Mtoto wa shetani

Mtoto wa shetani

Joined
Oct 10, 2017
Posts
11
Reaction score
6
Soma stori hii ni nzuri.
Mnamo mwaka 1996 katika nchi ya Tanzania, mkoani Singida sehem ya kijijini ambapo kijiji hicho kilizungukwa na msitu,, kati ya hao wanakijiji kulikuwa na binti wakike ambae binti huyo aitwae Lagingi,, alikuwa hataki kuolewa wazi umri wake ulifaa kuwa na mume, wazazi wake walimsihi mwanao aolewe na kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Mapogwa lakini juhudi za wazazi wa Lagingi hazikufanikiwa kumshawishi Lagingi kumkubali kijana Mapogwa.

Mama yake binti huyo alimuhoji kwanini hataki kuolewa wakati rafikizake wote wamekwisha kuolewa, lakini Lagingi hakuwa akitoa sababu za msingi juu ya msimamo wake,,siku moja nyakati za jioni Lagingi alizipiga hatua akaelekea mstuni kuokota kuni za kupikia, wakati akiendelea kutafuta kuni huku na kule ghafla akaonekana Nyoka mweusi mkubwa,,kwa upande wa nyuma yake.

Nyoka huyo alijiburuza taratibu akimfuata binti Lagingi,, Lagingi hakujua chochote zaidi aliendelea kuokota kuni kunako majani marefu makavu,, ghafla Lagingi alihisi kachomwa na mwiba kunako mguu wake haraka! alitazama mguu wake akashtuka kuona nyoka kubwa ikitokomea kwenye majani, huku akihisi maumivu makali kwenye mguu wake,, alijaribu kupiga hatua lakini ikashindikana akahisi maumivu makali kupita kiasi,, akapiga yowee ghafla akaishiwa nguvu akapoteza fahamu

Upande mwingine alionekana kijana wa ajabu ambae macho yake yalifanana na macho ya ndege bundi kijana huyo aliekuwa akikatiza huko na huku mara ghafla alimuona Lagingi akiwa amelala kwenye majani makavu amezilai, huyo kijana aliachia tabasam pana kisha akazipiga hatua kumfuata, kijana huyo asie tambulika alichuchuma chini, , nakuanza kumkagua Lagingi, huyo kijana akagundua kuwa Lagingi kaumwa na nyoka,,kijana huyo akatazama angani kisha akatamka maneno magumu ya kilugha.

Ghafla ukaonekana moshi mweusi ukitoka kwenye jeraha la kuumwa na nyoka kwenye mguu wa Lagingi,,baada ya dakika kadhaa Lagingi akapata fahamu alipotazama kwambele yake alimuona Kijana akitokomea kusikojulikana,, Lagingi akaigiwa na hofu kuona giza limetanda angani haraka alinyenyuka nakuanza kuludi kijijini kwao,, lakini akawa anajihoji maswali mengi kwani alijikuta akipoteza kumbukumbu kichwani ''mmh mbona sikumbuki kitu nifanyaje" ''khhaaah kama nahisi niligogwa na nyoka?'' eeh kwelii embu nitazame mguu wangu mmh lakini mbona sina alama yeyote wa maumivu""" Lagingi aliendelea kujihoji na kujijibu mwenyewe,,alipofika karibu na kwao alistajaabu kuona watu wakiwa umati mkubwa kwao huku wengine wakipaza sauti za vilio

Naam "kunanini nyumbani?" alijihoji Binti Lagingi huku hofu ikimuingia akazipiga hatua za haraka haraka akiifuata nyumba yao ghafla na yeye akaanza kuhisi maumivu kwenye mguu wake,, akastajaabu kuhisi mguu wake ukimuuma wakati alipozinduka hakuhisi maumivu yoyote, akamua kupinguza mwendo lakini maumivu ya mzidia hatimae macho yake yakapoteza uwezo wa kuona vizuri ghafla akahishiwa nguvu akapoteza faham kwa mara ya pili wakati huo huo alioneka kijana yule wa ajabu akiwa kakamatia kisu mkononi,, sambamba na kibuyu huku akimfuata Lagingi,.......
ITAENDELEA
 
Situmii kipawa hiki kuandika hadithi za dunia kwanzia leo, kipawa nitakitumia kwaajiri ya utukufu wa Mungu(Yesu Kristo) hivyo naomba msamaha kwa wote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom