GAMBLER
JF-Expert Member
- Nov 22, 2009
- 303
- 11
Mtuhumiwa EPA adaiwa kuandaa harambee CCM
*NI MARANDA, WAMWALIKA RAIS KIKWETE
Sadick Mtulya
MTUHUMIWA wa wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), Rajabu Maranda anadaiwa kuandaa harambee kwa ajili ya kuichangia CCM mkoani Kigoma kwa ajili ya uchaguzi mkuu, harambeee ambayo Rais Kikwete amealikwa kuwa mgeni rasmi.
Habari za kuaminika zimesema harambee hiyo itafanyika Februari 6 jijini Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Maranda, ambaye ni kada wa CCM, ndiye aliyeratibu harambee hiyo.
"Harambee kwa ajili ya kuchangia CCM mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, itafanyika Februari 6, mwaka huu, Maranda ndiye mratibu wa hili jambo na Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi," alisema mpashaji wetu wa habari hizo.
"Na kuna kamati imeundwa kwa ajili ya kufanikisha hilo... Maranda ameteuliwa kuwa katibu wakati mwenyekiti wake ni mzee Iddi Simba."
Hata hivyo, alipozungumza na Mwananchi jana kwa njia ya simu, Maranda alikiri kuwepo kwa kamati hiyo lakini akasema hawezi kuzungumzia lolote kuhusu harambee hiyo kwa kuwa yeye ni mjumbe tu wa kamati.
"Kweli kamati ipo, lakini mimi ni mjumbe na wala si katibu. Siwezi kuzungumza lolote kuhusu hii harambee kwa kuwa sio katibu wala mweyeketi," alisema Maranda.
"Kama unataka maelezo zaidi wasiliana na mwenyekiti au katibu wa mkoa wa Kigoma kwa kuwa wao ndiyo wenye shughuli hiyo. Mimi sielewi chochote kwa kuwa ni mjumbe tu na pia sijahusika na kitu chochote katika kufanikisha harambee hiyo."
Kwa mujibu wa habari tulizonazo kikao cha mwisho cha maandalizi ya harambee hiyo kilifanyika Januari 12, mwaka huu kwenye hoteli hiyo ya kiwango cha nyota tano na habari zinawataja waliohudhuria kuwa ni Maranda, Iddi Simba, mbunge wa jimbo la Muhambwe, Felix Kijiko, katibu CCM Kigoma, Mama Kastiko pamoja Katunda ambaye ni mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam na Kigoma.
Maranda amedaiwa kuhusishwa moja kwa moja na kuandaa harambee hiyo kutokana na kwamba ndiye katibu wa fedha na uchumi mkoani Kigoma.
"Kimkoa yeye ndiye anayepaswa kuweka na kuandaa mipango mbalimbali ya mkoa kupata fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli za kichama mbali na vile vitega uchumi vinavyojulikana mkoani Kigoma. Ndio maana ameshiriki moja kwa moja kuratibu na kufanikisha kufanyika kwa harambee hii," alisema mdokezaji huyo.
Hata hivyo, katibu wa CCM Kigoma, Mama Kastiko alisema kuwa haoni kikwazo kwa mkoa huo kufanya harambee hiyo.
"Cha ajabu nini? Kigoma kufanya harambee! Hili jambo ni la kawaida na linafanywa siku zote, na vyama mbalimbali, taasisi na hata watu binafsi," alisema Kastiko.
Alipoulizwa tarehe ya harambee hiyo, Kastiko alikataa kuitaja kwa madai kuwa bado hawajakuwa tayari kuitangaza hadharani.
"Aliyekuambia hizi taarifa ndiye akuambie na tarehe. Kifupi siwezi kukueleza tarehe ya harambee hiyo kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado na ukifika tutakuiteni waandishi na kukuelezeni," alisema.
Hata hivyo, Kastiko alifafanua kwamba kufanyika kwa harambee hiyo ni agizo la makao makuu ya chama.
"Isitoshe mikoa yote inatakiwa kufanya harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25," aliongeza.
Kwa mujibu wa habari tulizonazo ni harambee hiyo ilipangwa kufanyika kwa siri.
Maranda, Farijala Hussein na wafanyakazi watatu wa Benki Kuu (BoT), Imani Mwakosya, Ester Komu na Bosco Kimela, wamefunguliwa mashtaka ya kula njama na kuiibia benki hiyo zaidi ya Sh207 milioni baada ya kudanganya kuwa kampuni yao ya Russias T Ltd ilipewa deni na kampuni ya General Marketing ya India. Washtakiwa hao wako nje kwa dhamana.