Mtu agonga treni Tabata relini

piper

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2012
Posts
3,253
Reaction score
613
Habarini wakuu nimepata taarifa toka kwa mdogo wangu aliyekuwa kwenye usafiri wa treni toka Ubungo maziwa kuja stesheni kuwa asubuhi ya leo kuna mtu sijui ni kutokana na kilevi, alikuwa kalala relini maeneo ya tabata, treni lilimpigia honi lakini hakusikia na hakukuwa na mtu wa kumuondoa relini so treni limempitia na kumkata mguu, hali hii inatisha yapaswa watu wajifunze kuepuka maeneo ya reli maana kwa spidi hii wataondoka wengi na wengine kupata vilema vya kudumu.
 
hivi treni huwa halina breki hadi ionekane kuwa mtu anaigonga. Huu ni upendeleo wa hali ya juu huwezi kusema eti treni linagongwa
 
Watu walikuwa wameishasaha kama ile ni njia wa treni, sasa inabidi wakumbushwe kwa vitendo kama hivyyo.
 

Hata ile mifereji alongside Morogoro Road especially pale Ubungo Maji, watu walilalamika sana kuwa ile mifereji ifunikwe, lakini Dk. John Pombe Magufuli mbunge wa Chato alitoa solution simple tu, kuwa haitafunikwa mpaka pale madereva wazembe watakapojifunza kushusha kile kimteremko kwa adabu...so the same goes kwa wote ambao hawaheshimu njia ya treni
 
Hi sheria ya mtu kugonga garimoshi is wrong

Tubadirishe huu utaratibu wengi watagonga hili garimoshi.

leo mlevi kesho atakua mtoto wa shule au mtu yeyote yule.

Tuachane na hii 4- 4 -2 haitupeleki kokote watanzania

Serikali au mmiliki wa garimoshi lazima alipe fidia kwa madhara yoyote yale

Once is a mistake,twice is a choice
 
mlevi wa watu ameshazoea kulala pale relini.. Hamadi treni limeanza kazi inabidi wafanye matangazo hadi kwenye vilabu vya pombe ili wajue.. Hawa walevi bila shaka wapo mbali na media
 

Ndio mfumo treni huo mkuu! Huyo aliyeigonga kapata kilema tu au umauti umemfika?
 
Huyo lazima aache pombe

Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
 
Enzi zetu ilikua kinapita kwanza kiberenge ndo treni baadae
 
hivi treni huwa halina breki hadi ionekane kuwa mtu anaigonga. Huu ni upendeleo wa hali ya juu huwezi kusema eti treni linagongwa
Sijui ni nani aliyeanzisha hii kitu 'mtu kaiginga treni'
Hivi kwanini treni kama yenyewe inaonewa tu isingejengewa uzio?
 
Breki za treni sio kama gari lazima uzianzie mbali sana, hata gari papo kwa papo ni vigumu. Wananchi tuwe makini tu.
hivi treni huwa halina breki hadi ionekane kuwa mtu anaigonga. Huu ni upendeleo wa hali ya juu huwezi kusema eti treni linagongwa
 
Dereva wa treni alimuona huyo mtu ndio maana alipiga honi. Sasa kwa nini kama alimuona asingepitisha treni pembeni kidogo ya reli kumkwepa jamaa? :becky:
 
Dereva wa treni alimuona huyo mtu ndio maana alipiga honi. Sasa kwa nini kama alimuona asingepitisha treni pembeni kidogo ya reli kumkwepa jamaa? :becky:

😀

Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…