Mtoto wa Liyumba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Liyumba!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ballot, Feb 4, 2012.

 1. Ballot

  Ballot Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SAKATA la Morine Liyumba ambaye ni binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga', linawahusisha vigogo 10 Bongo.

  Vyanzo visivyo na shaka vimelitajia Amani majina 10 ya vigogo ambao wanahusika katika mtandao ambao ndiyo uliokuwa unasafirisha madawa hayo ya kulevya kabla ya kukamatwa na Jeshi la Polisi Tanzania, Lindi.

  Vimedai kuwa mtoto wa Liyumba na vijana wengine waliokamatwa ni ‘dagaa' na kuongeza kwamba ‘papa' wapo, siku wakitajwa taifa litatikisika kwa sababu majina yao ni makubwa na hadhi yao kijamii ipo juu.

  "Hali ni mbaya, inasikitisha kwa sababu taifa linawaheshimu lakini wao ndiyo wahalifu. Wanaendesha mitandao hatari ya kuuza ‘unga'. Vijana ambao ni nguvu kazi wanaharibika na kugeuka mateja kwa sababu yao," kilisema chanzo chetu ambacho kinahifadhiwa jina.

  Chanzo kingine kiliongeza: "Inatakiwa safari hii serikali iwe makini kwelikweli. Imeshaamua, kwa hiyo isisite kuchukua uamuzi mgumu. Hatutaki kuona majina ya watu yanaachwa kwenye hili sakata la kukamatwa kwa mtoto wa Liyumba. Wote wafikishwe mahakamani."

  Amani limetajiwa majina ya vigogo 10 ambao wanadaiwa kuwemo kwenye mtandao uliokuwa unasafirisha madawa ya kulevya kabla ya kukamatwa Lindi wiki iliyopita lakini yanahifadhiwa kwa sababu ya kukwepa kuvuruga upelelezi wa kipolisi.

  Morine, alikamatwa pamoja na mfanyabiashara wa magari, Ismail Adamu au kwa jina lingine, Athuman Mohamed Nyaubi, 28, raia wa Tanzania anayeishi Afrika Kusini.

  Mwingine aliyekamatwa ni dereva, Hemed Said, 27, mkazi wa Mtoni, Temeke, Dar es Salaam na Pendo Mohamed Cheusi, 67, mkazi wa Lindi ambaye ni mmiliki wa nyumba ambayo ilikutwa na madawa hayo.

  Kwa upande mwingine, wananchi waliozungumza na Amani, wamemtaka Rais Jakaya Kikwete adumishe ulinzi kwa Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa.

  Wamesema kuwa Nzowa anapambana na watu wazito ambao wana fedha nyingi lakini kazi yake ina manufaa makubwa kwa nchi kutokana na kitendo cha idara yake kuwaokoa vijana na janga la matumizi ya madawa hayo.

  Nzowa aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa amekuwa akipokea simu mbalimbali za vitisho kutoka kwa watu asiowafahamu kutokana na kazi yake. Alipoulizwa anafanya nini ili kujihami na watu hao, alisema mara nyingi huwa anamtegemea Mungu. "Mimi namtegemea sana Mungu na ndiyo maana mara zote utanikuta nikiwa na Kitabu cha Biblia Takatifu na huwa nasoma Zaburi ya 23."
   
 2. gozo

  gozo JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  udaku..
   
 3. U

  Uwilingiyimana Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  udaku nini sasa...au na wewe ni mmoja wa hao ''dagaa''?
   
 4. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Ni udaku na kama si udaku waandike hayo majina siyo kila siku kuna majina lakini hamyataji.
  La sivyo wakae kimya.
   
 5. j

  jigoku JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Gazeti la Amani
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mkuu wa nchi pia aliwahi kusema kuwa alikuwa anawafahamu ila aliwapa grace-period ya wao kujirekebisha; inaelekea ule muda umepita na hawa jamaa biashara wanaendeleza kama kawa hivyo it is time for the powers that be to act!!
   
 7. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mambo mengi mazito,huanziaga kwenye magazeti ya udaku! Chukulia kama Tetesi, will be confirmed later!!!
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  Majina weken sasa mwaogopa nn tena.
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  jina lenyewe ni gozo,ikimaanisha ananeemeka na madawa hayo
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hivi kuwakamata watu wanaojiushisha na madawa ya kulevya nako ni kuvunja haki za binadamu? kama sivyo mbona Mh Raisi amekuwa kimya sana na majina hayoo?
   
 11. m

  massai JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Vipi wale waliokamatwa mbezi na maburungutu ya hela wameishia wapi?? Alikuwepo mpakistan mmoja au wawili kama sikosei..........

  Itaisha kimya kimya kama zingine 'sijui mzee wa magogini nae anahusika.....!!mbona yupo kimya kama hayupo vile....madaktari wamegoma kimya..madawa yakulevya kimya....
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  Wapo
  mi naanza na........
   
Loading...