Mtu asiyejulikana agawa fedha jijini Dar

Mtu asiyejulikana agawa fedha jijini Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,850
Mtu asiye julikana.jpeg
attachment.php




Bajaji wakiwa kwenye foleni kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha

Mwanaume mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.

Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.

Akizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.

‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka bila kusema lolote’ alisema Subira.

Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgao huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.

Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha madereva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.

CHANZO JAMBO TZ

Mwenyeezi Mungu amlipe Pepo huyo Kijana inshallah Wanachama Wenzangu Semeni Ameen.
 
fedha za "mchele" hizo kutafuta public sympathy kama Escobar alivyokuwa anafanya kule Colombia enzi hizoo...atakuwa tayari kwenye interpol list ya most wanted drug traffickers so anatafuta protection cum immunity sort of! hebu jaribuni kuchunguza mienendo yake na link kati yake na zile kilo 120 za heroin zilizokamatwa J'burg, mtapata picha kamili
 
Back
Top Bottom