Mtu akiumwa hachangiwi ila akifa michango tele

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
993
782
Poleni na pilika za weekend,

Moja kwa moja naenda kwenye mada.
Naombeni kujadiliana kuhusu jambo hili, eti mtu akiumwa hachangiwi ila akifa michango tele, kwa wakristo unavotoa hata mkono wako wa kushoto usione mbona mnatupatia bahasha tuweke sadaka humo huku nje tukiwa tumeandika majina yetu, je wale wanaohesabu hizo sadaka hawayaoni majina yetu na kiasi tulichotoa, na mengineyo mengi tu ila leo naishia hapo.

Karibuni kwa michango zaidi.
 
Hata hii Mada yako itakosa Mchango wa Hoja kwa vile U hai ila kama unataka tuchangie kufa uone.

Nadhani umeelewa kuna tofauti kubwa kati ya uhai na Kifo. (kifo kinaogopwa kuliko uhai)
 
Lakini ngoja kwanza turudi nyuma, kama kweli kifo kinaogopwa kwa nini watu wasingekua wanafanya jitihada za kumuokoa mgonjwa kwa kumchangia ili asipatwe na kifo hasa kwa wale ambao wanakufa kwa kukosa gharama za matibabu.
 
Watz wamekua makatili sana ,kwa sasa hapa Tz kama una shughuli yako bora uwekeze ili siku ukiumwa hiyo hela ikusaidie kuliko kutumia mapato yako kusaidia ndugu,ukiishiwa utakimbiwa na ukiumwa ndo unaachwa kabisa ufe mwenyewe haya maisha ni unyambisi unyambisi tu
 
Kweli kabsa, nakumbuka kuna ndugu yangu alikuwa anaumwa na ilihitajika kama M 20 ya kumpeleka India ila ilikosekana kabsa hiyo pesa na alivyofariki michango ilikuwa zaidi ya M 50 Gharama ya usafiri na mazishi kwa ujumla bajeti ilizidi kiasi kilichohitajika ili akatibiwe
 
Nani yupo Tayari kutoa pesa zake kwa ajili ya kutibu mtu anaepona? Tunasubiri kutoa kidogo au kikubwa cha Mara moja kuliko kutoa michango ya mara kwa mara kukutibu.
Lakini ngoja kwanza turudi nyuma, kama kweli kifo kinaogopwa kwa nini watu wasingekua wanafanya jitihada za kumuokoa mgonjwa kwa kumchangia ili asipatwe na kifo hasa kwa wale ambao wanakufa kwa kukosa gharama za matibabu.
 
Ukiandika habari kama hizi usianze na majungu "mlikuwa Mnataka 20 nini Milioni, dola, au shilingi?

Kweli kabsa, nakumbuka kuna ndugu yangu alikuwa anaumwa na ilihitajika kama M 20 ya kumpeleka India ila ilikosekana kabsa hiyo pesa na alivyofariki michango ilikuwa zaidi ya M 50 Gharama ya usafiri na mazishi kwa ujumla bajeti ilizidi kiasi kilichohitajika ili akatibiwe
 
Kweli kabsa, nakumbuka kuna ndugu yangu alikuwa anaumwa na ilihitajika kama M 20 ya kumpeleka India ila ilikosekana kabsa hiyo pesa na alivyofariki michango ilikuwa zaidi ya M 50 Gharama ya usafiri na mazishi kwa ujumla bajeti ilizidi kiasi kilichohitajika ili akatibiwe
Umeona mkuu maajabu ya wabongo hayo, sijui ni sisi wabongo tu au ni waafrika wote.
 
Poleni na pilika za weekend,

Moja kwa moja naenda kwenye mada.
Naombeni kujadiliana kuhusu jambo hili, eti mtu akiumwa hachangiwi ila akifa michango tele, kwa wakristo unavotoa hata mkono wako wa kushoto usione mbona mnatupatia bahasha tuweke sadaka humo huku nje tukiwa tumeandika majina yetu, je wale wanaohesabu hizo sadaka hawayaoni majina yetu na kiasi tulichotoa, na mengineyo mengi tu ila leo naishia hapo.

Karibuni kwa michango zaidi.

Kuhudumia wagonjwa sio cost effective.

Wanaogua ni wengi wanaokufa ni wachache. Ikiwa tutaamua kutumia servings zetu kuhudumia wagonjwa wote hatutafika. Ila kifo ni one time event, tukikuzika Leo , kesho huwezi kutuingiza tena gharama ya kukuzika the second time unless jiji/ manispaa wanahamisha makaburi. Ukiumwa Leo tukajichanga haina guranteee kwamba hutoumwa tena, pia michango yetu ya kukuuguza haituhakikishii kuwa utapona,why tuchange Mara mbili, bora tusubiri kuchangia mazishi.

Kuumwa ni continuous , wakati kifo/ mazishi in Mara moja, I can't get a second chance to burry you, I have to do it anyway.

Hata hivyo afya/ huduma za afya ni jukumu lako mwenyewe. Tafuta bima, it is until when you are dead you become our responsibility, kwani tusipokuzika utatunukia tu.

Unapowekeza na kuweka akiba ufikirie na magonjwa ili usije kuleta lawama kwa watu. Bima ya afya ndio mwarobaini. MTU una 40 M bank Ila akili ya kukata bima ya family for 1.5M per year unakosa. Ukiugua 4 months tu akiba inapukutika then unabaki lawama.
Sichangii harusi, sichangiii kuumwa, nachangia mazishi tu baaasi,kupanga ni kuchagua.

Povu ruksa.
 
Last edited:
Kweli kabsa, nakumbuka kuna ndugu yangu alikuwa anaumwa na ilihitajika kama M 20 ya kumpeleka India ila ilikosekana kabsa hiyo pesa na alivyofariki michango ilikuwa zaidi ya M 50 Gharama ya usafiri na mazishi kwa ujumla bajeti ilizidi kiasi kilichohitajika ili akatibiwe
Aacha uhongo labda kama hamkutangaza ugonjwa wake.
 
Na ndo maana kuna michango kedekede ya harusi kuliko michango ya ada!

Akili zetu za kipuuzi sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom