Bado hainiingii akilini kuwa mbunge amekamatwa kwa uchochezi wakati yeye yupo upande huohuo wa serikali na hata walivyozindua kiwanda cha saruji kauli za mbunge huyu huyu zilionesha wazi kua yupo upande wa serikali,kukamatwa kwake kwa mtazamo wangu wanataka kuwafariji wananchi kuwa sio viongozi wapinzani peke yao ndio wanakamatwa bali hata viongozi wa ccm ili waendelee kuwa na imani na ccm na hasa wanatamani sana wananchi wawachukie wale viongozi waliounda umoja wa masuala ya gesi,ninatamani sana ule umoja waliouonesha wananchi kwenye masuala ya gesi basi uonekane kwenye chaguzi zijazo ebu tubadili aina ya mboga wanakusini tuachane na ccm kwanza na tuangalie upande mwingine unanogaje.
hiyo ndiyo gesi