Mtumishi hewa ni nani?

mtanganyika mpya

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
424
302
Naomba kujuzwa dhana nzima ya mtumishi hewa na mishahara hewa coz kwa sasa ndo imekuwa story ya serikali.

Utaratibu unakuwaje na inakuwaje mtu analipwa mshahara miaka au miezi bili kuwepo kazini.
 
Naomba kujuzwa dhana dhima ya mtumishi hewa na mishahara hewa coz kwa sasa ndo imekuwa story ya serikali.
utaratibu unakuwaje na inakuwaje mtu analipwa mshahara miaka au miezi bili kuwepo kazini.
hawapo kabisa wengine walikufa wengine walipigwachini lakini majina yao yanaendelea kuwepo kwenye pay roll
 
hawapo kabisa wengine walikufwa wengine walipigwachini lakini majina yao yanaendelea kuwepo kwenye pay roll

sasa wa kuwajibika ni serikali yenyewe maana kama mtu hayupo na bado mnashindwa kulitoa jina lake kwenye pay roll mnamlaumu nani?
 
Wapo wa aina nyingi. Nimegundua kuna kundi kubwa la vijana walioenda kusoma au kujiendeleza kielimu ndani na nje ya nchi bila ruhusa toka kwa waajiri wao. Wengi walifanya hivyo baada ya kunyimwa ruhusa ya kwenda kusoma kwa sababu mbalimbali.
Wanahesabika ni watoro lakini wajanja wanakula mishahara yao.
 
Hili ni swala kwanza kabisa kwa kiaongozi yeyote unakabidhiwa Ofisi ama Kampuni fulani kuongoza..Unapoanza kuangalia ni vitu gani vinavyokuwa na cost kubwa kwa shirika wafanyakazi huwa ni namba 1 ama 2 kutokana na nature ya biashara yako...Huwa ni hatua za awali kuitisha parade wafanyakazi wote hata walioko likizo kwa ajili ya kuwahakiki...Hili analolifanya Magu lilipaswa lifanywe tangu utawala uliyopita tena kila baada ya miezi 6 atleast...Wafanyakazi hewa kwa maana rahisi majina yaliyopo kwenye payroll ambayo watu wenyewe hawapo..Majina mengine ni ya kutungwa tu wala si kuwa mtu alikufa ma alistaafu hapana ila ni jina tu limetengenezewa hadi file lake na linapata stahiki zote ili hali hamna mtu kama huyo..
 
Back
Top Bottom