Mtoto wa ndani ya ndoa lakini si wako...

Mtoto wa ndani ya ndoa lakini si wako...

Truth Matters

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
2,633
Reaction score
5,615
Wakuu,
Napenda kujua mtizamo wa kisheria, mila na dini. Ikiwa imethibitika mtoto si wa baba (baada ya kupima DNA) lakini alizaliwa ndani ya ndoa halali ya huyo baba. Je haki zake ni zipi?
  1. Anaweza kurithi mali za 'baba' mlezi?
  2. Atatumia ubini wa 'baba' mlezi?
  3. Ana haki kwa 'real' biological father wake?
 
Kitanda hakizai haramu ndugu, hlf binadamu tulivyo - anaweza akaja kuwa msaada na baraka kuzidi hata hao unaoona ni biological father
 
Hayo mambo yenu ya DNA naona yanapeleka Dunia kwa Kasi ya ajabu sana.
Siku zile tulisema kitata hakizai haram, as long amezaliwa na mke wako kwa msaada wa kiuno chako, basi huyo ni mwanao wa halali.
Kumbuka ikiwa huyo kijana atagundua hayo ulio yagundua, basi pengine unaweza ukawa umem-bomoa kisaikolojia na kumuharibia maisha yake.
Na kumbuka kwamba hapa naona kama unaumizwa na mali ambazo wewe ulitamani umrithishe, labda nikukumbushe tena kwamba Mali si kitu if you talk about Dignity.
 
Hahaha ndoa haikua halali ndio maana mmpata mtoto wa nje ya ndoa ndani ya ndoa..kimsingi harithi mali kwa baadhi ya dini lakin hurith kama utamuandikia arthi kabla ya kufa..tuwasubir ma ustadh na wachungaji kwa majib mubashara zaidi
 
Kabla hujawaza mbali fikiria juu ya athari zitakazo mpata mtoto huyo kisha jiweke kwenye nafasi yake wewe kama ungekuwa ndiyo mtoto huyo ungejisikiaje. Hana hatia lakini hukumu anayoipata toka kwa wazazi na jamii ni fedheha kubwa sana inayogharimu maisha yake. Kama mtoto ameshazaliwa ndani ya ndoa achana na mambo ya DNA, Linda heshima yako lakini pia Linda afya ya moyo wako maana kwa kujua majibu hayo hutapata amani maishani mwako.
 
Muachie Mungu tu...makosa sio ya mtoto ww mlee tu kama bado unaendelea kuishi na huyo mama kama hamuishi pamoja baba yake atamlea
 
Sahau dini!

Sahau sheria!

Na-assume wewe ndie Baba Mlezi mwenyewe!

SWALI: Je, nani ali-initiate hiyo DNA test? Ni wewe au biological father wa huyo mtoto?

Kama uli-initiate wewe; baada ya ku-confirm huyo mtoto si wako! Hivi sasa unamchukuliaje?! Still like your own kid (though nitahoji ni kwanini basi ulienda kwenye DNA!) au unamchukulia si wako huku akikutia hasira ile mbaya?!

Kama unamchukulia ni wako; basi mwachie hizo privilege!!

Lakini kv ulishafukua makaburi; it's possible now atamfahamu baba yake mzazi... iwe leo au kesho but why should you care?! Hata kama c mwanao bado ni kaka/dada wa "Wanao!
 
Muachie Mungu tu...makosa sio ya mtoto ww mlee tu kama bado unaendelea kuishi na huyo mama kama hamuishi pamoja baba yake atamlea
Sasa anaweza kuendelea kulea alafu bhuku baba wa mtoto anajua kuna mtoto wake mahala
 
Sasa utaishi na mkeo halaf useme mtt sio wako si jamii itakushangaa
inaweza kuwa jamii wanajua sema tu hawataki kuingilia ndoa za watu.
mpaka mtu anazaa nje ya ndoa unadhani watu hawajui?
 
Hayo mambo yenu ya DNA naona yanapeleka Dunia kwa Kasi ya ajabu sana.
Siku zile tulisema kitata hakizai haram, as long amezaliwa na mke wako kwa msaada wa kiuno chako, basi huyo ni mwanao wa halali.
Kumbuka ikiwa huyo kijana atagundua hayo ulio yagundua, basi pengine unaweza ukawa umem-bomoa kisaikolojia na kumuharibia maisha yake.
Na kumbuka kwamba hapa naona kama unaumizwa na mali ambazo wewe ulitamani umrithishe, labda nikukumbushe tena kwamba Mali si kitu if you talk about Dignity.
Wewe kweli ni MWANAUME
 
kama ulishaamua kupima DNA, na ukweli ushaujua.....ni busara yako tuu..ila dogo atachanganyikiwa sana......muonee huruma..
 
Back
Top Bottom