Nimpongeze ndugu yangu maggid leo kajitahidi kweli kweli nimemzoea kila akianzisha thread anatimua mbio leo yuko hapa samba samba akidadavua hoja zenu bila chenga.
maggid,Ngongo,
Ahsante sana.
Hakika nimefurahia mjadala huu, maana, tofauti na mara nyingi, naona leo wengi wamejikitika kujadili hoja iliyo mezani badala ya kumjadili mtoa hoja. Ni mwelekeo wa mjadala kama huo wa mwisho ( kumjadili mtoa hoja) ndio mara nyingi hunifanya niishie kwenye kusoma comments tu lakini si kuchangia. Maana, ukianza kuchangia yenye kukujadili wewe mtoa hoja ina maana pia ya kuchangia kwenye kushusha kiwango cha mjadala.
Maggid,
Iringa.
Mkuu. Nadhani hao wanaosema kuwa watu wa Mtwara hawataki gesi isitumike na watu wengine, wanajua fika kuwa hilo si kweli, bali wanasema kwa makusudi tu kupotosha ukweli wa kile watu wa Mtwara wanachokitaka. Wanapotosha usemi huo ili jamii ione kuwa watu wa Mtwara hawana hoja za msingi na ni wachoyo.
Kitu amacho watu wa Mtwara wanachokitaka ni gesi kufuliwa pale pale Mtwara ili kuongeza ufanisi wa kiuchumi wa sehemu hiyo kwa sekta mbalimbali. Hakuania haja ya kujenga bomba la gesi ipelekwe mbali wakati kuna uwezekano wa kufuliwa hapo hapo.
kiongozi kwani Gesi haitakua na matumizi mengine zaidi ya kufua umeme? na kama yapo vip itasambazwa vip?
Kwani nichofaham PM alikubali kua UMEME utafuliwa Mtwara na pia grid ya taifa itafika Mtwara na ndivy alivyorudia JK jana wakati anafungua barabara. sasa fujo zinatokana na nini wakati walikubaliana PM umeme utafuliwa huko.

Siongelei matumizi ya gesi wala chochote kitokanacho na hiyo gesi. Ninachoongelea hapa ni maneno ya viongozi kutuambia sisi wananchi kuwa watu wa Mtwara wanataka watumie hiyo gesi peke yao, na Watanzania wengine wasifaidike. Niliposikiliza manung'uniko ya watu wa Mtwara sikuelewa hivyo. Hata katika kutaka kuelimisha umma, kuna upotoshaji dhahiri wa habari. Kufanya hivyo si vizuri kwani kunaleta hisia za wananchi kutokuamini kauli za viongozi na serikali kwa ujumla.
....swadakta ulichosea..! kinachoendelea mtwara ni tatizo pana ambalo kadri muda utakavyoendelea ndivyo, litakavyozidi kukua, labda tu...! (siasa na) wanasiasa waache kucheza mchezo wa siasa kupitia haki za wanamtwara juu ya gesi inayotoka mtwara"....vijana wa kawaida wa mtaani wa mtwara kwa kiasi kikubwa hawajaeleweshwa vya kutosha namna mipango iliyopo kuhusiana na gesi,(ipo) itakavyoinufaisha mtwara, na wakazi wake,( na lindi na wakazi wa lindi pia)..lakini pia, maandali na mikakati ya kivitendo kuwaandaa vijana wa mitaani wa mtwara kuingia katika( chambilecho, rais jakaya kikwete) uchumi mkubwa wa gesi inaelekea ni ya kusuasua, ikiwa imeachwa mbali na mikakati, na maandalizi ya wanasiasa, na wajanja wengine katika kuwaandaa vijana " wa kawaida wa mitaani" kufanya yanayofanyika , na tunayoyashuhudia sasa..!..kwa kina sisi ambao tunayumba na ukweli, sasa tuko kwenye fursa ya kushuhudia ukweli wa "kauli tata" iliyowahi tolewa na wanasiasa( nadhani wa vyama pinzani na kinachoongoza nchi), kwamba tatizo ni udhaifu wa raisi...na kama anavyotufundisha marehem shaaban roberts katika kazi yake ya " adili na nduguze", kwamba mbwa wa msasi mkali, ni wakali kama msasi mwenyewe..basi na tutazame...!Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; Hell is the other people Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.
Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ngombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.
Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.
Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.
Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.
Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.
Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.
Ndugu zangu,
Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.
Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.
Tunajifunza nini?
Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.
Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.
Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.
Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.
Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea Gesi ya Mtwara!?
Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.
Maggid Mjengwa,
Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
Huyu Jamaa, huwa ni ******* sana, Kila makala / andiko lake anaanza mara oh, "nikiwa jongging", mara... "wazo la Leo", mara "Ya..na mtazamo wangu." mara.."Tafakari ya usiku" huwa hana lolote lile, mtun makini ukimfuatilia haina haja wala ya kusoma makala za maggid wala thread zake zinazokuja kwa jia ya matangazo ya kiji-blog chake.