hapo kwenye red ndicho WanaMtwara wanachokikataa maana watu wanasema hawafikiri. Wakiongea wanasiasa wanasisitiza kuwa ni uchochezi, hawafikiri, watumie busara. Kwa hiyo watumie busara gesi iondoke!? Kwa uelewa wao wanaona hiyo ndio njia sahihi ya kujieleza baada ya kupuuzwa. Kumbuka ni wanasiasa ndio wanaingia mikataba ambapo wataalamu wanachukua nafasi ndogo sana na hao wanasiasa ndio wamaifanya nchi hii katika miaka 50 ya kuwepo kuwa tofauti na Kenya, Uganda, Rwanda nkNa hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng'ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.
Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.
http://mjengwablog.co.tz/
nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.
Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara.
Mkuu. Nadhani hao wanaosema kuwa watu wa Mtwara hawataki gesi isitumike na watu wengine, wanajua fika kuwa hilo si kweli, bali wanasema kwa makusudi tu kupotosha ukweli wa kile watu wa Mtwara wanachokitaka. Wanapotosha usemi huo ili jamii ione kuwa watu wa Mtwara hawana hoja za msingi na ni wachoyo.Sidhani sana kama wana mtwara wanasema hawataki ges itumiwe na watu wengine nje ya mtwara. Nadhani kuna haja ya kufanya utafiti na kuja ni nini hasa wana mtwara wanakitaka. Wakati mwingine tunafanya makosa kuamini au kutegemea mawazo au sweeping statements za wana siasa akiwemo muheshimiwa Rais JK kujudge mambo.
no ges hawawez wakafaid wana mtwara pekee!watanzania wengine watafaid ges ya mtwara pale ambapo gas ile ita badilishwa kua umeme kwa pale pale mtwara so watanzania wengine watapata electric energy kwa njia ya nguzo!
-ata gesi yote ikitumika pale pale mtwara kwa shuguli za kiuchumi serikal si itakusanya kod na kwa kutumia iyo kod watanzania wengine watapata mgao wao kwenye bajet
Na pata wasi wasi kama unaelewa ulicho andika na nakuamini sana kwa uwezo wako wa kueleaw na kuchambua mambo, lakini kwa hili kuna walakini, kwani nani kasema gesi iwe ya wana mtwara tu, kinachopigiwa makele ni kuto kufaidika, na tanzania ya leo wahamiaji wa Dar es salaan ni wengi kuliko wenyeji, kama ilivyo mtwara kunawatu wa makabila tofauti...hivyo kwa vyovyote kusema gesi ni ya wana mtwara ni kuongea hewa.
kwanini hiyo gesi isiwe mtwara ilikupanua shughuri za kimaendeleo za nchi?
na watu wa mtwara wana akili timamu kama walivyo hao wanao ng'ang'ania kila kitu