FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,817
INNA LI LLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUN
Aliyewahi kuwa meneja wa Simba miaka ya 70s na 80s (kama sikosei), Abdulrahman Khamis Muchacho, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, maandalizi ya maziko yanafanyika nyumbani kwake, Manzese, Dar. na maziko yatakuwa leo baada ya Swalat'l Jumaa makaburi ya Kisutu.
Muchacho aliwahi kuwa ni meneja wa Simba yenye mafanikio katika miaka hiyo na pia alikuwa ni mfadhili na mpenzi wa Simba wa ukweli.
Licha ya kuwa ni mwanamichezo, Muchacho pia alikuwa mwanamuziki. Muchacho ni mwanzilishi na meneja wa kundi la Taarab lililojulikana kama MAMESH Taarab. Alikuwa pia ni muimbaji katika kundi hilo. Kundi ambalo lilimuibua Sabah Muchacho (hawa ni ndugu kabisa, baba mmoja mama mmoja) ambae ni Muimbaji maarufu wa nyimbo za Taarab Tanzania.
Tunawapa pole wana Simba wote na ndugu jamaa na marafiki katika huu msiba mzito.