mtoto wa miezi nane na nusu hataki kula | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mtoto wa miezi nane na nusu hataki kula

Discussion in 'JF Doctor' started by Iyokopokomayoko, Dec 30, 2011.

 1. Iyokopokomayoko

  Iyokopokomayoko JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,808
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mwanangu wa kike ana miezi nane na nusu, tatizo lake kubwa ni kuwa hataki kula kabisa, inaweza kupita hata siku 2 kila tukimpa uji au chakula kingine analia sana kiasi tunaamua kumwacha lakini maziwa ya mama yake ananyonya bila matatizo. Naombeni ushauri wenu madaktari na wengine kwa uzoefu wenu tufanye nini kumuongezea apetite mtoto wetu. tunashukuru kwa ushauri wenumtakaotupatia
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapendi vyakula mnavyompa. Maana tatizo lingekua mtoto hata maziwa ya mama yake angesusa.

  Jaribuni recipe tofauti, muone itakuwaje.
  Mnaweza mkajaribu kumpondea viazi, uji wa mchele, au hata mkapunguza vikorombwezo kwenye hivyo mnavyompa sasa hivi.

  Watoto nao ni wajanja, binafsi nimeshapitia.Alikua vya makopo akipewa analia au anatemelea mbali, ila kinachopikwa vizuri nyumbani anakula kwa raha zote.
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  change your menu and recipe, make it funny, muimbie, muweke karibu na tv while eating
   
 4. Iyokopokomayoko

  Iyokopokomayoko JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,808
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Nashukuru mkuu, ila vyakula tunamubadilishia mara nyingi, tunamuandalia wenyewe uji wa lishe, tunampikia na kumsagia ndizi, viazi, karoti na hata juice za matunda kama embe, nanasi nk lakini bado anasumbua kula. Akiwa na miezi 5 hivi ilikuwa ukimpa tuuji alikuwa anazuga anasinzia lakini ukiacha tu kumlisha anafumbua macho na kuanza kucheza, kuna baadhi za siku anaweza akaamua kula mpaka mkashangaa lakini akianza tena kukataa inaweza chukua wiki hataki.

  tangu jana asubuhi ameanza akinyonya au kunywa vijiko 2 au 3 vya uji (kwa kumkaba), akimaliza anatapika, pia leo anaharisha kama maji hivi, bado anachezacheza lakini nachanganyikiwa nini nifanye kum-speed-up apetite yake, tafadhali wakuu tusaidiane
   
 5. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  soseji nayo kakataa? basi nenda mkamuone doctor. inawezekana ana homa. Poleni sana Mkuu. watoto wadogo wanasumbua sana, mtoto unakuta analia wala haemi analilia nini. Mungu awasaidie. Mia
   
 6. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  jaribu kumwekea pilipili kwenye uji na umpe ugali wa dona mboga matembele alafu uone kama atalia,akilia mpige makwenzi kwenye utosi
   
 7. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Jitahidini kumpa mara kwa mara hata kama atakula vijiko viwili itatosha. Kamwe msimlazimishe, kwani inaweza ikasababisha atapike. Na zaidi ya hapo mjaribu kumbadilishia vyakula tofauti tofauti. Siyo vibaya hata wkt mama anakula naye kumwonjesha hata kidogo. Pia jitahidi anapopewa chakula mama asiwepo karibu ili aweze kula. Changamoto ni kwamba kuna uwezekano atakuja kula zaidi kipindi akiachishwa.
  tahadhari: kamwe usijaribu kumpa mtoto wako dawa za kumpa hamu ya kula; nyingi kati ya hizo dawa zimeleta madhara ya kiakili kwa watoto baadaye. Hivyo, ni bora kuendelea naye hivyo hivyo na kunyonya maziwa ya mama kuliko kumpa dawa hizo.
   
 8. Mhindih

  Mhindih JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Yani miezi 5 tayar mmeanza kumpa mtoto vyakula? Na si ajabu mlianza muda mrefu. Mamake ana matatizo gani na matenite leave maanake nini? Ana haki ya kukataa vyakula muda wake bado.
   
 9. Iyokopokomayoko

  Iyokopokomayoko JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,808
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ubarikiwe mkuu, ukipata wazo jingine usisite kunijulisha, kwa hakika naogopa sana kumzoesha mwanangu madawa ya hospitali.
   
 10. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,978
  Likes Received: 6,621
  Trophy Points: 280
  vipi hata supu ya pweza kagoma? Mwambie mama ake amnyonyshe bana. acheni mchezo. kama vipi kamuoneni doctor. Mia
   
 11. Iyokopokomayoko

  Iyokopokomayoko JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,808
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mkuu hapo miezi 5 tulikuwa ndo tunamtest kumpa japo vijiko 2 kwani tulikuwa tunajuwa atakapofikisha miezi ndo tungeanza rasmi kumpa chakula, nashukuru hata hivyo kwa ushauri wako.
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Du mtoto wa miaka 8?
   
 13. Iyokopokomayoko

  Iyokopokomayoko JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,808
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  usinikumbushe pweza mkuu, nimemiss supu yake usiseme, kuna dr mmoja nimeambiwa yupo k/koo mzuri sana kwa watoto, nacheki cku mbili tatu nitampeleka akamchunguze
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kitendo cha yeye kutapika baada ya kumlazimisha kula ni dhahiri kwamba tatizo lipo kwenye chakula.Yani hapendi, inawezekana ni namna mnayotengeneza. Jaribuni kumtengenezea chakula ambacho hata nyie mkionjeshwa hamtokunja nyuso. Make it fun. . . . pia ni vizuri ikifika muda wa kula mkawa mnaanza na chakula kabla ya maziwa ya mama yake maana inawezekana hua mnachanganya sana kwahiyo anapokua ameshaonja maziwa (matamu kwake) alafu mkampa chakula ambacho pengine hakina ladha anagundua tofauti right away.Na pia matunda jaribuni moja moja, hawezi kupenda yote kwahiyo jaribuni moja moja mpaka mtakapopata lile atakalokua anafurahia.
   
Loading...