Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,050
- 144,458
Ni imani yangu wote humu tumeishi na wazee katika nyakati tofauti tofauti za maisha yetu. Wazee hawa wanaweza kuwa ni bibi au babu zetu, au wazazi wetu ambao wamezeeka/wamestaafu kazi miaka mingi, n.k.
Tukichukilia mfano wa wazee wanaostafu serikalini na kutimiza miaka kumi na kuendelea baada ya kustaafu, wazee hawa majumbani mwetu sio ndio huwa wanaanza ku-behave kama watoto? Je, si hawa wazee huwa wanapoteza kabisa network? Sasa wanakuwaje viongozi tena Maraisi wa nchi?!
Wazee hawa wa miaka 70 na kuendelea, hata kumbukumbu kwao huwa si shida?
Wazee hawa wa miaka 70 hats kama walikuwa wasomi, baadhi hata hizi smartphone zinawapa shida kutumia?
Je, si kweli kuwa watoto wa wazee hawa ambao ni watu wazima, sometimes hulazimika kufanya maamuzi ya kifamilia bila kuwashirikisha wazazi wao(wazee) wakiamini wazee wakishirikishwa ni ama watavuruga,kukwamisha au kushiriki miwili tu lakini wanakuwa hawana tena mawazo ya kujenga?
Mifano iko mingi na ndio inanifanya niamini watu wenye umri mkubwa kuwa viongozi mfano maraisi wa nchi, huwa si jambo sahihi na kuna uwezekano mkubwa wasaidizi wao ndio hufanya zaidi ya asilimia 80 mpaka 90 ya maamuzi na wao hubaki kubariki tu maamuzi hayo.
Niambieni iwapo Mzee Ruksa angeng'ang'ania madaraka mpaka leo hii kama kina Marehemu Mugabe, maamuzi angekuwa anayafanye yeye?Wote si mnakumbuka kauli zake kwenye msiba wa Mwendazake?
Ni wazi hata Biden atakuwa Raisi jina tu, ila wasaidizi wake ndio watakuwa wanaendesha nchi.
Hata Biblia inampa mwanadamu miongo saba tu ya kuishi halafu sisi wanadamu hatuna ukomo wa umri katika uongozi. Huwa sielewi kabisa.
Hata Mapapa wa Kanisa Katoliki ambao huwa ni wazee, naamini wasaidizi wao ndio huongoza hilo kanisa na wao huwa wako tu kwasababu ni lazima wawepo na watimize baadhi ya majukumu ila huwa wameshapangiwa na kuandaliwa lila kitu wao ni kutekeleza tu.
Huu ndio ukweli japo unaweza kuwa mchungu kwa baadhi yetu.