Wangeniomba ushauri ningewaambia huu si wakati wa kuingia katika siasa kwa umri wao kwasababu hawatanufaika zaidi ya majina yao kutumika kisiasa kuvutia wengine. Kwani si lazima niwe mwanachama wa chadema,ccm au cuf hasa ukizingatia siasa zao za kuchafuana majukwaani, mwanasiasa anataja mabaya ya kingine mara 24 halafu mazuri ya chama chake kataja mara mbili sasa hapo siasa yenye mtizamo wa kitaifa iko wapi?
Kwahiyo ni vema ukabakia kuwa mpiga kura usiye na upande kwa sasa ili utendee haki nafsi yako na niwe huru na kura yangu moja mwaka 2015.
Huu ni msimamo wangu binafsi, unaweza kunikosoa hasa ukiwa mshabiki wa siasa za watu binafsi.