Mtoto wa Kiza Besigye ashinda urais Oxford

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,296
Mwana wa kiume wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye amechaguliwa kuwa rais wa chama cha mijadala chuo kikuu cha Oxford.
Anslem Besigye alikuwa ametengeneza video fupi ya kuomba wanafunzi wenzake wampigie kura.

Mamake Winnie Byanyima amefurahia ushindi wa mwanawe na kuandika kwenye Twitter: “Ameshinda! Anslem amechaguliwa rais wa chama cha mijadala katika bewa lake. Najionea fahari kama mamake.”

Kwenye video aliyokuwa ameitengeneza alikuwa amesimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.

Mwisho wa video mamake Bi Byanyima, alionekana na kusema “huna budi kushinda uchaguzi huu, nimekusaidia sana!”.

Babake Anslem, Dkt Kizza Besigye, amewania urais mara nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni bila mafanikio.


Chanzo: BBC
 
Kama sio viongozi wa afrika kuwa ving'ang'aniz hata baba yake ameshinda chaguzi 2 zilizo pita !!hongera yako naamin iko siku utakuja kuongoza Uganda pia
 
Mtoto wa mwanasiasa machachari nchini Uganda Dr.Kizza Besigye anayemnyima usingizi Rais Museveni ameshinda nafasi aliyokuwa anagombea katika Chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza

Mtoto huyo wa kiume aitwae Anslem Besigye aliwagaragaza washindani wake na kutwaa nafasi ya urais wa mijadala (debate) katika bweni lake

Mtoto wa nyoka ni nyoka,naona Dr.Besigye anamuandaa dogo arithi mikoba yake

Hongera Anslem..!

Source-BBC
 
he! wa bweni? dom leader? au kwa wenzetu ni uongozi wa dom ni mkubwa sana
 
Watoto zao wapo hukoo ... wanasoma kwa raha mustarehee... huku kwetu wanaanzisha mavarangati, wale wanaotegemewa na familia kama waingiza vipato wanakamatwa na watoto wao wanapata shida ya kupata elimu nzuri hata hapa nyumbani.

Unafki huu mpaka lini?!
 
Ameshinda kuwa kiongozi wa mjadala katika "bewa" lake?

Lini wata tweet atakapoenda kujamba chooni kwake?

Mimi nilifikiri mtu kawa rais wa Oxford University.
 
Back
Top Bottom