Mtu akifikisha miaka 70 hapaswi kuwa kiongozi, akiwa kiongozi wasaidizi wake ndio huongoza

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Ni imani yangu wote humu tumeishi na wazee katika nyakati tofauti tofauti za maisha yetu. Wazee hawa wanaweza kuwa ni bibi au babu zetu, au wazazi wetu ambao wamezeeka/wamestaafu kazi miaka mingi, n.k.

Tukichukilia mfano wa wazee wanaostafu serikalini na kutimiza miaka kumi na kuendelea baada ya kustaafu, wazee hawa majumbani mwetu sio ndio huwa wanaanza ku-behave kama watoto? Je, si hawa wazee huwa wanapoteza kabisa network? Sasa wanakuwaje viongozi tena Maraisi wa nchi?!

Wazee hawa wa miaka 70 na kuendelea, hata kumbukumbu kwao huwa si shida?

Wazee hawa wa miaka 70 hats kama walikuwa wasomi, baadhi hata hizi smartphone zinawapa shida kutumia?

Je, si kweli kuwa watoto wa wazee hawa ambao ni watu wazima, sometimes hulazimika kufanya maamuzi ya kifamilia bila kuwashirikisha wazazi wao(wazee) wakiamini wazee wakishirikishwa ni ama watavuruga,kukwamisha au kushiriki miwili tu lakini wanakuwa hawana tena mawazo ya kujenga?

Mifano iko mingi na ndio inanifanya niamini watu wenye umri mkubwa kuwa viongozi mfano maraisi wa nchi, huwa si jambo sahihi na kuna uwezekano mkubwa wasaidizi wao ndio hufanya zaidi ya asilimia 80 mpaka 90 ya maamuzi na wao hubaki kubariki tu maamuzi hayo.

Niambieni iwapo Mzee Ruksa angeng'ang'ania madaraka mpaka leo hii kama kina Marehemu Mugabe, maamuzi angekuwa anayafanye yeye?Wote si mnakumbuka kauli zake kwenye msiba wa Mwendazake?

Ni wazi hata Biden atakuwa Raisi jina tu, ila wasaidizi wake ndio watakuwa wanaendesha nchi.

Hata Biblia inampa mwanadamu miongo saba tu ya kuishi halafu sisi wanadamu hatuna ukomo wa umri katika uongozi. Huwa sielewi kabisa.

Hata Mapapa wa Kanisa Katoliki ambao huwa ni wazee, naamini wasaidizi wao ndio huongoza hilo kanisa na wao huwa wako tu kwasababu ni lazima wawepo na watimize baadhi ya majukumu ila huwa wameshapangiwa na kuandaliwa lila kitu wao ni kutekeleza tu.

Huu ndio ukweli japo unaweza kuwa mchungu kwa baadhi yetu.
 
Age is nothing but a number mfano Biden huwez mfananisha na vijana wa ccm upstairs
 
Kaka mtazamo wako ni wa nyuma kidogo.

Zamani mzee alifanya kazi nzito maishani mwake, na wengi walikwisha nguvu kuanzia miaka 50 au 60.

Maisha yamekuwa tofauti. Katika mazingira yaliyobadilika, wako "wazee" wenye nguvu kabisa. Huwezi kusema kwa wote, lakini mifano ya kinyume cha hoja lako iko tele.

Mfano bora ni Konrad Adenauer aliyekuwa kiongozi wa serikali ya Ujerumani akiwa na umri wa miaka 73 mnamo 1949.

Aliendelea hadi 1963 alipokuwa na miaka 87 - wakati ule alipaswa kujiuzulu na kukabishi mamlaka kwa makamu wake.

Alisimamia inayoitwa "miujiza ya uchumi ya Ujerumani" katika miaka ya 1950s ambako nchi hiyo ilirudi kuwa na nguvu kubwa y akiuchumi baada ya uharibifu mkubwa wa vita kuu ya pili.

Kweli kuna mifano mibaya ya viongozi wazee, tumkumbuke Mugabe mzee aliyekataa kuachana na madaraka au labda pia M7ni!
 
Discrimination on the basis of age. Kwa mwendo huu hata makampuni ya kuuza magari yatakataa kuwauzi wazee kwamba hawawezi kuendesha tena. Weka term limit kwenye katiba halafu acha demokrasi inchukue mkondo wake.
 
Rais wa sasa wa Marekani ameingia madarakani akiwa umri wa miaka 78.
Tofautisha wazungu na waafrika,
Ndugu yenu leo Alfa Konde Raisi wa Guinea amenyakuliwa Kama kuku,Tuliona kwa Mgabe,Alliy Bashili,Raisi wa Mali na Sasa tutaona kwa Kagame na M7.
 
Discrimination on the basis of age. Kwa mwendo huu hata makampuni ya kuuza magari yatakataa kuwauzi wazee kwamba hawawezi kuendesha tena. Weka term limit kwenye katiba halafu acha demokrasi inchukue mkondo wake.
 
Unachokisema hakina uhalisia yoyote, wenda kama una hila binafsi.
Chukulia nyumbani kwenyu mzee wako hana 70+ utamchukulia poa kwamba ni mzee asiongee hapana.
Issue kubwa hekima kama bado ipo its okay
Mfano mdogo ni
Nelson mandela halipewa nchi akiwa na umri gani. Lakini hakufanya makubwa,
Joe Biden saivi hana- approach 80yrs vip
Maamuzi yake unayaonaje?
 
kuongoza ni akili zaidi kuliko nguvu. wako watu wana miaka 90+ lakini akili ziko nzuri kabisa. wako vijana wana nguvu lakin akili ya kuongoza ni zero.hivyo inavary kati ya mtu na mtu. mawazo ya kugawa watu kiumri bila kuzingatia uwezo si vema sana. katiba inataja kuwa na akili timamu na si kuzeeka
 
Back
Top Bottom