Mtu mmoja akutwa amefariki ndani ya basi

naliwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
479
Reaction score
1,065
Kwa hali yakushangaza mtu mmoja ambae alikuwa akitokea Dar kwenda Mpwapwa, Dodoma akutwa amefariki dunia wakati basi ilipotia Nanga kwenye stendi ya busi ya wilaya ya Mpwapwa

Mtu huyo inasemekana alivyokuwa njiani alikuwa na mafua makali na pamoja kuhema kwa shida.

Mungu tusaidie
 
Hatari sana,hapo basi zima watakuwa hatarini..Mungu tunusuru
 
Hatari Sana watu wamejawa na taharuki kweli kweli,dar inatakiwa lock down ya haraka Sana tutashudia mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vifo vya namna hiyo vimekuwa vya kawaida kwa waathirika wa Covid 19. Wanasema ukifikia stage ya ARDS, bila Respiratory Ventilator, una only 20 minutes before death.

Huko Ecuador, maiti nyingi za waliofariki kwa Covid 19 zimekuwa zikiokotwa kwenye mabasi, vituo vya mabasi na majumbani kiasi cha kushindwa kupata hata takwimu halisi za waliokofa na kuugua.

Huko Kahama, nako kuna kisa kinachunguzwa. Kuna mchina na mkewe walichukua chumba hotelini. Wahudumu waligundua mchina mwanamke alikuwa ni mgonjwa hasa japo hakusema. Walipoujulisha uongozi wa hotel, walichukuliwa kwenda hospitali. Uchunguzi unaendelea lakini hwakuruhusiwa kurudi hotelini japo walikuwa wamekwishalipia kwajili ya kukaa siku kadhaa. Kuna hisia walitaka kuifanya hoteli ndiyo isolation place yao.

Ushauri: Kipindi hiki, kama siyo lazima sana, ni aheri kujizuia kusafiri. Na ukisafiri, kama una usafiri binafsi, ukichoka, pumzika ndani ya gari kuliko kulala hotelini.
 

imeshaisha hiyo..watawapatia wapi hao watu????cyo kwa Tz....mbona kazi tunanyo..tusubiri na dodoma nayo iteme...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…