Ninaishi kwenye familia ambayo wazazi wamempa nafasi kubwa mtoto wa kwanza Tuseme first born wetu.
Kiukweli hali hii imekuwa ikinikwaza sana hadi niliapa siku nikija kuzaa sitafanya hivi kwa watoto wangu.
First Born wetu ni kama ndo msemaji mkuu wa familia, kila anachosema yeye ni sahihi hataki mawazo wala ushauri hali hii imepelekea mimi kugombana naye muda mwingi.
Kiukweli amekuwa na mchango mkubwa katika familia Yetu hata kuhakikisha sisi Wote tumesimama wenyewe.
Leo hii nimekuwa mkubwa najigemea ila nimejikuta Niko mbali na familia yangu kwa kitendo cha kuchukia dada yetu mkubwa kutaka kuchukua nafasi ya wazazi na kunyenyekewa.
Anaamua kuuza kiwanja anaamua chochote akipigwa hataki na mzazi atamsapoti kwa kila kitu.
Muda mwingi amekuwa na ukaribu na baba name Wanashirikishana Siri zao wenyewe.
Mimi urithi wangu nitaangalia mtoto Yule mwenye akili na mwenye kumiliki vyake. Siwezi mpa mtoto ambae hana chochote maana hachelewi kuuza. Yule mwenye nacho kama angekuwa muuzaji angeuza vyake.
Huwezi ukawa unateseka na Mali za wazazi wako. Wamechuma wao ni haki yao kufanya wanachokihitaji
Huyo dada yako mjanja. Watoto wanaoelewana na baba hula mema ya nchi. Watoto wengi huwa ni wapuuzi kuegemea kwa mzazi mmoja. Ninawashauri watu wote ambao wazazi bado wapo kuwa nao karibu sana hasa baba. Akina baba wana mambo mazito ila huwa wameuchuna tu.