Mtoto wa miaka 2½ hataki kula

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,131
3,911
Nina mtoto wa kiume wa miaka miwili na nusu hapendi kula kabisa. Nimempima minyoo na haumwi chochote lakini kula kwake ni kwa shida mpaka umlazimishe. Inaweza ikawa nini?

Nifanyeje arudi tena kama zamani.
 
Hebu naomba kujua ratiba yake ya chakula ulivyomlisha jana na juzi siku nzima, anza na ijumaaa Full diet yake ilikuaje tangu asubuhi hadi jioni kisha Jmos Full diet yake ilikuaje asubuhi to jioni.

Kisha nitajua shida ni wewe au ni mwanao,naomba ratiba ya siku hizo mbili,usisahau kusema mtoto n wa jinsia gani na upo mkoa gani.Asante.
 
Mpeleke kwa daktari wa watoto, ataweza kupewa multivitamins.

Pia usimfungie ndani mwache ajichanganye na wenzie acheze nao .

Ikibidi mpeleke Shule ya baby class akajichanganye michezo ni mazoezi!
 
Mpeleke kwa daktari wa watoto, ataweza kupewa multivitamins.

Pia usimfungie ndani mwache ajichanganye na wenzie acheze nao .

Ikibidi mpeleke Shule ya baby class akajichanganye michezo ni mazoezi!
Miaka 2? Wewe mkuu ulipelekwa kote huko na wazazi wako ukiwa na miaka 2 na nusu?
 
Nina mtoto wa kiume wa miaka miwili na nusu hapendi kula kabisa. Nimempima minyoo na haumwi chochote lakini kula kwake ni kwa shida mpaka umlazimishe. Inaweza ikawa nini?

Nifanyeje arudi tena kama zamani.
Mkuu mpe chips Kuku,,
Hakuna mtoto asiyependa kula,,ni aina gani ya chakula anachopenda,,
Hapo ndy tatizo..
 
Hebu naomba kujua ratiba yake ya chakula ulivyomlisha jana na juzi siku nzima,anza na ijumaaa Full diet yake ilikuaje tangu asubuhi hadi jioni kisha Jmos Full diet yake ilikuaje asubuhi to jioni.

Kisha nitajua shida ni wewe au ni mwanao,naomba ratiba ya siku hizo mbili,usisahau kusema mtoto n wa jinsia gani na upo mkoa gani.Asante.
Akijibu hili la Ratiba na aina ya mlo uniTag pia.
 
Miaka 2? Wewe mkuu ulipelekwa kote huko na wazazi wako ukiwa na miaka 2 na nusu?

Kambaku mtoto wa umri wa miaka 2 na nusu ni umri mzuri tu kwa mtoto kwenda kuchezacheza na kujichanganya!

Huo ni umri wa kawaida ilimradi isiwe mbali na nyumbani.

Halafu kuna sehemu rasmi siku hizi walimu n a wafanyakazi kwenye hizi Shule wamesomea malezi ya watoto wa umri Mdogo kama huo.

Mtoto analelewa kama yuko nyumbani!

Siku hizi hata mayaya wakizungua wamama wanapeleka watoto kwenye hizo Shule kisha wanaenda kazini badae wakirudi wanawapitia watoto wao Shuleni
 
Anakunywa uji asubuhi wa lishe,maziwa fresh yapo wakati wote kwa ajili yake na pia huwa anakula chakula cha pamoja kama ni wali,ndizi,ugali na nyama,maharage,mchicha nk.

Kama ni nyama unaweza anafyonza tu na kutema. Kama ugali kila kitonge na maji.

Hapo ni mbinde mara akimbie mara aingie chini ya uvungu. Anachopenda ni juice ya embe sana sana na vitu vya maji maji kwa hiyo uji na maziwa huwa yapo available wakati wote.

Anaweza akalilia chakula aina flani ukimletea anagusagusa tu.
Hebu naomba kujua ratiba yake ya chakula ulivyomlisha jana na juzi siku nzima,anza na ijumaaa Full diet yake ilikuaje tangu asubuhi hadi jioni kisha Jmos Full diet yake ilikuaje asubuhi to jioni.

Kisha nitajua shida ni wewe au ni mwanao,naomba ratiba ya siku hizo mbili,usisahau kusema mtoto n wa jinsia gani na upo mkoa gani.Asante.
 
Anakunywa uji asubuhi wa lishe,maziwa fresh yapo wakati wote kwa ajili yake na pia huwa anakula chakula cha pamoja kama ni wali,ndizi,ugali na nyama,maharage,mchicha nk...
Rudia kusoma nilichokuomba kisha nijibu upya,najua mtoto anakula vitu tofauti mimi naomba rudia kusoma swali na ombi langu kisha nijibu upya.

Jibu kulingana na nilivyotaka au nilivyouliza mimi,Narudia naomba ratba ya siku mbili za mtoto yani juzi na jana kuanzia asubuhi,mchana,jioni,usiku wakati analala.
 
Miaka 2? Wewe mkuu ulipelekwa kote huko na wazazi wako ukiwa na miaka 2 na nusu?

Halafu hawalazimishi wapelekwe asubuhi asubuhi, wenyewe hata saa 3 saa 4 mtoto anapokelewa!

Ni vizuri mtoto asisumbuliwe kuamshwa alfajiri kisa Eti awahi Shule mtoto wa miaka 2 -4

Ni kwenda kuchezacheza na wenzie na kujichanganya tu!

Wengine inawasaingia mtoto kujifunza kuongea na kuchanganya haraka na kuimbaimba!

Ila iwe karibu na nyumbani ili mtoto asiamshwe asubuhi asubuhi kwa kusumbuliwa eti awahi Shule sababu huo umri mtoto anatakiwa alelewe nyumbani, aachwe aamke kwa wakati wake

Iwe Shule ya mazingira fulani mazuri na isiwe uswazi !
 
Rudia kusoma nilichokuomba kisha nijibu upya,najua mtoto anakula vitu tofauti mimi naomba rudia kusoma swali na ombi langu kisha nijibu upya.

Jibu kulingana na nilivyotaka au nilivyouliza mimi,Narudia naomba ratba ya siku mbili za mtoto yani juzi na jana kuanzia asubuhi,mchana,jioni,usiku wakati analala.
Wacha kumzingua mleta mada huyo ana shida kweli.. Wewe kama una msaada mpe...
 
Bora umenisaidia.Mi ni baba kujua hiyo ratiba mpaka niulize. Na hata hivyo hii tabia ya kutopenda kula ni ya muda mrefu si ya jana na juzi.

Help pls

Nipe muda niko barabarani:Nitakulizia kwa ma professional tiba na makuzi ya watoto... Lakini kiufupi tumia njia ya asili baadhi ya kina Mama wanazijua sana..
 
Mbadilishie vyakula tofauti tofauti .Pia unapomlisha msimjazie chakula kiiiingi mwekeeni kiasi anachokula akianza kusumbua muache...baada ya masaa mawili tena apewe kitu tofauti kama tunda,smoothie ,yoghurt ana juice nzito. Saa ingine mtoto anasumbua sio kwamba hapendi ila inawezekana ameshiba muda huo ama amechoka aina hiyo ya chakula.

Bila shaka mnampa na uji pia.Nashauri awe na aina angalau mbili za uji akizoea mmoja tu anauchoka.So mwamweza mtengenezea lishe na mkamnunulia na oats ama cerelak ili muwe mnambadishia badilishia.

Chakula chake pia unapopika kipike vizuri kiwe na ladha maana nimeshaona sehemu mtoto anapikiwa chakula ila mama akiambiwa kula hawezi kwasabu ni tasteless anakipika kama limchemsho tu.Chakula cha mtoto kinatakiwa kimvutie na kiwe na rangi nzuri kama ni wali utie carrot na njegere. Matunda yakate shapes tofauti etc....pia kuna sahani (zile zenye cartoon) kama hana mtafutie zinauzwa 2500 tu huwa zinawavutia...kwa kuongezea saa nyingine mpeni chakula sawa na wengine kama ni wali, ugali etc.

Kwa kuongezea wakati wa kula usimkabe maana kuna ile mtoto akiwa hapendi kula anabanwa na kufunguliwa mdomo kwa nguvu ndo maana wanaona chakula ni vita...mwekeeni cartoon, imbeni nae au tokeni nje ashangae kidogo huku anakula.
 
Wacha kumzingua mleta mada huyo ana shida kweli.. Wewe kama una msaada mpe...
simzingui nataka kumsaidia ila unaweza kuona kama namzingua,nipo serious sana ila yeye ndio hayupo serious kwasababu hajui ratiba ya mtoto kula halafu anasema mtoto anasumbua kula.

wewe mtu mzima ushindiliwe machakula kila baada ya nusu saa hiyo hamu ya kula utaitoa wapi? tena mavyakula yawe yanakuja kwa fujo bila hata mpangilio unafkiri utapata hamu ya kula?

Mfano mzuri,Jaribu kufululiza wewe binafsi kula wali asubuhi mchana,jioni kwa wiki nzima halafu uone kama utaweza endelea kuwa na hamu na wali ukija mbele yako.
 
Nimeandika kwa uzoefu tu coz na mie mwanangu yupo kwenye age range hiyo.Alikua hapendi kula nikaanza kutengeneza ratiba yake ya chakula na kumbadikishia vyakula vipya kila mara....sasa hivi anakula yani sina wasi wasi hata kama sipo anasimamiwa vizuri tu na anakula naridhika.
Msije mkazoesha zile dawa za kuongeza hamu ya kula maana atakua dependent sio nzuri sana
 
Watoto wengi husumbua kula kwasababu ya ratiba mbaya ya wazazi kwa watoto,kutopangilia aina za vyakula na mara nyingi kumlisha mtoto aina moja ya chakula kila siku.

ukiangalia mtoto tangu akiwa na mwaka m1 alikua anafululizwa Uji uji uji uji uji hivi kwanini huyu mtoto akifika huo umri asianze sumbua kula? wazazi wanashauri kuwa wabunifu sana hasa kwenye vyakula vya watoto.

mtoto hasumbui kula kama hana shida kiafya kama ugonjwa,kama mtoto n mzima wa afya na anasumbua kula shida ni mzazi/mlezi wa huyo mtoto ktk mipangilio ya lishe ya mtoto.
 
Nimeandika kwa uzoefu tu coz na mie mwanangu yupo kwenye age range hiyo.Alikua hapendi kula nikaanza kutengeneza ratiba yake ya chakula na kumbadikishia vyakula vipya kila mara....sasa hivi anakula yani sina wasi wasi hata kama sipo anasimamiwa vizuri tu na anakula naridhika.
Msije mkazoesha zile dawa za kuongeza hamu ya kula maana atakua dependent sio nzuri sana
siri ya mtoto asiependa kula ipo hapa na wala hamna utaalamu ktk hili.
 
Back
Top Bottom