Mtu mmoja ajinyonga nyuma ya jengo la bodi ya korosho mkoani Mtwara. RPC akanusha tukio kuhusiana na korosho

Kuhusu hili la mazao ni vizuri ikatafutwa njia ili mkulima wa Tanzania aweze kufaidi jasho lake. Kimasingi mimi nilishawahi kuwa mtoto wa mkulima, nina machungu sana na jinsi wanavyofanya kazi kwa mazingira magumu halafu kipato kidogo. Kuhusu hili la mimba, kama umesoma shule za Tanzania, unafahamu kuwa hakuna Binti anayepata mimba baadaye arudi shule, wamekuwa wakiondoka wenyewe/kuondolewa hakukuwa na sababu yoyote ya kuutangazia umma. Hata hivyo, Rais naye ni Binadamu, ana upungufu wake. Tunachotakiwa kufanya ni kuangalia kama upungufu ni kiasi gani ikilinganisghwa na mazuri, Binafsi naona upungufu ni mdogo, tatizo ni washauri wake.

Tunayajua madhara ya watu wa kati katika biashara yoyote. Hata watu tunaopangisha nyumba hawa madalali usifikiri tunawapenda. Wanatudhulumu.... Lakini maamuzi tunayafanya bila tafiti.


Tuna bahati mbaya saana...Kwa heri mkuu...
 
Siwezo mfanyia kazi Great thinker!
Una uwezo wa kujua alipokosea ila huna uwezo wa kusahihisha....kazi kweli kweli. Nakukumbusha tu kwamba .... Kuna shule ya vitabu na shule ile ambayo ni real life
 
MTU MMOJA AMEJINYONGA NYUMA YA BODI YA KOROSHO MKOANI MTWARA.

Mtu huyo mwenye jinsia ya kiume, bado ananing'inia kwenye mti wa Muarobaini kwenye kichaka kilichopo nyuma ya jengo la BODI YA KOROSHO Manispaa ya Mtwara mikindani na sababu bado haijajulikana.

Jeshi la polisi wameshafika maeneo haya ili taratibu zingine zichukuliwe.

View attachment 970227
Mbona sioni jengo hapa, naona vichaka na watu. Ingefaa ikawa "......kwenye vichaka karibu na yalipo majengo ya ofisi za Bodi ya Korosho"
 
Baada ya tukio la mtu mmoja kukutwa amejinyonga mtaa wa maduka makubwa mkoani Mtwara, kwenye kichaka kilichopo nyuma ya jengo la Bodi ya Korosho, Kamanda wa Polisi mkoani humo amesema kwamba mpaka sasa tukio hilo halina uhusiano na suala la korosho japo bado uchunguzi unaendelea.
Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda wa Polisi, ACP Blasius Chatanda amesema kwamba Marehemu aliyejulikana kwa jina la Mosses Malolela, 'Wadasani' alikutwa amejinyonga saa nane usiku wa Disemba 16 mwaka huu huku kukiwa hakuna ujumbe wowote aliouacha.
Kamanda Chatanda amesema kwamba marehemu Mosses (30), ni mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma na kwamba bado haijajulikana ni jambo gani ambalo lilimpeleka mkoani Mtwara hivyo bado wanafuatilia.
Akijibu swali la kama marehemu Mosses ni mmoja kati wa wafanyabiashara wa Korosho wasio waaminifu, maarufu kama wanunuzi wa 'Kangomba', Kamanda Chatanda amesema, "Mpaka wakati huu hakuna taarifa zozote ambazo zinahusisha tukio hilo na suala la korosho. Kwa kuwa bado tunaendelea na uchunguzi tutajua sababu za kujinyonga ingawa siku hizi matukio ya kujinyonga yanasababishwa na mambo mbalimbali yakiwepo msongo wa mawazo, hali ya maisha lakini pia mapenzi nk, japo kwa marehemu Mosses bado hatujafahamu ni nini".
Mwili wa Marehemu Mosses upo katika sehemu ya kuhifadhia maiti mkoani Mtwara baada ya kutolewa juu ya mti ulipokuwa ukining'inia baada ya kujinyonga kwa kutumia waya.
 
Baada ya tukio la mtu mmoja kukutwa amejinyonga mtaa wa maduka makubwa mkoani Mtwara, kwenye kichaka kilichopo nyuma ya jengo la Bodi ya Korosho, Kamanda wa Polisi mkoani humo amesema kwamba mpaka sasa tukio hilo halina uhusiano na suala la korosho japo bado uchunguzi unaendelea.

Kamanda wa Polisi, ACP Blasius Chatanda amesema kwamba Marehemu aliyejulikana kwa jina la Mosses Malolela, 'Wadasani' alikutwa amejinyonga saa nane usiku wa Disemba 16 mwaka huu huku kukiwa hakuna ujumbe wowote aliouacha.

Kamanda Chatanda amesema kwamba marehemu Mosses (30), ni mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma na kwamba bado haijajulikana ni jambo gani ambalo lilimpeleka mkoani Mtwara hivyo bado wanafuatilia.
Akijibu swali la kama marehemu Mosses ni mmoja kati wa wafanyabiashara wa Korosho wasio waaminifu, maarufu kama wanunuzi wa 'Kangomba', Kamanda Chatanda amesema, "Mpaka wakati huu hakuna taarifa zozote ambazo zinahusisha tukio hilo na suala la korosho.
"Kwa kuwa bado tunaendelea na uchunguzi tutajua sababu za kujinyonga ingawa siku hizi matukio ya kujinyonga yanasababishwa na mambo mbalimbali yakiwepo msongo wa mawazo, hali ya maisha lakini pia mapenzi nk, japo kwa marehemu Mosses bado hatujafahamu ni nini".

Mwili wa Marehemu Mosses upo katika sehemu ya kuhifadhia maiti mkoani Mtwara baada ya kutolewa juu ya mti ulipokuwa ukining'inia baada ya kujinyonga kwa kutumia waya.

...............,....................

...USIKU UTAKAPOKWISHA...
 
Kamanda amesema suala hilo halina uhusiano na Koro-show, kwani kuna mtu alihusisha Koroshow?
 
Kama halina uhusiano na korosho kwa nini ajinyonge karibu na hilo ghala?, kama sio machumgu yakudhulumiwa!
 
Hapo chanzo ni korosho tu hamna kingune.
Na huenda aliacha ujumbe polisi wakaamua kuuminya
 
'Inasadikika amejinyonga'

Hivi ukisikia mshabiki wa manchester united kujinyonga ile jana itakuwa ni nini kama sio kile kipigo cha liverpool? Kwakuwa huko Mtwara kuna suala la korosho hapo utauliza nini?
 
Back
Top Bottom