Mtoto wa Osama bin Laden Akataliwa Kuoa Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Osama bin Laden Akataliwa Kuoa Uingereza

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Dec 5, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Omar Bin Laden, mtoto wa kiongozi wa kundi la Al Qaeda, Osama Bin Laden Friday, December 04, 2009 5:23 AM
  Mtoto wa kiume wa Osama bin Laden mwenye umri wa miaka 28 amenyimwa viza ya kuingia Uingereza kumuoa mchumba wake mwanamke wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 54. Omar Bin Laden, mtoto wa kiongozi wa kundi la Al Qaeda, Osama Bin Laden anayetafutwa na Marekani kwa udi na uvumba, amenyimwa viza ya kuingia Uingereza kumuoa mchumba wake mwanamke mzaliwa wa Uingereza ambaye ana umri karibia mara mbili ya umri wake.

  Omar Bin Laden alikata rufaa hukumu iliyotolewa mwaka jana ya kumnyima viza ya kuingia Uingereza kumuoa Jane Felix-Brown ambaye alisilimu na kupewa jina la Zaina.

  Baba yake Omar, Osama Bin Laden ndiye anayetuhumiwa kuhusika na mashambulizi ya septemba 11 nchini Marekani ambayo yaliua mamia ya watu na mashambulizi katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 ambapo zaidi ya watu 200 walifariki.

  Omar alifunga ndoa na Jane mwaka 2006 nchini Misri lakini ndoa yake ilikuwa haitambuliki kwa mujibu wa sheria za Uingereza kwakuwa Jane alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine nchini Uingereza wakati huo na Omar alikuwa ana mke na mtoto nchini Saudia Arabia.

  Kabla ya ndoa yao, Omar alikuwa ameoa na kuwaacha wanawake watano wakati Jane naye alikuwa ameolewa na kuachika mara nne.

  Wakati wanafunga harusi yao nchini Misri, Jane alikuwa ndio yupo kwenye taratibu za kuachana na mume wake wa tano Andrew Yeomans.

  Ingawa mahakama iliambiwa kuwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu Jane alikuwa akihesabika ameachana na mumewe Bw. Yeomans lakini kwa sheria za Uingereza kuvunjika kwa ndoa yao kulitakiwa kuidhinishwa na mahakama. Hatimaye taratibu za mahakama kuivunja ndoa hiyo zilikamilika februari 2007.

  Mwezi wa nne mwaka jana, Omar ambaye alidai hajawahi kumuona baba yake tangia mwaka 2000, alinyimwa viza ya kuingia Uingereza kwakuwa ndoa za kiislamu hazitambuliki kisheria nchini Uingereza.

  Omar alikata rufaa na kuomba viza ya Uchumba ili amuoe mchumba wake kwa mujibu wa sheria za Uingereza ndani ya Uingereza lakini alinyimwa pia viza hiyo.

  Omar aliambiwa kuwa baba yake jina lake kamili ni Osama Mohammed Awad bin Laden, ndiye anayetuhumiwa kuhusika na matukio mengi ya kigaidi duniani hivyo kuwepo kwake nchini Uingereza kutahatarisha amani.

  Omar alikata rufaa tena akisema kuwa haki zake za kibinadamu zimevunjwa kwa kukataliwa kufunga ndoa na mchumba wake.

  Hukumu iliyotolewa jana alhamisi ilizidi kumnyong'onyesha Omar na mpenzi wake kwani mahakama iliendelea kusisitiza kumnyima viza Omar ya kuingia Uingereza, ikisema kuwa mahakama haina uhakika kama kweli wapenzi hao wana nia ya kufunga ndoa ya kweli na kuishi pamoja.

  Pia mahakama ilisema kuwa suala la baba yake Omar, Osama bin Laden kuwa gaidi anayetafutwa duniani limechangia yeye kunyimwa viza.

  Akizungumzia hukumu hiyo Jane alisema "Nina wajukuu lakini niko tayari nikae nao mbali ilimradi niwe karibu na Omar".

  Omar ni mtoto wa nne kati ya watoto 11 wa Osama bin Laden aliozaa na mke wake wa kwanza. Osama bin Laden inasemekana ana jumla ya watoto 19.
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  siasa za wenzetu nazo mmh!
   
 3. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mH! Kwani makosa ya baba yake ayahesabiwe yeye???
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  The politics of this issue aside there is one thing I've noticed. Normally when one asks for a visa you specify a specific reason for entry. In his case he probably stated marriage. Now if islamic marriages are not recognized there it means you reason to request entry is invalid. So in that perspective I can see their case. But the fact that they stated that his father is one of the reasons he was denied a visa shows that this whole thing has been politicized some what.
   
 5. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Bwana we, Nataka nikiwa London nisiwe na wasiwasi wa kupigwa Bomu, , hata kama makosa sio yake ni ya baba yake still siko comfortable kwa huyu dogo kuwa mji mmoja na mimi, ina wezekana ana akili za baba yake vile vile .
  Sometimes hizi haki nazo zina tulostisha vile vile , inabidi watu kama hawa wasipewe haki kama wengine labda itasaidia, (sorry guys naogopa kupigwa bomu)
  Na kwanini ang'ang'anie UK si aende kumuoa huko Saudia , Kuna Dubai, Kuna Maskat , kuna Iran , kuna sehemu kibao ambazo weza karibishwa kwa moyo mkunjufu , kwani yeye lazima UK imtambie ? si wana hela bwana !
   
 6. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hey! Osama si alisha fariki dunia? au sio kweli? Ila huyu dogo nadhani angeenda kufunga ndoa yake huko Pakistani!
   
 7. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Omar bin Laden

  Bin Laden's son wants to join the UN to promote peace

  London, Nov 19 : The son Osama bin Laden favoured to carry on his work says he would like to work for the United Nations instead -- as a peace campaigner.

  In a magazine interview published Thursday following launch of a book about him, Omar bin Laden - the fourth eldest son of the Al Qaeda leader.

  [​IMG]

  [​IMG]

  Omar Bin Laden, the 26-year-old son of al Qaeda leader Osama Bin Laden, poses with his wife Jane Felix-Browne (Islamic name Zaina Mohammad) before the broadcast 'Niente di Personale' on Italian television channel 'La Sette', on February 4, 2008 in Rome, Italy. Omar Bin Laden has expressed an interest in being an 'ambassador for peace' between Islam and the West.

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 8. D

  Darwin JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Afadhali amekataliwa,
  Asingeingia kwa amani UK.
  Mbali ya hayo huyo mtoto ni photocopy ya baba yake, watu wangeweza kumuua wakimuona mitaani.

  Omar bin Laden mchukue mke wako uishi naye huko unakoishi
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Basi zuia kabisa usife..ndugu...maana kama mtoto wa osama ameshanyimwa viza..hakutakuwa na mabomu tena...na wewe hutakufa..
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mizungu siku zote ni mijitu mijinga tu. Angekuwa mtoto Hitler wangemnyima viza?

  Omar ndoa omba ndoa yako itambulike na kukubalika kwa Mola na sio wanadamu.
   
 11. D

  Darwin JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  1.Hitler inasemekana alikua gay or maybe bisexual hakupata watoto, ndio maana aliwaua gays wenzake kwa kutojijua mwenyewe vizuri.


  2.Post yako imekua yakiudeen deen.
  Uk wanajua wanachokifanya hasa kuzuia ghasia zitakazojitokeza kwenye nchi yao kama akikubaliwa visa.

  Yuko mwanasiasa hapa Netherlands jina lake Geert Wilders alikataliwa visa yakuingia UK kwakile kinachoitwa kuzuia ghasia zitakazotokea UK kama akikubaliwa.

  soma zaidi kuhusu Geert Wilders hapa kwenye link chini.

  http://en.wikipedia.org/wiki/Fitna_(film)

  Fitna ([ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Arabic_language"]Arabic[/ame]: فِتْنَةٌ‎) is a 2008 [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Short_subject"]short film[/ame] by [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Netherlands"]Dutch[/ame] [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/House_of_Representatives_of_the_Netherlands"]parliamentarian[/ame] [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Geert_Wilders"]Geert Wilders[/ame]. Approximately 17 minutes in length, the film shows selected excerpts from [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Sura"]Suras[/ame] of the Qur'an, interspersed with media clips and newspaper cuttings showing or describing acts of violence and/or hatred by [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Muslim"]Muslims[/ame]. The film is intended to demonstrate that the Qur'an motivates its followers to hate all who violate [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Islam"]Islamic[/ame] teachings. Consequently, the film argues, Islam encourages, among other things, acts of [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Terrorism"]terrorism[/ame], [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Antisemitism"]antisemitism[/ame], [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Violence_against_women"]violence against women[/ame] and [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Homosexuals"]homosexuals[/ame], and Islamic [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Universalism"]universalism[/ame]. A large part of the film deals with [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Islam_in_the_Netherlands"]the influence of Islam on the Netherlands[/ame].
  The Arabic title-word "fitna" means "disagreement and division among people" or a "test of faith in times of trial".[1] Wilders, a prominent critic of Islam, described the film as "a call to shake off the creeping tyranny of [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Islamization"]Islamization[/ame]".[2]
  On March 27, 2008, Fitna was released to the Internet on the [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Video_hosting_service"]video sharing website[/ame] [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Liveleak"]Liveleak[/ame] in [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Dutch_language"]Dutch[/ame] and [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/English_language"]English[/ame] versions. The following day, Liveleak removed the film from their servers, citing serious threats to their staff. On March 30, Fitna was restored on Liveleak following a security upgrade, only to be removed again shortly afterwards by Wilders himself because of copyright violations. A second edition was released later.

  Now you will understand why UK didnt want Osama┬┤s son and Geert Wilders to get in their soil.
   
 12. M

  Makanyagio Senior Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Huyo dogo ni mzushi tu ana nie nyingine kabisa. Aitie timu kabisa uku UK atatuharibia mabombo yetu ya maana. Kuna usemi wa kiswahili unasema 'Mtoto wa nyoka ni Nyoka' hata uku UK unamaana sana. Hiyo VIZA hata mimi ningezua.
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sababu mbili kuu:
  1. Mtoto wa nyoka ni nyoka na hafundishwi kuuma. Kwani mmesahau jinsi Osama bin Laden anavyoua kila Mmarekani na raia wa Magharibi anayemwona machoni pake haka kama hana hatia?
  2. Damu ni nzito kuliko maji. Uwezekano wa Osama bin Laden kumtumia mtoto wake ili kulipiza kisasi dhidi ya adui zake ni mkubwa kuliko kutumia mtu mwingine yeyote.
  Hongereni Waingereza kwa kumzuia mtoto wa Osama bin Laden kufanya infiltration ndani ya nchi yenu!
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Acha kuvaa miwani ya mbao, Waingereza hawajasahau London bombing na milipuko mingineyo ambayo imesababishwa na magaidi ya Kiislamu kama akina Osama na washirika wake. Hayo masuala ya akina Hitler ni historia ndugu yangu lakini ya magaidi yanaoperate in 24 hours! Ukicheza na magaidi ya kiislamu ndugu yangu umeliwa, utakuta mwana si wako!
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Lanatu Lllah yeyote lazima ahusishe dini anayoichukia na mambo binafsi yanayofanywa na waumini wa dini hiyo. Nani kakuambia uislamu unafagilia kuua mtu asiye na hatia?, go back to school Lanatu Lllah
   
 16. October

  October JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Nyoka katumwa na baba yake kuingie Uingereza ili wapate nafasi ya kuwapiga waingereza.
  Bravo Uingereza msiruhusu huyu nyoka kuja nchini kwenu, Kama anashida ya kuoa si aende Afghanistani au Saudi Arabia akaoe huko?

  Halafu hii dhana ya kuoa vibibi vizee kaitoa wapi huyu kijana mdogo? Ahhh Nshakumbuka, Kuna mhishimiwa mmoja alioa kibibi kizee, na kitoto cha miaka tisa, Kumbe huyu kijana anafuatilia mafundisho ya mhishimiwa kwa vitendo.

  Baada ya muda baada ya kulipua London tutasikia anaoa katoto ka miaka 9 kujip ongeza.
   
Loading...