Mtoto wa miaka 9 ajifungua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa miaka 9 ajifungua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tabutupu, Jan 8, 2011.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  KONA za mji wa Mbeya zimezizima kwa minong'ono baada ya kuibuka kwa taarifa za mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa kujifungua mtoto ambapo inadaiwa kuwa mimba hiyo alipewa na kaka yake mwenye umri wa miaka 18.

  Binti huyo aliyekuwa akiishi na mama yake mkubwa alipewa mimba hiyo na kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa na alipobainika kuwa mjamzito alifungiwa ndani na mama yake huyo ili wananchi wasibaini tukio hilo.

  Mtoto huyo ambaye alikuwa akisoma Shule ya Msingi ya Ndora iliyopo Kijiji cha Salala, Mji Mdogo wa Mbalizi Mbeya, alisema kaka yake alikuwa akimtishia kwa kisu na kumlazimisha kufanya naye ngono, jambo ambalo anadai lilimfanya akubalie naye.

  Anasema alisimamishwa kwenda shule na mama mkubwa huyo baada ya mama yake mzazi kufariki dunia.

  Aliongeza kuwa anamshukukru Mungu kwa kujifungua salama mtoto wa kike, lakini mama yake huyo alishindwa kumpa huduma nzuri, hivyo kupata vidonda sehemu za siri vilivyosababisha kutokwa usaha mara kwa mara.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Pipeline eneo la Mbalizi, Asifiwe Mwakalonge, taarifa hizo alizipata Januari 2, mwaka huu kutoka kwa Mjumbe wa Kitongoji hicho, Kennedy Maniamba.

  Alidai kuwa mjumbe huyo alimkuta binti huyo mdogo akienda kuchota maji Mto Mbalizi huku akichechemea na kuvuja usaha ambapo baada ya kumhoji ndipo alipopata taarifa hizo za kusikitisha.

  Lakini cha kushangaza mama huyo hakuonesha nia yoyote ya kumpeleka binti huyo hospitalini.

  Baada ya polisi kupata taarifa hizo walimlazimisha kumpeleka hospitali na baada ya kufika huko alidanganya umri akidai kuwa ana miaka 14.

  Mtoto huyo aliendelea kusisitiza umri wake huo na aliyempa mimba ni kaka yake. Hata hivyo, mama anayeishi naye alikanusha taarifa hizo akidai kuwa mimba hiyo alipewa na kijana ambaye yuko mbali kwa sasa.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alipopigiwa simu na gazeti hili kuthibitisha tuhuma hizo alisema yupo kikaoni na atatoa taarifa hizo baadaye leo.

  source:Darleo
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  masikini mdogo wangu hakupewa hata fursa ya kupata elimu ya msingi! inasikitisha na kuuma sana. binti anahitaji maombi na msaada wa haraka sana. kweli wapendwa tunapaswa kubaki zizini mwa kondoo kwani huko nje kuna mbweha na mbwa mwitu wakali sana. lo Mungu tuhurumie na utuhifadhi kwa kadiri ya wingi wa rehema zako
   
 3. Nipigie

  Nipigie Senior Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii inatokana na malezi mabovu. inawazeje kaka mtu afanye mapenzi na dada mtu. Halafu hapa mjini dar utakuta dada na vimaziwa vyake analala na kaka ake kitanda kimoja au deka mooja ila chumba kimoja, kisingizio . uhaba wa makazi.

  Ivi ni kweli kaka na dada moto hauwaki????

  Kama sivyo kwanini tuwajaribu watoto kwa jinsi hiyo.???

  haya ndoo matokeo.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dah siku hizi mivyakula tunayo kula hii kuwa nayo makini
   
 5. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Duh balaa hilo! Kijana ana miaka 18 nadhani ashtakiwe kwa kosa la kubaka..
   
Loading...