Mkuu
BIG X,
Karibu kila mtu huzaliwa na "akili"..nikimaanisha uwezo wa kufikiri.Lakini mara baada ya kuzaliwa kuna tofauti zinaweza kujitokeza(hata kwa wale waliozaliwa siku moja na maeneo sawa).
Kuna makundi mawili unayoweza kusema ya "watu wenye akili"
Mwenye akili-I (Smart, Intelligent)
Hii huelezea uwezo wa ubongo wa mwanadamu katika kufanya kazi(Person's mental ability).Na hapa ndipo pale tunaposema "fulani ana akili"..yaani mwanafunzi fulani ana akili.Hii ni kutokana na ufahamu, ujuzi(knowledge, skills).
Aina hii ya watu wenye akili, hutokana na kusoma, kujikumbusha, na kufaulu hasa kwa mitihani ya mambo yale yaliyosomwa kabla.
Katika kipimo cha Intelligent Quotient(IQ), kuna madaraja(grades) mbalimbali hasa kutokana na Ufahamu, usomi(Knowledge) ambayo mtu anayo tayari.
Mwenye akili-II (Busara,Hekima):
Huyu anakuwa na uelewa, na mambo yake yako kimpango, mkakati, hata kama ni jambo dogo au katika mazingira magumu...yaani, uwezo wa kufanya maamuzi(hasa magumu) na kuamua kufanya jambo(ukiwa na sababu kwa nini unafanya, muda gani, kwa namna gani), na ushauri.
Pia aina hii ya "akili" hutokana na kuishi muda mrefu, uzoefu mwingi/mkubwa mazingira mbalimbali.mf. mara kadhaa watu husemai wazee wanahekima/busara(hasa kutokana na uzoefu wa mambo aliyowahi kuona/kusikia/kufanya kabla ya wale aliowatangulia)..hata kama hakuwahi kuwa shule.
Hivyo basi makundi yote haya tunawaita wenye akili, ikiwa kundi la kwanza hutegemea kuwa na uwezo kwa ufahamu ulioupata tayari na kundi la pili kutokana na uzoefu.Hata hivyo baadi ya watu huweza kuwa katika makundi yote.