Muafaka: Third Party Needed


Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Likes
101
Points
145
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 101 145
Waungwana,

Hivi chama chetu makini cha CHADEMA kwa nini kisiingie kuwasuluhisha CCM na CUF? Mimi nadhani ndio wakati muafaka.


Ahsanteni
 
Mtu wa Pwani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,127
Likes
99
Points
145
Mtu wa Pwani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,127 99 145
Wao Wenyewe Hawajijui Hawajitambui
 
Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2006
Messages
7,712
Likes
259
Points
180
Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2006
7,712 259 180
....^^Halafu waje kwenye muafaka wa ccm?
 
Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,842
Likes
96
Points
145
Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,842 96 145
Chadema kusuluhisha ndugu Kasheshe you are not serious .CCM siasa kwao ni vita na si maendeleo ya Nchi .Wamesha sema hakuna mgogoro ZNZ , hata watu wanapeleka barua UN wanakamatwa usiku na kuhojiwa .Kama Chadema wanaongelea Ufisadi wa uwazi kabisa na nyie CCM mnakataa kwa nguvu zenu zote ndugu Kashehe mjiangalie na Chame chenu kwanza na serikali yenu .Kweli mnaitakia mema Tanzania ?
 
M

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,459
Likes
186
Points
160
M

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,459 186 160
Kasheshe,
Mkuu unajua nilicheka sana majuzi nilipomsikia Seif akimtaka Kikwete asimamie MUAFAKA ati kama alivyofanya KENYA....
Yaani huyu jamaa kashindwa kabisa kuona tofauti ya Kenya na Tanzania.. kama vile aliyesimamia Muafaka wa KENYA ni Mwai Kibaki..
Nafasi ya KIkwete ktk Muafaka huu ni sawa na ile ya Kibaki sasa itakuwaje asimame against wale waliomweka madarakani yaani baraza la Mapinduzi. hawa jamaa wote walkimchagua JK dhidi ya Salim leo abadilike na kuwatupa jambo ambalo haliwezi ku guarantee nafasi yake ndani ya chama..Haya nasikia leo kasema Kikwete kalogwa!.. duh ama kweli Seif ana visa yaani kashindwa kabisa kuona upana wa hoja nzima ya Muafaka!
Mimi nadhani swala la Muafaka limesha pitwa na wakati ni swala ambalo linahitaji mtazamo mpya na iundwe upya Kamati maalum itakayoweka mapendezo ya kiutawala na kamati hiyo ijumuishe vyama vyote, wazee waasisi wa vyama na Uhuru wa sehemu zote mbili..Pia maoni ya wananchi ni muhimu sana kutokana na kwamba hawa viongozi watakaopitishwa ndani ya Muafaka ni lazima waheshimiwe na kukubaliwa sehemu zote mbili kuwa ni viongozi walkiopitishwa kutokana na utaratibu wa katiba ya nchi.
Nje ya hapo, ni changa la macho kwa wananchi wa pande zote mbili na sidhani kama viongozi kama kina Salmin watakubaliana na MUAFAKA huu...
 
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
7,011
Likes
38
Points
145
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
7,011 38 145
Ukiacha statement ambayo Mkjj ameiweka, nimebahatika kupata miniti za vikao vyote vya kamati ya mazungumzo. Ukisoma kwa undani, utabaini kuwa hiki kinachoitwa muafaka ni mchezo mwingine wa siasa. Kuna uwezekano kuwa tabasamu la JK liliwapumbaza CUF wakakubali kuingia kwenye hii kitu kichwakichwa. Na inawezekana pia CUF nao ni sehemu ya mchezo huu wa siasa kwa sababu kwa mujibu wa miniti zile, hakuna sehemu ambayo hawa mabwana walikubaliana kuhusu haya wanayotueleza leo hadharani.
So, I think it is safe to believe that kuna watu wanachotwa akili katika hili. Kama hawakukubaliana kuhusu serikali ya mseto, kwa nini UF waliibuka na hilo na awali CCM haikukemea! Badala yake wao wakaenda Butiama na kuja na kura ya maoni.
Sasa wamebaki kubishana, CCM na kura ya ,aoni, CUF na serikali ya mseto na hakika malumbano haya hayatafikia mwisho siku za karibuni. Lakini acha tuendelee kuangalia hii sinema, inaelekea ndo mustakabali wa maisha yetu huo
 
Kamende

Kamende

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2008
Messages
415
Likes
6
Points
0
Kamende

Kamende

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2008
415 6 0
Sishtushwa na ghiliba za sisiem.

Hiki ni chama kilichospecialize kwenye dhuluma. Muafaka hauwezi kupatikana mbele ya CCM na chama chochote kinachochaguliwa na wananchi bila ya CCM kuondolewa nguvu yake ya fedha. Somo hili la fedha ndani ya CCM ni gumu kwa wengi.

Kwa matendo ya CCM, wananchi walitakiwa wawe wameandamana nchi nzima wakitaka chama hicho kifutwe. Wametenda maovu ya kutosha kufutwa kwao. Lakini milango ya fedha na fursa inawaghilibu wengi waendelee kuishabikia na kuilinda.

Kama nchi hii inataka usalama mbele ya CCM ni budi kuitenga CCM na dola, fedha na mafisadi. hapo demokrasia itakuwa tele.
Kuhusu CHADEMA kuingia kati kuisuluhisha CCM na CUF. Hili nalipinga sana kwa sababu zifuatazo:-
1. CHADEMA yenyewe inailalamikia CCM kuwa imewaibia kura zao nyingi tu za
urais, wabunge kadhaa wa CCM waliiba ushindi wa wagombea wa CHADEMA
madiwani wengi tu wameibiwa ushindi na CCM na pia viongozi wa
CHADEMA wamenunuliwa na wengine wanaelendelea kunyemelewa na
CCM. Kwa maneno haya naamini kuwa panatakiwa pia mazungumzo ya
MUAFAKA BAINA YA CCM NA CHADEMA.
2. CCM si chama cha kusuluhishwa na mtu yeyote duniani. Wao wanajua
kutawala tu na ya kwamba hakuna mtu anayeweza kutawala nchi hii ambaye
hatokani na CCM. Hata salaam zao zinathibitisha hilo.
3. CCM wanaamini kuwa wanawatawala watanzania wajinga sana. Kama
akitokea mtanzania mjanja wanamchonganisha na watanzania wenzake
haraka sana.

kwa maneno hayo naamini suluhu ya chama chochote na CCM ni kuiacha iendelee kuwatesa sana wananchi ili ifike siku nchi haitawaliki tena.

UMkonto we sizwe
 

Forum statistics

Threads 1,239,140
Members 476,434
Posts 29,343,858