Mtu anatakiwa ku-format hii nchi

Mtu anatakiwa ku-format hii nchi

Joined
Oct 25, 2012
Posts
30
Reaction score
7
KWA KUWA WALIOKO MADARAKANI WENGI WAO WAMEHARIBIWA NA RUSHWA NA KILA NAMNA YA UBAYA, MTU ANATAFUTWA WA KUFORMAT NCHI HII ILI VIRUSI WOTE WAFE NA IANZE UPYA.:whoo:
 
mhhhjjj no no ikiwa formatted hatutabaki at least tupate tu anti virus Mpwa
 
mhhhjjj no no ikiwa formatted hatutabaki at least tupate tu anti virus Mpwa
MTU AMBAYE HAJAWAHI KULA RUSHWA HATA MARA MOJA ANATAKIWA KUWA RAIS NCHI HII, PIA ASITEMBELEE NCHI HIZO ZA KIBEPARI, MAKAMU WAKE NDO AWE ANASAFIRI MAANA AKIENDA HUKO ATALUBUNIWA.
:whoo:
 
Mi nahisi kabla yakui-format tuifanyie kwanza de fragment.

A lie has speed,but truth has endurance
 
Mia. Naunga mkono hoja.

Tulikwishapotea! Sasa Turudi


Taifa ni kama Nyumba

Ujenzi wa nyumba bora huanzia kwenye usanifu ambapo pamoja na mambo mengine muonekano wake (appearance) ikijumuisha mazingira yake (landscape) huonekana kabla hata msingi kuchimbwa. Hii ina maana kwamba mjenzi anajua nini kitapatikana baada ya ujenzi kukamilika.

Taifa lolote ambalo halijasanifiwa hugeuka kuwa kituko. Tanzania ya leo ni kituko! Nashawishika kuamimi kuwa haikusanifiwa – it happened to exist by default! (ni mtizamo wangu but I stand to be corrected). Nitafafanua:

  • Huwezi kujua mbele ni wapi na uani ni wapi. Tanzania haijulikani kama inaendelea au inarudi nyuma kimaendeleo. Watawala wanasema uchumi umekua wakati wananchi wameendelea kuwa maskini zaidi. Wengine wanapima maendeleo kwa kuangalia barabara na majengo, na wengine kwa kuangalia unafuu wa maisha. Kila mmoja ana tafsiri yake kuhusu maendeleo
  • Hakuna anayejua msingi ni upi. Je ni Ujamaa? Ni ubepari? Ni Ukomunisti?
  • Kila mtu analalamika. Wananchi wanalalamika, watawala wanalalamika, wahisani wanalalamika, viongozi wa dini wanalalamika. Kila kundi linalaumu mwenzake

Kwakuwa hatukuwahi wala hatujaamua kusanifu aina ya Taifa tunalotaka huko tuendako, wakoloni wetu wameamua kusanifu aina ya Tanzania waitakayo. Mifano michache inadhihirisha hili:

    • Kuua utaifa na uzalendo - hujitahidi kutumia mass media (local radio + tv) kwa kutumia Kiswahili kurusha matangazo yao ambayo kwa asilimia kubwa SANA hayazungumzii uzuri wa tz wala mazuri ya tz bali migogoro na vuguvugu nyingine zinazoendelea nchini pamoja na matukio hasi. Wakati huohuo wakijitahidi kupenyeza ama utaifa wao na/au mazuri yanayofanywa na taifa lao. Hii inakwenda sambamba na kufadhili urushwaji wa tamthilia mbalimbali ambazo zinatukuza tamaduni za mataifa ya kwao. Hata soka ya kwao itatangazwa kwa Kiswahili kwenye radio zetu ambapo matokeo yake yako wazi: tunarusha matangazo ya ligi zao tukipuuza za kwetu, hata vipindi vya michezo kwenye tv na radio muda mwingi unatumika kushabikia michezo ya nje. Majarida ya michezo hivyohivyo!
    • Kuua misingi na fikra za kujitegemea kwa uzalishaji mali kwa kupandikiza fikra za kupata utajiri bila kuzalisha. Hapa wanatumia sanaa ya muziki na uigizaji pamoja na ulimbwende katika kuifanya nguvukazi ya taifa (hapa nazungumzia vijana) kukimbilia kutafuta umaarufu wa kitambo kidogo kwa kudhani kujua mistari (lyrics) na kuonekana kwenye tv ndio maisha. Vitu hivi huvutia vijana wengi kwa kuwa vinafungamanishwa na starehe na u-magharibi
    • Kuua mshikamano na udugu kwa kupalilia ubaguzi. Katika hili wamekuja kwa kuvaa ngozi ya kondoo. Wanatumia mbinu za medani kutuchonganisha kwa kisingizio cha haki ama usawa. Kuna vitu kama haki za wanawake, haki za mtoto wa kike, usawa wa kijinsia n.k these may look innocent motives but believe me, they are FATAL! Nani asiyejua kuwa mshikamano katika familia mojamoja huzaa mshikamano wa Taifa? Nani asiyejua kwamba rais na makamu wake hawawezi kuwa na madaraka sawa na nchi ikatawalika? Nani anayedhani familia itatawalika baba na mama wakiwa na madaraka sawa. Watu wengi huamini kwamba ubaguzi mbaya ni wa kabila, dini, kanda au rangi! Ni kweli lakini ubaguzi wa kijinsia ni mbaya kuliko wote kwani hubomoa si taifa tu bali hata mzizi wa taifa ambao ni familia. Katika hili wanafanikiwa kwa kasi katika kutugawa kwa misingi ya jinsia. Mifano michache: Vyama vya kitaaluma vya WANAWAKE (sheria, habari, madaktari n.k) benki ya wanawake, wizara ya wanawake n.k Ukatili wa kijinsia nao umekuwa biased kwa kuhubiri kwamba wanaume ni wakatili, wabakaji n.k na kutegemea kwamba ndoa zitadumu kwa kupanda mbegu hiyo ya uadui kati ya mtoto wa kike na wa kiume.
    • Kujenga uongozi dhaifu wa kitaifa na kitaasisi kusudi iwe rahisi kwao kuingiza sera zao bila kipingamizi. Katika hili wanajenga mfumo wa kutukuza vyeti badala ya maarifa (skills). Wanawapaka watawala mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuwazawadia PhD na kuwamwagia sifa za kufikirika. Matokeo yake ni mashindano ya kuitwa Dkt au Prof ili kuteuliwa kuwa viongozi wa serikali na taasisi za umma bila kujali michango yao ni ipi katika ujenzi wa taifa. Hili linakwenda sambamba na kaulimbiu ya 50-50 kwenye uongozi kwa maana ya gender balance. Tukiweka sifa namba moja ya uongozi kuwa ni jinsia, matokeo yake ni kama yanavyoonekana bungeni leo. Pima mwenyewe matokeo kama uongozi wote wa umma utakuwa 50-50 kwa maana ya namba itakuwaje.
    • Kutuondoa kwenye mijadala yenye maslahi mapana kwa taifa kwa kufadhili peripheral issues zionekane ni core issues. Masuala kama ya ukeketaji, uuzaji wa viungo vya albino kwa minajili ya kupata utajiri n.k ni peripheral issues. Ubora wa elimu, uwekezaji katika kilimo, ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi n.k ni core issues. Ukweli ni kwamba core issues zikipata solution peripheral issues zina-sublime. Lakini local media nyingi zimekuwa zinatoa coverage pana zaidi kwenye peripheral issues ( kwa udhamini wa wakoloni) badala ya core issues. Na hii sio bahati mbaya, it is a calculated move.

Hii orodha siyo exhaustive, ni ndefu nawe waweza kuongezea ya kwako. Nimeainisha haya matano tu ili uweze kujenga taswira ya Tanzania ya miaka 20-30 ijayo. It will be a pure HELL!

Ukweli ni kwamba tumechelewa lakini bado kuna nafasi.
 
MTU AMBAYE HAJAWAHI KULA RUSHWA HATA MARA MOJA ANATAKIWA KUWA RAIS NCHI HII, PIA ASITEMBELEE NCHI HIZO ZA KIBEPARI, MAKAMU WAKE NDO AWE ANASAFIRI MAANA AKIENDA HUKO ATALUBUNIWA.
:whoo:

Arubuniwe kwani yeye amekuwa mtoto ?
 
Duh! Mkuu ukiformat nchi maana yake watu wote tufe including you kije kizazi kipya kabisa. Inawezekana hii kweli??
KWA KUWA WALIOKO MADARAKANI WENGI WAO WAMEHARIBIWA NA RUSHWA NA KILA NAMNA YA UBAYA, MTU ANATAFUTWA WA KUFORMAT NCHI HII ILI VIRUSI WOTE WAFE NA IANZE UPYA.:whoo:
 
Hapo mkuu itabidi kabla ya kuformat tufanye backup ya raia wazalendo wasiyo na mawaa pamoja na pamoja na viumbe hai vyote, wakiwemo wanyama, maana kuformat kila kitu kinakuwa kitakufa kabisa. Hila wale mafisadi, wala rushwa na wezi tuwaache wawe formatiwe.
 
Mmh ni kweli lkn mimi nafikiri tuupgragrade operating system na tuanze upya kabisa. Tuki install OS ya sasa na kamwe tusiyarudishe mafaili ya zamani huenda yakawa na worms. Hii itaongeza ufanisi.
 
Back
Top Bottom