Mtoto wa miaka miwili amuokoa mama yake

Mtoto wa miaka miwili amuokoa mama yake

Usiku

Senior Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
174
Reaction score
47
140401084742_mama_mtoto_london_512x288_bbc_nocredit.jpg



Mtoto mwenye umri wa miaka miwili nchini Uingereza Riley Ward amepokea sifa kedekede kwa kuokoa maisha ya mamake kwa kupiga nambari ya simu 999 baada ya mamake kuzimia.

Wahudumu wa afya katika kituo cha kupokea simu za dharura nchini Uingereza walisema kuwa walipokea simu ya mtoto mdogo aliyewambia ''Mama amelala''. Wahudumu hao walifanikiwa kwenda nyumbani kwa mtoto huyo katika mtaa Leicestershire, na kumpa huduma ya kwanza mamake mtoto huyo na kisha kumpeleka hospitalini.

Walimfanyia upasuaji wa dharura baada ya kupatikana na damu iliyokuwa imeganda kichwani huku akivuja damu nyingine kutoka katika kizazi chake. Sasa mtoto huyo Riley Ward amezawadiwa kwa kitendo chake cha ujasiri na wahudumu hao waliosema kuwa huyo ndiye mtoto mchanga kabisa kuwahi kupiga simu kituoni humo. Mamake , Dana Henry, alimtaja mwanawe kama shujaa wake mdogo.

Dana mwenye umri wa miaka 27 alisema kuwa alishtushwa sana na kitendo cha mtoto wake aliyekuwa na uwezo wa kupiga simu. Pia alisema kuwa ameweza kuwafundisha watoto wake wadogo namna ya kupiga simu ya dharura ikiwa yeye na mumewe hawahisi vizuri.

CHANZO: BBC SWAHILI; 1 Aprili 2014: Saa 08:51 GMT!!
 
Lovely son.....Inabidi tuwafundishe watoto yaliyo muhimu na sio kufundisha kutukana

me love dat
 
exactly!!Samaki mkunje angali mbichi!!
 
140401084742_mama_mtoto_london_512x288_bbc_nocredit.jpg



Mtoto mwenye umri wa miaka miwili nchini Uingereza Riley Ward amepokea sifa kedekede kwa kuokoa maisha ya mamake kwa kupiga nambari ya simu 999 baada ya mamake kuzimia.

Wahudumu wa afya katika kituo cha kupokea simu za dharura nchini Uingereza walisema kuwa walipokea simu ya mtoto mdogo aliyewambia ''Mama amelala''. Wahudumu hao walifanikiwa kwenda nyumbani kwa mtoto huyo katika mtaa Leicestershire, na kumpa huduma ya kwanza mamake mtoto huyo na kisha kumpeleka hospitalini.

Walimfanyia upasuaji wa dharura baada ya kupatikana na damu iliyokuwa imeganda kichwani huku akivuja damu nyingine kutoka katika kizazi chake. Sasa mtoto huyo Riley Ward amezawadiwa kwa kitendo chake cha ujasiri na wahudumu hao waliosema kuwa huyo ndiye mtoto mchanga kabisa kuwahi kupiga simu kituoni humo. Mamake , Dana Henry, alimtaja mwanawe kama shujaa wake mdogo.

Dana mwenye umri wa miaka 27 alisema kuwa alishtushwa sana na kitendo cha mtoto wake aliyekuwa na uwezo wa kupiga simu. Pia alisema kuwa ameweza kuwafundisha watoto wake wadogo namna ya kupiga simu ya dharura ikiwa yeye na mumewe hawahisi vizuri.

CHANZO: BBC SWAHILI; 1 Aprili 2014: Saa 08:51 GMT!!
Thefact is, kids are really angels manifesting among us as human beings, ..., and because of this fact, I really like kids from the bottomof my heart! Nawashangaa mno na kuwalaani mno wanaowa-abuse watoto wadogo both physcally and spritually. I always pray that God should istantaneously descend on their shoulders with a ton of concrete,..., and He will, believe me!
 
mhh!!!!!!!! id nyngne balaa, sijui ni me/ke Usiku, chausiku mpo!
 
Last edited by a moderator:
1gb mimi ni mwanaume!!by the way nilijiunga usiku!!
 
kwa siku hii ya wajinga? tutaona na kusikia mengi...

mtoto wa miaka miwili anaitwaje mtoto mchanga???

nipeni mwongozo jamani ndani ya april fools..
 
hongera kwanza KWA huyo mama yake KWA kumfundisha mwanae kupiga cm ya dharura hongera pia KWA mtoto.kubwa kabisa ni KWA watoa huduma kujali name kukimbilia kujua kulikoni.maana MTOTO kasema mama amelala.wangeweza kudharau tu .
 
safi sana sio akina siye tulianza kutumia simu tulivyofika chuo kikuu
 
sio samaki nkunje hadi anye
PROVERBS 1:5-6 from KING JAMES VERSION (5) A wise man will hear, and will increase learning; and a man of understanding shall attain unto wise counsels🙁6)To understand a proverb, and the interpretation; the words of the wise, and their dark sayings.
 
hiyo ni kwa wenzetu wa mbele wanaojali, huku bongo wangesema mtoto anachezea simu then wangekata.
hapa tu mtu mzima unapiga cm ya dharura wanakuja baada ya tukio sembuse wasikie sauti ya katoto.
by the way that kid is a hero.
 
Back
Top Bottom