Mtoto wangu nimpeleke chuo kipi??

pet geo pet

JF-Expert Member
Jun 30, 2018
461
644
Wakuu habarini za usiku huu!

Leo Baraza la mitian limetangaza matokeo ya kidato cha nne miongoni mwao alikuwepo binti yangu alihetimu mwaka jana..ivyo amepata matokeo yafatutayo:

26
IV
CIV - 'C' HIST - 'D' GEO - 'C' KISW - 'C' ENGL - 'D' CHEM - 'D' BIO - 'F' B/MATH
Nimejaribu kuongea na walimu wakasema mwanao amejitaidi sana kwa hayo matokeo ...ila mimi nilitaka arudie darasa tu lakin walimu wamenishauri nimpeleke chuo akasome tu..

Kwahiyo wakuu naombeni mnishauri nimpeleke chuo gani kwa hayo matokeo.
 
Yeye ndio atakayesoma kokote utakakompeleka sio Sisi wala wewe.

Kabla ya yote muulize muulize yeye anapenda nini
 
Mbona anaweza kusoma advance kwa comb ya HKL au HGL sifa anazo lakini shule za private, unajua nyie wazazi hamna utamaduni wa kusomesha wstoto private zenye ada ya 1.5m. CCM alisha wapumbaza.
 
Noma sana kama Ada ipo mpeleke chuo tu , TIA , IFM , CBE (diploma) ila awe makini na shule tu , kwa upande wa kozi mtajadili.
 
Mkuu ungetupa Mwongozo Ili tujue tunakushauri vipi Yani ungetuambia kipaumbele mtoto anataka kusomea nini au fani/faculty gani vyuo ni vingi ukisema tu chuo gani hapo Kila chuo kinamfaa mbona ni Hela yako tu
 
Kwa ufaulu huo kwa nn asiendelee na kidato cha sita kwa mfumo wa kujitegemea!? mana naona ana sifa zote za kuendelea na masomo kama private candidate kwa mwaka mmoja tu, ambapo mwaka kesho anafanya mtihan wa taifa vizuri kabisa! kama utaona hili wazo ni zuri naomba tuwasiliane 0679168264
 
Kwa ufaulu huo kwa nn asiendelee na kidato cha sita kwa mfumo wa kujitegemea!? mana naona ana sifa zote za kuendelea na masomo kama private candidate kwa mwaka mmoja tu, ambapo mwaka kesho anafanya mtihan wa taifa vizuri kabisa! kama utaona hili wazo ni zuri naomba tuwasiliane 0679168264
 
Muulize yeye anapenda kusomea kitu ngani
Vyuo kama IFM, CBE, TIA, AIA, MIPANGO, DIT ana anzia cheti mpaka diploma alafu akipenda Anaweza uganisha Degree
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom