Mtuhumiwa asomewa mashtaka 21

Mtuhumiwa asomewa mashtaka 21

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Na Peter Saramba na Moses Mashalla

Posted Jumatatu,Mei13 2013 saa 20:28 PM

KWA UFUPI

  • Saa moja kabla ya Ambroce kupandishwa kizimbani saa nne asubuhi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas aliitisha mkutano na waandishi wa habari kitendo ambacho kiliwafanya baadhi yao kushindwa kufuatilia vyema tukio hilo.




Arusha. Mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni kuhusiana mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha na kusomewa mashtaka 21 yakiwamo ya mauaji na kujaribu kuua.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kamuzora, mtuhumiwa huyo, Victor Ambrose (20), dereva wa Bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo, Arusha alisomewa mashtaka hayo yakiwamo matatu ya mauaji ya watu watatu waliofariki katika tukio hilo lililotokea Mei 5, mwaka huu.

Wakisoma kwa kupokezana hati ya mashtaka, Mawakili wa Serikali, Zachariah Elisaria na Haruna Matagane walidai Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kimyakimya akiwa chini ya ulinzi wa maofisa wa polisi na hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mashtaka yanayomkabili yanapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 27, mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa amerudishwa mahabusu.

Saa moja kabla ya Ambroce kupandishwa kizimbani saa nne asubuhi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas aliitisha mkutano na waandishi wa habari kitendo ambacho kiliwafanya baadhi yao kushindwa kufuatilia vyema tukio hilo.



Waarabu waachiwa huru

Polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni waliokuwa wakishikiliwa kuhusiana na tukio hilo baada ya uchunguzi uliofanywa na Polisi wa Tanzania, Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na Polisi wa Kimataifa (Interpol) na kubaini hawakuhusika.

Kamanda Sabas aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa raia hao walikamatwa baada ya kutiliwa shaka walipoonekana wakitoka kwenye hoteli moja karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi Arusha, muda mfupi baada ya tukio hilo.

Raia watatu wa Falme za Kiarabu(UAE), walioshikiliwa na kuachiwa wamegundulika kuwa ni watumishi wa Serikali.

Kamanda Sabas aliwataja kuwa ni Abdul Azziz Mubarak (30), (Mamlaka ya Mapato), Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29), (Zimamoto) na Daeed Abdulla Saad (28), ambaye ni Askari wa Usalama Barabarani.

Raia hao pamoja na mwenzao, Al-Mahri Saeed Mohseen (29) kutoka Saudi Arabia, walikabidhiwa kwa Idara ya Uhamiaji kuchunguzwa iwapo waliingia nchini kihalali.

Waliachiwa katika kipindi ambacho Serikali ya Tanzania ilikuwa ikikabiliwa na shinikizo kutoka kwa mabalozi wa nchi wanakotoka wakipinga kukamatwa kwao na kutangazwa kwenye vyombo vya habari. Mabalozi wa nchi hizo za Mashariki ya Kati walifuatana na wanasheria wao kwenda kuangalia hali za watuhumiwa kutoka nchi zao huko Arusha.

Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdalla Momenah aliliambia gazeti la Al-Hayat la nchi yake akidai watu wao alikamatwa kwa hisia tu.

“Tuna matumaini makubwa kuwa watu wetu wataachiwa huru na tutaendelea kufuatilia suala lao hadi tuone mwisho wake,” alieleza Balozi huyo, ambaye akisisitiza asingeondoka Arusha hadi kieleweke.

Kaimu Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi, Vitalis Mlay alisema tayari wageni hao wameondoka nchini kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Raia hao waliingia nchini Mei 4, mwaka huu, siku moja kabla ya tukio hilo la bomu na walifika Arusha alfajiri ya siku ya tukio na kwamba wangekaa nchini kwa shughuli za kitalii kwa siku tatu.



Mtaalamu mwingine alichambua bomu

Ofisa Usalama Mwandamizi katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) ameunga mkono kauli Polisi mkoani Arusha kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba bomu lililolipuliwa halikutengenezwa kienyeji akisema maelezo aliyopata huenda limetengenezwa kiwandani.

Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliyekataa kutaja jina lake, alisema msingi wa maelezo yake ni kutokana na vyuma vilivyotawanyika na kuumiza zaidi ya watu 20.

“Mabomu ya aina hii nayafahamu kwani yanatumika vitani zaidi na ni mahsusi kwa kutupa kwa mkono,” alisema.




 
ustaadh AMBROSE tehe tehe.....aibu tupu,,,kila tukio utaskia waislamu hao hao,,huyu atakuwa ni mfuasi wa kile chama cha KIGAIDI ambacho kiongozi wake yupo jela
 
Afadhali interpol na fbi wapo. Wangekuwa makanjanja wetu, unatupwa ndani miaka 4 afu unaambiwa hakuna ushahidi kuwa ulihusika. Waarabu wangekishuhudia cha mtema kuni!

Sasa hayo mashtaka waandishi hawakuyaandika wakawa wanasubiria allowance ya press conference? Mbona hawasemi hata hiyo mkutano ilikuwa juu ya nini? Na hakuna hata mmoja alieona bora akose press conference soda and allowance akimbilie mahakamani?

Safari bado sana.
 
Mbona mashtaka ni mawili tu? Hilo la kuua na la kujaribu kuua, hebu ainisha hayo yaliyobakia.
 
Kwa kifupi ni kwamba watuhumiwa wengine wote wameachiwa huru na kuruhusiwa kuondoka nje ya nchi! Pole sana kijana Ambrose!!!!!
 
Kwa vile mtuhumiwa kafikiswa kwenye vyombo vya kisheria ukweli hautajificha kamwe mbichi na mbivu zitafahamika tu.
 
Mkuu umetuambia mashitaka ni 21halafu umetaja mawili mengine ni yapi.
 
serikali dhaifu na coward utaijua tu always going after easy and soft target yaani ni mtoto huyu ndio imeona imgandamize(scapegot) ili kuficha udhaifu wa kushindwa ku deal hasa na watu waliousika na mpango mzima wa bomu la arusha. yaani mtoto dereva wa bodaboda maskini kutafuta kwake riziki ndio kumemponza kugeuzwa kuwa cover up ya serikali kuwajibu baraza la wakristo kuwa tunashugulikia waalifu wa mabomu hapa ndio mjionee jinsi jakaya kikwete alivyo msanii.
 
Watuhumiwa waislamu wote wameachiwa huru, amebaki kijana mkristo Ambrose!!! Mshishangae order ikatoka ikulu kwamba huyo kijana anyongwe haraka ili kuthibitisha kwamba Kikwete yuko serious katika kupambana na ugaidi. Yetu macho!!
 
Kweli hujafa hujaumbika kijana wa watu namhurumia sana nchi hii hamna haki, bora kuishi syria kuliko Tanzania.
 
Kweli hujafa hujaumbika kijana wa watu namhurumia sana nchi hii hamna haki, bora kuishi syria kuliko Tanzania.
Mkuu unamaana gani na hiyo kauli yako,kama unmpango kwenda syria hamna haja ya kutangaza nenda tu mkuu.
 
Kwani neno gaidi maana yake nini? Kwa nadharia ya kawaida kwenye neno gaidi popote duniani futa kwenye akili yako weka muslim, sasa huyu jamaa kama sio muslim afutiwe kosa la ugaidi na afunguliwe mashtaka ya kuuwa na kujaribu kuua,ndio itaeleweka vizuri

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Wenye mtandao wa Ugaidi ni akina PONDA hata document zinaonesha, cha ajabu wanamuachia huru
 
Makosa umexema yako ni 21. Lakini umebainisha makosa 2, hayo 19 yako wapi? Na wakosaji walikuwa 9 wanne wa wameachiwa je wale wanne ukimtoa victor mbona hamelezi ni kina nani, Na walihusikaje?.
 
Ufanisi wa shughuli :-

quote_icon.png
By Hiroshima
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013

Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.

Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

Rai hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen. Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo.

Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao katika upelelezi wa shauri hilo.

Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.

Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa kukamatwa kwa watu hao.


ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.
 
Huyu mtu anayechochea ugaidi ameshakamatwa?

[video=youtube_share;BaJHhlIdXK8]http://youtu.be/BaJHhlIdXK8[/video]
 
Watuhumiwa waislamu wote wameachiwa huru, amebaki kijana mkristo Ambrose!!! Mshishangae order ikatoka ikulu kwamba huyo kijana anyongwe haraka ili kuthibitisha kwamba Kikwete yuko serious katika kupambana na ugaidi. Yetu macho!!
Ama kweli wahalifu ni waisilam tu. Yaani imekua ajenda kwanini waisilam wameachiwa hata kama hawana hatia? Basi tuiombe serikali imuachie mtuhumiwa kwakuwa imani yake haina wahalifu na iwashike waisilamu na kuwanyonga bila kufuata utaratibu wa kisheria. Tuache kuangalia maswala makubwa kama haya kwa ushabiki wa kidini au kisiasa maana maadui zetu wanaweza kutumia mwanya huu kutufarakanisha. Muhalifu ni muhalifu tu haitegemei imani yake aweza kuwa muisilamu au imani nyingine.
 
Back
Top Bottom