Muda gani sahihi wa kubadili oil kwenye pikipiki

Habari wadau, nimenunua pikipiki mpya Boxer BM 150, kwa ajili ya matumiz binafsi napenda kufahamu ni mda gani sahihi au ni baada ya KM ngapi natakiwa kubadili Engine oil.

Shukrani sana.
Mkuu hongera sana kwa kununua Boxer..kwenye user manual ya Boxer BM 150 wanakuambia utumie oil ambayo ni SAE 20w50 API SL or JASO MA grade na umwage oil kila baada ya kilometer 5000,bila kusahau kubadili oil filter kila baada ya kilometer 20,000(kama ni oil filter original) basi hapo utadumu nayo.Binafisi huwa siangalii kilometer nimejiwekea tu utaratibu wa kumwaga oil na kubadili oil filter kila mwisho wa mwezi maana oil filter tunazouziwa huku sio original..kwa kufanya hivyo hadi leo piki piki bado mpya na haijafunguliwa injini japo inakimbilia mwaka wa 3.
 
Attachments

  • user manual.PNG
    user manual.PNG
    40.6 KB · Views: 414
Mkuu hongera sana kwa kununua Boxer..kwenye user manual ya Boxer BM 150 wanakuambia utumie oil ambayo ni SAE 20w50 API SL or JASO MA grade na umwage oil kila baada ya kilometer 5000,bila kusahau kubadili oil filter kila baada ya kilometer 20,000(kama ni oil filter original) basi hapo utadumu nayo.Binafisi huwa siangalii kilometer nimejiwekea tu utaratibu wa kumwaga oil na kubadili oil filter kila mwisho wa mwezi maana oil filter tunazouziwa huku sio original..kwa kufanya hivyo hadi leo piki piki bado mpya na haijafunguliwa injini japo inakimbilia mwaka wa 3.
Shukrani sana mkuu, utararatibu wa kila mwezi nimeupenda.
 
Mkuu hongera sana kwa kununua Boxer..kwenye user manual ya Boxer BM 150 wanakuambia utumie oil ambayo ni SAE 20w50 API SL or JASO MA grade na umwage oil kila baada ya kilometer 5000,bila kusahau kubadili oil filter kila baada ya kilometer 20,000(kama ni oil filter original) basi hapo utadumu nayo.Binafisi huwa siangalii kilometer nimejiwekea tu utaratibu wa kumwaga oil na kubadili oil filter kila mwisho wa mwezi maana oil filter tunazouziwa huku sio original..kwa kufanya hivyo hadi leo piki piki bado mpya na haijafunguliwa injini japo inakimbilia mwaka wa 3.
Mkuu mimi ninahitaji boxer BM 150 iliyotumika kidogo, yaani yakununua kwa mtu vipi ni vitugani nizingatie ili ninunue iliyo bora pia nisiuziwe copy (mchina)
 
Mkuu..boxer used hata mimi nimeshanunua sana cha kuzingatia ni hakikisha namba ni B(sasa hv zimefika C), injini haijawah kufunguliwa,kagua mngurumo wake kama ni wa boxer wa asili(inabidi uwe na uzoefu na mlio wa boxer,huwa hautofautiani sana na ule wa bajaj ya miguu mitatu ambayo ni nzima),hakikisha haijachomelewa sehemu yoyote,kagua kama haitoi moshi(boxer huwa zinaua sana block),kagua kama haigongi mkono wa injini(crankshaft) maana ni ugonjwa mkuwa wa boxer,chukua zile zenye top cover ya injini nyeusi ya plastic ndo nzuri kuliko zile ambazo top cover ya injini sio plastic(hizi mpya)..mwisho kabisa test kuiendesha kwenye bara bara ambayo ni mbovu hasa yenye mashimo au mawe huku ukiisikilizia kama haipigi kelele za hovyo...all the best Mkuu.
 
Somo zuri kabisa!...
 
Kama walivyosema wadau kwakweli oil tulizonazo nyingi zinapoteza viscosity haraka sana hivyo ni vema kwa misele ya town tu humu badili oil kila ifikapo 1000km. Ila endapo utasafiri safari kwa siku moja ya kama 400km ukifika badili oil itakuwa imepoteza kabisa viscocity level.
 
Mkuu..boxer used hata mimi nimeshanunua sana cha kuzingatia ni hakikisha namba ni B(sasa hv zimefika C), injini haijawah kufunguliwa,kagua mngurumo wake kama ni wa boxer wa asili(inabidi uwe na uzoefu na mlio wa boxer,huwa hautofautiani sana na ule wa bajaj ya miguu mitatu ambayo ni nzima),hakikisha haijachomelewa sehemu yoyote,kagua kama haitoi moshi(boxer huwa zinaua sana block),kagua kama haigongi mkono wa injini(crankshaft) maana ni ugonjwa mkuwa wa boxer,chukua zile zenye top cover ya injini nyeusi ya plastic ndo nzuri kuliko zile ambazo top cover ya injini sio plastic(hizi mpya)..mwisho kabisa test kuiendesha kwenye bara bara ambayo ni mbovu hasa yenye mashimo au mawe huku ukiisikilizia kama haipigi kelele za hovyo...all the best Mkuu.
Chief, vizuri kwa ufafanuzi mzuri kwa ambaye sio mzoefu wa pikipiki ni viashiria gani ambavyo vitamjulisha mkaguaji kua mkono unagonga kwa maana ya crank shaft.

Much thanks!
 
Mkuu..kama Mkono unagonga huwa unasikia kabisa jinsi unavyogonga na huwa unasikika juu kabisa ya injini,lakini pia wakati wa kuendesha piki piki utaona kabisa vibrations zinakuwa kali hasa kwenye foot rester unapoweka mguu kama dereva.Njia nyingine ni kuwasha piki piki then unaweka mkono wako chini kabisa ya injini kama vile injin ipo kiganjani mwako then bila kutoa huo mkono unavuta mafuta kwa mkono mwingine,utaskia crankshaft inagonga chini ya injini..Tofauti na hapo mpaka fundi afungue cylinder head na block then kwa kutumia mkono mmoja atashika connecting rod kama unavyoshika maiki halafu atagonga gonga juu yake kwa mkono mwingine kama unagonga atajua tu..kwa mimi nikisikiliza tu mngurumo wa injin najua.
 
Elimu nzuri kiongozi.
 
Safi brother..., me kuna boxer nimeiona ni nzuri ila kwenye tank kuna sehemu imebonyea, sasa vipi tank huwa linanyooshwa?
Na vipi haitapelekea tank kutoboka?
 
Tank la boxer original ni ngumu kunyoosha likawa kama mwanzo kutokana na ukweli kuwa ni mazito mno,labda lichanwe kidogo ipatikane sehemu ya kuingiza kitu linyooshwe then lichomelewe kwa gesi..ila Mkuu kama piki piki injini ni nzima chukua then kanunue tank jipya original haizidi 120,000/= maana ukilinyoosha lililopinda utaharibu umbo la boxer but kuwa makini yapo ma tank ya kichina kama sio mtaalamu huwezi jua kama ni fake yenyewe haizidi 80,000/= na ukiweka hili kwenye maungio ya tank na bumper inabaki nafasi so components za ndani kama battery zinaonekana na utapoteza muonekano wa boxer.Ukihitaji maelezo ya kutofautisha tank fake na original ntajaribu kukusaidia.
 
Asante kwa maelezo murua mkuu.

Nina maswali mengine mawili naomba pia niulize;
1. Nina boxer Bm150 nyuma kwenye shock ups haigusi wala haigongi (iko comfortable) lakin nikipita kwenye bums (hasa nikipakia mtu) wakati wakunesa shock ups zinatoa kamlio flan hivi "kwich kwichi" kwa mbaali,, nilienda kwa fundi akaniwekea oil lakin bado inaendelea kutoa hako kamlio,, tatizo inaweza kuwa ni nin boss?

2. Pia kwenye hio boxer battery yake naona imechoka nimeshauriwa nikabadili maji ya battery,, naomba kufahamu ni kwa muda gani betri itakua na nguvu yakutosha ikiwa na maji mapya kabla yakubadili tena.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom