Mtwara: Amuua Mkewe na kumzika shambani

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Kaimu RPC wa mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo, linamshikilia Shaibu Kuselela 58, mkazi wa kijiji cha Lipalwe halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha kumzika shambani.

====================

ACP Nicodemus Katembo alisema tukio hilo lilitokea Februari 28, mwaka huu, ambapo mwanamume huyo alifanya unyama wa mauaji hayo ya mkewe Amina Mtausi (40) kwa kutumia kitu kinachodaiwa kuwa na ncha kali.

Alieleza baada ya kutekeleza mauaji hayo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuufukia katika shimo shambani kwao kisha kuchukua mpunga na kuupanda juu ya shimo hilo.

Pia, baada ya kutekeleza azma yake alitoweka kusiko kujulikana kutokana na kuhofia kukamatwa na vyombo vya sheria na chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana.

ACP Katembo alisema tukio hilo liligundulika baada ya mdogo wa mtuhumiwa huyo, Omari Saidi alipokuwa akienda kisimani kuchota maji katika shamba hilo na kubaini harufu isiyo ya kawaida.

Alisema alipofuatilia kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikitoa harufu aliona baadhi ya viungo vya marehemu huku sehemu ya mwili ukiwa umefukiwa ndani ya shimo.

ACP Katembo alisema, Said alitoa taarifa kwa vyombo husika kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo kwa kina zaidi.

Pia soma > Atuhumiwa kuua mke na kumzika, juu ya shimo apanda mpunga
 
Duuuh miye penzi likiisha naliogopa kweli, Pumzika mama aliye kuwa mpenzi kakutoa roho inasikitisha sana
 
dah jamaa sijui wanawezaje mtu kakukatia sana viuno kitandani unaanzaje kumfanyia unyama kama huo
 
Kaimu RPC wa mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo, linamshikilia Shaibu Kuselela 58, mkazi wa kijiji cha Lipalwe halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha kumzika shambani.

Bado Mtwara hajateuliwa RPC?​

C2CB9809-EE77-4D1B-B60B-E44FC6FA305A.jpeg
 
Kaimu RPC wa mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo, linamshikilia Shaibu Kuselela 58, mkazi wa kijiji cha Lipalwe halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha kumzika shambani.

LICHADI na Janja weed Njooni muone huku makatili wanaendeleza ukatili wao. Afrika ni Afrika tu.
 
Kweli mkwezi akisifiwa lazima tembo alitie maji.
Juzi tu tulikua na mada humu ya kushinikiza Ntwala ipewe tuzo ya Nobel kutokana na kutokua na matukio ya mauaji.
Naona wana Ntwala wamekasirika wameona kama vile tunawaletea dharau, wameamua sasa kuanza kutuonyesha kua na wao wanaweza vilevile sio kila mara sifa zinaenda kanda maalumu tu.
 
Kaimu RPC wa mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo, linamshikilia Shaibu Kuselela 58, mkazi wa kijiji cha Lipalwe halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha kumzika shambani.

====================

ACP Nicodemus Katembo alisema tukio hilo lilitokea Februari 28, mwaka huu, ambapo mwanamume huyo alifanya unyama wa mauaji hayo ya mkewe Amina Mtausi (40) kwa kutumia kitu kinachodaiwa kuwa na ncha kali.

Alieleza baada ya kutekeleza mauaji hayo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuufukia katika shimo shambani kwao kisha kuchukua mpunga na kuupanda juu ya shimo hilo.

Pia, baada ya kutekeleza azma yake alitoweka kusiko kujulikana kutokana na kuhofia kukamatwa na vyombo vya sheria na chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana.

ACP Katembo alisema tukio hilo liligundulika baada ya mdogo wa mtuhumiwa huyo, Omari Saidi alipokuwa akienda kisimani kuchota maji katika shamba hilo na kubaini harufu isiyo ya kawaida.

Alisema alipofuatilia kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikitoa harufu aliona baadhi ya viungo vya marehemu huku sehemu ya mwili ukiwa umefukiwa ndani ya shimo.

ACP Katembo alisema, Said alitoa taarifa kwa vyombo husika kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo kwa kina zaidi.

Pia soma > Atuhumiwa kuua mke na kumzika, juu ya shimo apanda mpunga
dah jau
 
Huo mpunga ungekomaa, natafakari harufu yake ukipikwa unakuaje..🤔
Lakini inreal sense mtwara na geita ligi yao ya mauaji sio ya kawaida
 
R.I.P Amina

Ila huyu jamaa si yupo dini ya haki angetoa talaka fasta na kuvuta wengine wanne
 
Huyo itakuwa kauwa bahati mbaya ile mwanamke anakwambia kama ww mwanaume kweli niguse unamtisha ngumi anadondoka anajigonga kwenye kitanda ndo ntolee hyo ila mtu hawezi akafanya kama alivyofanya jamaa huyo.
 
Mbeya mwanamke kaua mme

Mtwara mwanaume kaua mke

Kwa hiyo ngoma ni 1-1

Ova
 
Back
Top Bottom