MgungaMiba
JF-Expert Member
- Aug 28, 2011
- 999
- 815
Bw Mtulia alichaguliwa na wananchi wa jimbo la Kinondoni kuwa Mbunge wao. Bw Mtulia akajiuzulu ubunge kwa hiyari yake ili aweze kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya. Mimi nilimuelewa vizuri, kwani moja ya kazi za bunge ni kuikosoa na kuidhibiti serikali ili ifanye kazi zake vizuri.
Sasa huyu bwana Mtulia alipoamua kujiuzulu ubunge nikaelewa kuwa aliona hakuna haja ya kuikosoa wala kuidhibiti serikali ambayo yeye anaona Mkuu wake, ambae ni Mh Rais Magufuli, anachapa kazi kiasi cha kumridhisha yeye Mtulia.
Hivyo niliona ni uungwana kwa yeye kujiuzulu kwenye ubunge (ingawa kitendo hicho kilileta maumivu makubwa na vilio kwa waliompigania hadi akashinda) ili ampishe mtu mwingine kwenye nafasi hiyo ili aende akaifanye kazi ya kibunge inavyopasa na yeye akaendelee kumuunga mkono Rais Magufuli kwa njia nyingine atakayoona inafaa isiyokuwa ya kibunge ambayo alijiuzulu.
Ghafla nikashtukia bwana huyu karudi tena kwa watu walewale, wa jimbo lilelile, tena kwa gharama kubwa kutaka tena nafasi ileile ya Ubunge, ndipo nikaona niulize, Je sasa ndio ameghairi kumuunga mkono Rais Magufuli?