Mtwara walipwa Sh130 kupisha bomba la gesi...

naddin

Member
Nov 20, 2012
6
0
Ukizingatia kua ni eneo lilikua nyuma sana kimaendeleo ukifananisha na maeneo mengine nchini wanayo haki yakudai maendeleo kwa rasilimali zinazowazunguka.

SOMA:

WAKULIMA wa Kijiji cha Mangamba Manispaa ya Mtwara-Mikindani ambao bomba la gesi linajengwa na Serikali Kijiji cha Msimbati katika Halmashauri ya Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam na kupita kwenye mashamba ya wakulima hao wameulalamikia mradi huo badala ya kuufurahia.

Kwanini wakulima hao wanalalamikia mradi huo mzuri wa gesi? Hilo ni moja ya maswali ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Wananchi hao wanaulalamikia mradi huo kwa sababu wamedhulumiwa.

Wanasema fidia waliolipwa kwenye mashamba yao ambako bomba la gesi limepita ni kidogo na kwamba hailingani na kipande cha muhongo wa kukaanga ambao unauzwa Sh100.

Fidia ambayo inalalamikiwa na wakulima hao ni ya mazao, hususani zao la muhogo ambapo wamelipwa Sh130 kwa shina moja. Wakulima hao kwa nyakati tofauti wanasema kiwango kidogo kuliko thamani ya zao hilo.

Wakulima hao wamewatupia lawama wathamini waliothamini mazao yao huku wakisema ndio matunda ya kuwa na wasomi wasiojua thamani ya mazao ya kilimo.

Mkazi wa Mangamba, Abdallah Rahisi Nyodo (34) ni miongoni mwa wakulima ambao wamepoteza mashamba yao baada ya bomba la gesi kupita katika eneo hilo.

Anasema hawakutendewa haki kwa kuwa walipaji wameshusha thamani ya zao hilo.

"Hadi leo hatuamini kama kweli Serikali inaweza kufanya dhuluma hii kwa wakulima wake, shina la Muhogo wametulipa kwa Sh130 hivi kuna haki hapo?. Shina hili la muhogo, mkulima ametumia misimu miwili hadi mitatu kulihudumia leo analipwa bei ya kipande cha muhogo wapi haki?

"Malipo haya yamefanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), hebu jiulize leo hii shina la Muhogo ukiuuza kwa wachuuzi utapata Sh5,000 hadi 7,000, hii ni bei ya shamba, ukipeleka mjini tenga la mashina matano ya muhogo mbichi utauza Sh50,000 hadi Sh40,000"

Anabainisha kuwa shamba lake lilikuwa na mihogo 486 ambayo amelipwa fidia ya Sh130 kwa shina na kupata jumla ya Sh63,180 badala ya Sh2.4 milioni iwapo mashina hayo angeyauza kila shina moja kwa bei ya Sh5,000.

Gesi siyo mkombozi'
"Muhogo kwetu ndiyo zao kuu la chakula, ndiyo kimbilio letu, kwenye shina moja unaweza kupata mihogo mikubwa hadi 10 ambayo ukiamua kuiuza kwa rejareja kila muhogo unaweza kutoa vipande kumi vya Sh100 kwa kila kimoja.

"Hapa gesi hatuwezi kuitazama kwa jicho la ukombozi bali ni janga linalopora kidogo tulichonacho, kama wapo wanaosema gesi ni neema basi ni kwa upande wa Serikali, sio sisi wakulima,"anasema.

Mkazi mwingine wa Mangamba, Ali Abdallah Mabangi (38) anasema shamba lake lenye mashina ya mihongo 280 amelipwa fidia ya Sh36,400 baada ya kulipwa Sh130 kwa kila shina.

"Fidia ya zao la muhogo kwa kweli imenigandamiza, ni heri wangeniambia ning'oe mihogo yangu nikatafute kwa kuuza kuliko kulipwa fidia hii, ningeuza zaidi ya Sh5000 kwa shina, mihogo yangu nimeihudumia kwa miaka mitatu leo nalipwa Sh130 kwa shina, sio haki.

SOURCE: MWANANCHI
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,106
2,000
Je madini yamewanufahisha wana geita? Ntwara ni ntwara tu lazima wachinjiwe baharini........
 

mceddy

Senior Member
Apr 16, 2012
106
0
Umoja wao na mshikamano wao ndio uta saidia kilio chao kusikilizwa tho ifke mahali ss kila mahali peny resources kma hzo zianze kuwasaidia wtu wa hyo sehemu ikiwemo ajira ndogo ndgo etc inspite elimu yao ina weza kuwa ndogo ila wawe wame saidika kwa kiasi flani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom