Ukiacha statement ambayo Mkjj ameiweka, nimebahatika kupata miniti za vikao vyote vya kamati ya mazungumzo. Ukisoma kwa undani, utabaini kuwa hiki kinachoitwa muafaka ni mchezo mwingine wa siasa. Kuna uwezekano kuwa tabasamu la JK liliwapumbaza CUF wakakubali kuingia kwenye hii kitu kichwakichwa. Na inawezekana pia CUF nao ni sehemu ya mchezo huu wa siasa kwa sababu kwa mujibu wa miniti zile, hakuna sehemu ambayo hawa mabwana walikubaliana kuhusu haya wanayotueleza leo hadharani.
So, I think it is safe to believe that kuna watu wanachotwa akili katika hili. Kama hawakukubaliana kuhusu serikali ya mseto, kwa nini UF waliibuka na hilo na awali CCM haikukemea! Badala yake wao wakaenda Butiama na kuja na kura ya maoni.
Sasa wamebaki kubishana, CCM na kura ya ,aoni, CUF na serikali ya mseto na hakika malumbano haya hayatafikia mwisho siku za karibuni. Lakini acha tuendelee kuangalia hii sinema, inaelekea ndo mustakabali wa maisha yetu huo