Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,627
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumiliki silaha bila kibali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 27, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, DCP Lucas Mkondya amesema mmoja wa watuhumiwa hao ni mkazi wa Kijiji cha Kitere na alikamatwa na bunduki moja aina ya gobore,maganda 66 ya risasi.
Amesema katika uchunguzi wa awali imebainika mtuhumiwa huyo ni fundi wa kutengeneza silaha za kienyeji na kuwauzia watu wanaojihusisha na uwindaji haramu haramu.
Pia, Kamanda Mkondya amesema mtuhumiwa mwingine ni mkazi wa Kjiji cha Lukula alikamatwa kwa kosa la kupatikana na silaha bila kibali.
“Tulipokea taarifa kutoka kwa wananchi wema kwamba kuna mtu anamiliki silaha kinyume lakini pia anaitumia silaha hiyo katika kujihusisha na uwindaji haramu,”amesema Mkondya.