mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,411
- 7,016
Hali? Kuna watu wanadhani ni ajabu na kuwa watumishi wa Mungu wakigombana ujue ni wa shetani na hawatoki kwa Mungu. Siyo kweli. Kugombana HATA kwenye kazi ya Mungu, ni kawaida SANA.
Paulo mtume aligombana na mtume mwenzake Barnaba kufikia mpaka hatua ya kutengana na kila mtu kuangalia biashara zake, huku kisa kikiwa ni kazi hiyo hiyo ya Mungu.
Paulo aligombana na kumchana wazi wazi Petro ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa kanisa muda huo. Paulo hakujali cheo, alimuumbua Mtume Petro mbele ya kadamnasi. Leo hii nani angethubutu?
Achilia mbali visa hivyo hapo juu, kuna vingine vingi zaidi vya Mtume Paulo kugombana na mitume wenzake.
Achilia mbali ile ya kumkataa mtume Marko asiongozane nao... Paulo hakuwa anasamehe kirahisi. Alikuwa mkali sana.
Hakuwa na mizaha wala itifaki kwenye kusem ukweli.
Pamoja na hayo yote, na bado alikuwa na roho mtakatifu. Unajiuliza mtu mwenye hulka ya Paulo anawezaje kuwa na roho mtakatifu?
Leo makanisani ukiwa kama Paulo utaambiwa bado Yesu hajaumbika ndani yako, utaambiwa bado una dhambi, utaambiwa hujaokoka kiukweli, na maneno kadha wa kadha.
Hivyo ugomvi kwenye injili ni kawaida mno, na hiyo haimaanishi kuwa watumishi ni wa uongo kwa kuwa wanagombana. Kanisa la leo limepotosha mno kwa makusudi, mafundisho ili ku favor upande wa viongozi na wachungaji.
Ukiwa na tabia za Paulo wewe si rafiki wa makanisa YOTE ya leo, ya kiprotestanti na katoliki yote. Hata kutengwa utatengwa.
Ndipo hapa tulipofika?? Nahuzunika mno!