Tunajifunza nini?
Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.
Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.
Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.
Maggid Mjengwa,
Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
'.........
Neno La Leo: Mtwara Tunagombania Kivuli....'
Kejeli kama hizo hapo kwenye kichwa cha habari, ndio zinazoamsha hasira za wana-Mtwara.
Juzi juzi waziri wa nishati aliwaita wana-Mtwara kuwa ni chura..!!
Kwa nini ?? kwa sababu wanapigania haki yao ya kufaidika na gesi inayochimbwa huko Mtwara..!!
Ulichoandika hapo kwenye blue, ni uwongo mkubwa wa shetani...
Wana-Mtwara hawajawahi hata siku moja kusema kuwa gesi ni yao peke yao..!!
Wanachotaka ni kufaidika na gesi hiyo inayochimbwa Mtwara.
Wewe mleta mada maggid unashiriki kwenye udhalimu wa serikali..!!
Sera ya CCM inasema kuwa raslimali za nchi ziongezewe thamani pale pale zinapozalishwa..!!
Sasa kwa nini gesi isiongezewe thamani kule Mtwara..??
Mleta mada upo hapo ..??
Mleta mada unaandika kama vile wewe ni msemaji wa serikali..!!
Unawaponda wana-Mtwara kuwa wanapigana na kivuli..!!
Kwako wewe mtu kudai haki ya maendeleo ni kupigana na kivuli..!!
Kwako wewe mleta mada, mikataba mibovu ya gesi ni bora kuliko haki ya wana-Mtwara..!!
Umelaaniwa wewe mleta mada maggid pamoja na wale wote wanaoendeleza udhalimu dhadi ya wana-Mtwara.
Mungu ibariki Tanzania.
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; " Hell is the other people" – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.
Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng'ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.
Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.
Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.
Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.
Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.
Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.
Ndugu zangu,
Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.
Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.
Tunajifunza nini?
Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.
Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.
Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.
Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.
Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ' Gesi ya Mtwara!'?
Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.
Maggid Mjengwa,
Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
Nilikuwa nimekasirishwa sana na upotoshaji wa huyu ndugu lakini baada ya kusoma komenti yako nimecheka sana.. maggid, Who is next after David Mwangosi? RIP. maana swwaiba kamuhanda amesema kuna wandishi 7 watakufa Iringa, vipi umemuanda yupi baada ya Mwangosi?
Vipi leo Jogging?
Kwa muda mrefu sasa, nimekuwa ni msomaji wa makala za Bwana Majjid Mjengwa hasa katika gazeti la raia mwema, lakini kadiri siku zinavyoenda nimejikuta naanza kuzipuuza na hata kufikia hatua naziruka tu na kusoma mambo mengine.
Ndugu Majjid ameamua kukengeuka na kuacha weledi na kukubali kutumika katika propaganda nyepesi nyepesi ambazo hazija tija.
Kinachoniuma zaidi ni upotoshaji wa makusudi unaofanywa na watu kama akina Majjid.
Mfano mmojawapo ni pale juu nilipopapaka rangi nyekundu,
Ni lini wanamtwara wamedai kuwa gesi iwe ni ya wanamtwara tu?, Kwa uelewa wa Majjid, kudai kuwa iwanufaishe wana mtwara ndio kumaanisha kuwa iwe ni ya wanamtwara tu?
Ina maana wanavyotaka kuisafirisha kupeleka Dar es salaama itakuwa ni ya wana Dar es salaama tu?.
Acha kutumika bwana Majjid.
Na katika dunia hii kuna wenye kusikia wanavyopenda kusikia, kuna wenye kusoma wanavyopenda kusoma, na kuna wenye kuona wanavyopenda kuona. Wanadamu hawa huwa hawana mengi mapya ya kujifunza zaidi ya yale wanayodhani wanayajua. Sasa hilo ni tatizo la wenye matatizo hayo.
Very logical. you are a Great Thinker (GT).Mjengwa umeeleweka vyema;
Hakika Serikali na viongozi wake hawafikiri; wanatumia spinal code kwenye maamuzi ya mambo magumu; nasisitiza kwamba gesi ya Mtwara ni ya watanzania wote; na kwakuwa Mtwara pia ni Tanzania kuna haja gani ya kuisafirisha hadi Dar? Tafakari.
Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.
Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea Gesi ya Mtwara!?
Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.
Wataachaje kushabikia wakati wanafaidika kupitia vurugu na damu za watu. Ndio TZ hiyoUmeeleweka mkuu.
Ingawapo wapo watakaokuja kishabiki zaidi.
Lini watu wa Mtwara walisema gesi ni yao tuu? Upotoshaji huu ndio unaoamsha hasira kwao. Maana kwa makusudi mazima serikali (baadhi ya viongozi) wanapandikiza hilo kwa malengo yao na watu wa Mtwara wameshalielewa.
SULUHISHO; Ushauri wa kambi ya upinzani kuhusu kukaa pamoja na wadau wote na kujadili ndio suluhisho pekee.