mpemba mbishi
JF-Expert Member
- Nov 27, 2011
- 1,132
- 185
Mtuhumiwa wa mauaji ya padri Mushi, Omar Mussa ameachiwa kwa dhamana na mahkama kuu Vuga.
Mahakama Kuu ya Zanzibar imemuachia kwa dhamana ndugu Omar Musa Makame baada ya wadhamini wawili kujitokeza na kumuwekea dhamana ya Shilingi laki 5 kwa kila mmoja.
Dhamana hiyo imekubaliwa na Mahakama, na ndugu Makame yupo nje,hali hii imemfanya Ndugu Makame kuungana na familia,ndugu,jamaa na marafiki ktk kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Baadhi na jamaa na ndugu wameonekana kububujikwa na machozi na kuamini ipo siku haki itatendeka na ndugu yao kuwa huru,kwani wanaamini kesi hiyo alipewa kutokana na misimamo yake ya kisiasa na si kwamba alitenda.
Source: Mimi nikiwa Zenji