuri tu au kukamilisha mambo yote kweli tunasahau ujenzi wa miundo mbinu, barabara ya kwenda kusini jengo jipya la moyo muhimbili, ujenzi wa chuo cha dodoma ajira nyingi zimepatikana kipindi cha kikwete, uunganishwaji wa umeme kwa kasi hasa vijijini, kukua na kushamiri kwa biashara nyingi. ujenz wa shule za kata. na maboreshp mengi aliyofanya kwenye sekta mbalimbali,
Japo ana mapungufu yake ila kuna zawadi nzuri katuachia Kikwete tusimbeze kama vile hJafanya kitu.
 
kikwete ali create ajira nyingi sana hata police, uhamiaji, magereza, zimamoto walikua wanachukua vijana wengi ili watu wasiwe "unemployment" wakati magufuli ndo kwanza anafukuza wengine ili unemployment problem liongezeke.
 
Mapungufu ni mengi kuliko mazuri, na hayo mapungufu yaliathiri uchumi, na kuathirika kwa uchumi kulimgusa kila mtu hata wa kijijini. Labda ww ulifaidika na utawala wake
 
Media ya Tanzania inachangia katika kujenga negative mindsets ya watanzania wengi. Mwandishi wa habari anamuuliza mkurugenzi wa shirika la umma, mzee unataka tukuandikeje?. Halafu matajiri wanaomiliki vyombo vya habari hawataki kuwepo na regulator wa habari!, wanataka uhuru usiokuwa na mipaka, kitu ambacho duniani hakipo. Sio ajabu kuona kuwa kila mwanzo wa awamu fulani yule rais aliyemaliza muda wake anachafuliwa na baadhi tu ya magazeti. Vyombo vya habari Tanzania ni mateka wa siasa za makundi, vikiweza kuwa na uhuru wenye kuheshimu maadili, jamii itaanza kuwa na watu wengi wenye positive mindsets.
 
kikwete ali create ajira nyingi sana hata police, uhamiaji, magereza, zimamoto walikua wanachukua vijana wengi ili watu wasiwe "unemployment" wakati magufuli ndo kwanza anafukuza wengine ili unemployment problem liongezeke.

Unamlinganisha Magu na Mkwere????? Mtu kashindwa kazi, amekiuka "ethics" za kazi yake aachwe tu?????
 
Ukweli ni kwamba chuki imejengeka kwa hawa jamaa,,, ukweli lazima usemwe kosa la JK kwao ni kuharibu system ya wizi au mtandao wao wa kimafia na wizi walioujenga kwa miaka mingi na kuja kuharibiwa ndani ya mwaka mmoja, mkwere kwao ni adui namba moja maana ndio mtu pekee aliyejua formula yao huku akiwa si kibaraka wao, kwa kulijua hilo walitamani wamfanye chochote mkwere maana ndio mwiba pekee uliobaki, BWM hawakumuogopa maana walimjua always ni muoga kwao.. chuki lazima ibaki kwa mkwere tu
 
Kila mtu anamapungufu yake lakin ya JK yalizidi nakupelekea nchi kuingia mikataba hewa,wizi wa escrow,upigaji Bandarini,ubinafsishwaji nyumba za serikali nk...yapo aliyojitahidi lkn si kwa kiwango alichotuaminisha wakati wa kampeni zake.
 
Mapungufu ni mengi kuliko mazuri, na hayo mapungufu yaliathiri uchumi, na kuathirika kwa uchumi kulimgusa kila mtu hata wa kijijini. Labda ww ulifaidika na utawala wake
Naungana na wewe asilimia mia. Wakati wa JK nchi ilikuwa imesimama kana kwamba haina kiongozi. Kibaya zaidi ni pale zilipoibuka kashfa kubwa kubwa na akashindwa kuwachukulia hatua wahusika. kingine kikubwa kuliko vyote, kuna kashfa alizibeba mabegani mwake yeye mwenyewe kwa vile alikuwa nazo toka huko alikotoka akiwa waziri wa nishati na madini. Kashfa kama ya escrow hii alikuwa anaifahamu fika kwa vile ni yeye mwenyewe aliyeisaini mikataba hiyo akiwa waziri wa nishati na pia fedha miaka ya 1994/1995. Richmond aliitengeneza kutokana na uzoefu wake ndani ya Tanesco akiwa waziri wa nishati. Kuna kashfa ya Katibu mkuu wa Nshati na madini David Jairo aliyechangisha fedha ili kuwahonga wabunge wapitishe bajeti ya wizara yake. Hizi na nyinginezo nyingi alizipotezea ili isifahamike ushiriki wake, au kuwaokoa washkaji zake. Ukiziangalia kashfa hizi tatu tu mbali na nyingi nyingine zimhusuzo, haihitaji kuwa na digrii au kupitia mafunzo ya upelelezi kufahamu kuwa yeye akiwa kama Rais wa nchi alishiriki kutekeleza michezo hii michafu. Acha historia imtafune.
 
Ni bavicha ndo wanamponda! Wenyewe wameapa hata rais awe nani na afanye mazuri, wao ni kuponda tu mpaka lowasa awe rais!
Wapotezee tu!
 
kikwete ali create ajira nyingi sana hata police, uhamiaji, magereza, zimamoto walikua wanachukua vijana wengi ili watu wasiwe "unemployment" wakati magufuli ndo kwanza anafukuza wengine ili unemployment problem liongezeke.
kweli ajira nyingi za vyombo vya usalama tumezisikia kipindi ch kikwete.
 
Kinachotuboa ni kwamba hata hizo barabara ni mikopo mitupu, aliacha watu wajipigie pesa watakavyo, kiongozi wa chini yake akiharibu zaidi ya alivyoelekezwa nae anakwenda kumwambia mkuu wabunge wamegundua na wamemind ,yy anampoza na kusema huu ni upepo tu, hakuna kukusanya kodi, kusema mataifa ya nje yanahela nyingi sana ni sisi tu kwenda kuomba. Haya ndio yanatuboa.
 
Baada ya mwaka ndo tutajua kati ya jpm na jk yupi bora. Ni mapema sana kulinganisha, najua wote walianza vizuri but tunchoangalia mwendelezo na umaliziaji. Ni mapema kumsema jk na ni mapema kumsifia jpm. Jpm hajakutana na changamoto kama epa, richmond, katiba mpya,escrow. Busara,hekima,uongozi bora hupimwa na changamoto ngumu.
 
Mazuri yapo hatukatai lakini ukichunguza hayo mazuri yametucost sana watanzania wani kwenye miradi mingi imefanywa chini ya viwango na mengine yametumia hela nyingi kuliko thamani zake. JK asilaumiwe sana kwani system iliyokuwepo inaficha haya waovu na maovu. Wanananchi hawaambiwi ukweli serekali inapoumizwa kwa kuogopa kukosolewa.
Nategemea rais huyu hataweka system ya uwazi ili tuweze kujua ukweli.
 
wasalaam,
Jamani pamoja ba mapungufu ya Kikwete kama binadamu kuna mambo mazuri mengi kayafanya kwanini hatuyaongelei hayo tunataka awe alikamilisha kila kama vile sisi miaka 10 iliyopita tumefanya mazuri tu au kukamilisha mambo yote kweli tunasahau ujenzi wa miundo mbinu, barabara ya kwenda kusini jengo jipya la moyo muhimbili, ujenzi wa chuo cha dodoma ajira nyingi zimepatikana kipindi cha kikwete, uunganishwaji wa umeme kwa kasi hasa vijijini, kukua na kushamiri kwa biashara nyingi. ujenz wa shule za kata. na maboreshp mengi aliyofanya kwenye sekta mbalimbali,
Japo ana mapungufu yake ila kuna zawadi nzuri katuachia Kikwete tusimbeze kama vile hJafanya kitu.
Wewe utakuwa jibu la kwapani
 
Back
Top Bottom