Mtoto wa Rais kizimbani kwa ufisadi

Mtoto wa Rais kizimbani kwa ufisadi

COARTEM

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
3,622
Reaction score
3,696
Kesi ya ufisadi dhidi ya Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade imeanza kusikilizwa huko Dakar Senegal.

Hata hivyo kesi hiyo inaanza kusikilizwa mshitakiwa akiwa kizuizini katika gereza kuu la Dakar, Rebeuss kwa mwaka mmoja sasa.

Waziri huyo wa zamani atatakiwa kuieleza mahakama vyanzo vya utajiri wake wa Uero milioni 178.

Hata hivyo kiwango hicho cha fedha kinadaiwa kuwa kidogo ikilinganishwa na kile kilichosababisha kukamatwa kwake ambacho ni Euro bilioni moja.

Seydou Diagne, mmoja wa wanasheria wa Karim Wade, amelalamikia mashitaka hayo na kuyaita ya kisiasa akidai kuwa kitu pekee kinachowasukuma wanao mshitaki mteja wake.

Wanasheria wake pia wamedai hata hiyo mahakama itakayotumika kuchunguza matumizi mabaya ya ofisi haina uwezo wa kuisimamia kesi hiyo.

Hii ni moja ya kesi za kuwatafuta vigogo waliozitumia vibaya ofisi zao wakati wa utawala wa Rais Abdoulaye Wade.

SOURCE: BBC Swahili
 
140730172139_karim_wade_304x171_afp_nocredit.jpg

Karim Wade

Chanzo: BBC
 
Nilifikiri mtoto wa rais wetu. Nikajiuliza si tumefuta vipengele vya uadilifu na uwajibikaji kwenye tunu za Taifa na UKAWA hawajarudi kuvirudisha?
 
Nilifikiri wanataka kumtuhumu Makongoro na nduguze wenye kutupiga Vizinga kila kukicha!!! Kimti, Hussein, Riziwan, Aman et al wako vizuri kwenye ujasiriamali lakini wa Babab wa Taifa ...Mwee?!!!
 
Nilijua ni Rizmoko nilitaka kushangaa miujiza hii kama mtu baki hakamatwi kwa ufisadi itakuwa mtoto wa prezdaa!
 
Hii ni message nzuri sana kwa riziwani kikwete.
Maisha huwa yanabadilika
 
Kwa kweli huo ni mwanzo mzuri sana kwa bara letu la afrika hasa kwa viongozi wa kiafrika ambao wao RUSHWA sio tatizo na hawajishughulishi nayo kabisa.Mtu ghafla tu anakuwa tajiri hatari bila kujulikana ana biashara ipi iliyompaisha kimaisha hivyo.Walioendelea huhoji hicho kitu,huku kwetu sisi MASIKINI wa kutupwa ukihoji unaambiwa una wivu na hata ungelikuwa wewe ungelifanya hivyo kama hao unaowatuhumu.Yaani tunajustify wizi/ufisadi kipuuzi kabisa halafu hapo hapo unataka nchi iendelee,tuwe na barabara nzuri,hospitali zinazotoa huduma stahiki kwa wagonjwa wetu, mashule bora yatoayo elimu bora, na mbaya zaidi hii hali imewaingia hata wananchi wetu hasa pale tu aliyekuwa kiongozi anapoondoka madarakani asipokuwa na kitu,wanajamii humdhihaki eti kachezea maisha ndio maana hana MALI,tutaweza kweli kufika popote tusipokemea tabia hizi na za viongozi wetu kujilimbikizia mali pasipo kuangalia ustawi wa wananchi wao,kwa kweli Afrika bado tuna safari ndefu sana na ndio maana tunadharaulika sana kwa kushindwa kwetu kusimamia mambo ya msingi kabisa
 
Nilifikiri wanataka kumtuhumu Makongoro na nduguze wenye kutupiga Vizinga kila kukicha!!! Kimti, Hussein, Riziwan, Aman et al wako vizuri kwenye ujasiriamali lakini wa Babab wa Taifa ...Mwee?!!!

Hata Karim Wade nazani alijiona mjasirimali. Baada ya kuona yaliyomtokea Gaddafi na watotowake. Hakuna nitakacho shangaa tena dunia ya leo.
 
Yaliyowapata Ghadaffi na Watoto wake ni Muendelezo wa Dhulma na Aggressions za Western Power kwa Wanaadamu! Enzi za Ghadaffi Libya ilikuwa na Surplus ilikuwa inasaidia nchi nyingi duniani, wananchi walikuwa wanapatiwa kila kitu na serikali yao: Leo hii wamarekani wameigeuza nchi ya vita ya kutwangana wenyewe kwa wenyewe na sasa wanaikimbia ... SAME kwa Saddam Hussein, muda si mrefu Asad na watamua kama kawaida yao... Tukubaliane kimsingi kuwa Mitego ya kuwawekea hizo fedha kwenye a/c za Uswis hufanywa na hao hao ambao mwisho wa siku huwazunguka na kuwafungulia mashtaka baada ya kuwatumia na mwisho wa siku wanaingia tena deal na watakao kuwa madarakani ... Wajinga ndio waliwao...
Hata Karim Wade nazani alijiona mjasirimali. Baada ya kuona yaliyomtokea Gaddafi na watotowake. Hakuna nitakacho shangaa tena dunia ya leo.
 
Back
Top Bottom